Benki ya Dunia inatarajiwa kuidhinisha mkopo wa $500M kwa Tanzania baada ya Tanzania kutoa utetezi wake

Benki ya Dunia inatarajiwa kuidhinisha mkopo wa $500M kwa Tanzania baada ya Tanzania kutoa utetezi wake

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Bak ya Dunia inatarajia kuidhinisha mkopo wa elimu kwa Tanzania wa dola za kimarekani millioni mia tano ($500M) sawa na pesa za kitanzania Trillion 1.3 ambao ulisitishwa hapo mwezi January 2020 baada ya wanasiasa na wanaharakati kuingilia kati.

Hayo yamejiri baada ya serikali ya Tanzania kwenda kutoa utetezi wake mbele ya wawakilishi wa Bank ya Dunia, ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Prof. Kabudi.

Muwakilishi wa Bank ya Dunia kutoka Marekani kwenye mazungumzo hayo Bi. Jennifer JD Nordquist ameahidi watapitisha huo mkopo hivi karibuni baada ya Tanzania kwenda kueleza na kuondoa sintofahamu iliyokua imejitokeza hapo awali.

Tanzania yatakiwa kuweka mfumo maalum wa elimu ya wanafunzi wajawazito
 
Kwaiyo wanafunzi hawatasitishwa masomo endapo watapata mimba?

Kama sheria ya kukataza mwanafunzi mjamzito asisome ilikua inapingana na haki za binadamu na ndio sababu iliyochangia kuzuiwa kwa mkopo. Basi kama kweli wamedhamilia kutoa mkopo basi lazima serikali imekubali kutengua sheria yake
 
Rudia mudoma udidhanie!
 
1583620847598.png
 
Kwaiyo wanafunzi hawatasitishwa masomo endapo watapata mimba?

Kama sheria ya kukataza mwanafunzi mjamzito asisome ilikua inapingana na haki za binadamu na ndio sababu iliyochangia kuzuiwa kwa mkopo. Basi kama kweli wamedhamilia kutoa mkopo basi lazima serikali imekubali kutengua sheria yake
Sheria zetu ziko wazi juu ya hilo
 
Kutoka Donor cantry,hadi walilia mikopo,na bado si mnaona mabenki yenu yanavyokufa, mmekuja na msamiati mpya,eti benki imeunganishwa.
 
Bado kuna ustahimilivu katka kuzidi kukopa, kukopa na kukopa. Angalizo tu ni kwamba tunapozidi kukopa tunawatwika mzigo mzito watoto na wajukuu zetu ktk kulipa madeni hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo wanafunzi hawatasitishwa masomo endapo watapata mimba?

Kama sheria ya kukataza mwanafunzi mjamzito asisome ilikua inapingana na haki za binadamu na ndio sababu iliyochangia kuzuiwa kwa mkopo. Basi kama kweli wamedhamilia kutoa mkopo basi lazima serikali imekubali kutengua sheria yake
Watabadilishiwa mfumo, hawatatumia mfumo rasmi.
 
Bak ya Dunia inatarajia kuidhinisha mkopo wa elimu kwa Tanzania wa dola za kimarekani millioni mia tano ($500M) sawa na pesa za kitanzania Trillion 1.3 ambao ulisitishwa hapo mwezi January 2020 baada ya wanasiasa na wanaharakati kuingilia kati.

Hayo yamejiri baada ya serikali ya Tanzania kwenda kutoa utetezi wake mbele ya wawakilishi wa Bank ya Dunia, ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Prof. Kabudi.

Muwakilishi wa Bank ya Dunia kutoka Marekani kwenye mazungumzo hayo Bi. Jennifer JD Nordquist ameahidi watapitisha huo mkopo hivi karibuni baada ya Tanzania kwenda kueleza na kuondoa sintofahamu iliyokua imejitokeza hapo awali.

Tanzania yatakiwa kuweka mfumo maalum wa elimu ya wanafunzi wajawazito
Kuna watu wamenuna balaa baada ya kusoma hapa.[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

macson
 
1583652540354.jpeg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye pia anashughulikia masuala ya Afrika Mhe. Tibor Nagy mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Washington,Marekani

Benki ya dunia imeishinikiza serikali ya Tanzania kuanzisha mfumo wa elimu kwa wananfunzi wanaokatiza masomo yao kutokana na sababau kama vile uja uzito.

Ikuzungumza katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi, benki hiyo imesema kwamba inafuatilia kwa karibu maswala yote yanayoendelea nchini Tanzania na kwamba itaendelea kushirikiana na taifa hilo katika maswala ya elimu.

Akizungumza katika mkutano huo mkurugenzi wa benki ya dunia anayeiwakilisha Marekani Dkt. Jennifer "DJ" Nordquist amesema benki hiyo inavutiwa na mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali ya Magufuli katika utoaji wa elimu ya bure kwa shule za msingi na sekondari.

Hatua hiyo inajiri siku chache tu baada ya Benki ya Dunia kuahirisha kupiga kura kuhusu mkopo wa dola milioni 500 kwa Tanzania zilizokuwa zikilenga miradi mbalimbali ya elimu.

Kura hiyo ilikuwa inatarajiwa kupigwa tarehe 28 mwezi Januari , lakini tayari kulikuwa na mgawanyiko mkubwa wa maoni juu ya benki hiyo iidhinishe mkopo huo kwa Tanzania ama la.

Taarifa za kuahirishwa kwa kura hiyo zilijiri siku chache baada ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati wa Tanzania na wa kimataifa waliokuwa wakiitaka benki hiyo isitoe mkopo huo kwa serikali kutokana na kile walichokiita kuwa ni sera na sheria ya elimu ya kibaguzi.

1583652686964.jpeg

Image captionWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akikabidhi ujumbe maalum wa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenda kwa Rais wa Marekani Doland Trump. Anayeshuhudia ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi

Kwa mujibu wa nyaraka za Benki ya Dunia, pamoja na mambo mengine, mkopo huo ulikusudiwa kwenda kusaidia upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi waliokuwa wanarudi shule baada ya kuwa wamepata ujauzito.

Lakini Katika mkutano viongozi hao pia walizungumzia masuala mbalimbali ya miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu mbali na maeneo ambayo Benki hiyo imeisaidia Tanzania aidha kwa mikopo ya masharti nafuu au misaada ikiwa ni pamoja na ujenzi na uendelezaji wa shule za msingi na sekondari.

1583653107354.jpeg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Dunia anayeiwakilisha Marekani Dkt. Jennifer "DJ" Nordquist katika makao makuu ya Benki ya Dunia Washington,Marekani.Nyuma ya Prof. Kabudi ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani

Mkurugenzi Mtendaji mbadala wa Kanda Namba 1 ya Afrika kutoka Benki ya Dunia Bw. Taufila Nyamadzabo amesema mazungumzo baina ya Tanzania na benki ya dunia yamekuwa ni ya manufaa kwa kuwa yameondoa sintofahamu iliyokuwepo kati ya pande hizo mbili na kwamba mradi huo utapitishwa na bodi ya benki ya dunia hivi karibuni.

Mkopo huo uliotarajiwa kutolewa na Benki ya Dunia ulitarajiwa pia kugharamika wanafunzi wajawazito kupitia elimu mbadala na si katika mfumo rasmi.

Swala hilo lilizua utata na kuwasukuma wanaharakati wa Tanzania kuiandikia bodi ya utendaji ya Benki ya Dunia ikiwa benki hiyo itaipa Tanzania mkopo huo, kabla ya nchi hiyo haijaahidi kuondoa sera na kipengele cha sheria kinachowakataza wanafunzi wa kike kurudi shuleni baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN la nchini Marekani, hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kuahirishwa kwa kura hiyo japo inaripotiwa kuwa uongozi wa benki hiyo ulifanya kikao cha dharura na wanaharakati wa haki za binaadamu kutoka Tanzania na mashirika ya kimataifa .

Sheria ya elimu ya Tanzania imebeba kipengele cha nidhamu ambacho kinaipa mamlaka uwezo wa kuwafukuza shuleni wasichana wanafunzi wanaogundulika kuwa na ujauzito.

Hatahivyo hatua yetu ya kumtafuta mwakilishi wa benki hiyo nchini Tanzania kutoa tamko lake haikufua dafu

1583653462145.jpeg

Image captionWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (aliyevaa tai nyekundu) Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi

Kutoka Donor cantry,hadi walilia mikopo,na bado si mnaona mabenki yenu yanavyokufa, mmekuja na msamiati mpya,eti benki imeunganishwa.
Dona contries kubwa zote wana madeni, hakuna nchi isiyokopa labda Brunei.
Saudia wenyewe wanakopa na utajiri wote wa mafuta walio nao.
 
Dona contries kubwa zote wana madeni, hakuna nchi isiyokopa labda Brunei.
Saudia wenyewe wanakopa na utajiri wote wa mafuta walio nao.
Wanakopa ili kuendeleza walichonacho, na siyo kuanzisha.umeona wamarekani wanakopa pesa kwa ajili ya mashimo ya vyoo vya wanafunzi au madawati au kujenga barabala au kujenga vyumba vya kusomea watoto.
 
Mpaka hapo umenikatisha tamaa kujadili na wewe, unataka kulinganisha changamto na vipaumbele vya mataifa mawili ambayo moja (USA) limetimiza karibu miaka 350 au 400 ya kuwa huru na lingine (Tanzania) lina miaka 60 ya uhuru?
Au moja (UK) lina miaka zaidi ya 600 ya uhuru na lingine (TZ) lina miaka 60?

Unajua kama nchi masikini sana kama Cuba ilikuwa inakopa pesa kuwekeza kwenye afya kiasi cha kushika nambari moja duniani kwa baadhi ya huduma za afya? Iliipita Marekani na nchi zote za Ulaya kwenye maeneo flani.

Kwanini haikukopa kuwekeza kwenye mambo ambayo Marekani ilikuwa inawekeza?
Sababu vipaumbele na changamoto ni tofauti.
 
Back
Top Bottom