Wapendwa Wateja wetu!
Kuna Habari zinasambazwa Kwenye mitandao kuhusu tawi la benki ya CRDB Mbagala. Habari hiyo sio ya kweli na tunawaomba wateja wetu na watanzania kutosambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo au hawajui chanzo cha taarifa hizo. Usambazaji wa taarifa za namna hiyo ni kosa kisheria.
Ninawashauri Wateja wetu kutumia kituo chetu cha Huduma kwa Wateja kupata taarifa za uhakika. Kituo kinafanya kazi saa 24 na namba ya kituo ni 0714 197700. Asanteni!
Imetolewa na Idara ya Masoko ya benki ya CRDB