The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
- Thread starter
- #101
Huduma za afya za mama kujifungua bado ni shida ndio huduma ya kuwasaidia watoto waliobakwa itakuwepo?Huko kooote kuanzia, QT, Private Candidate, nk mbona wamejaa wanafunzi wazazi wanasoma bila shida na wanafanya vizuri tu? Kuna Ulazima gani wa kuwachanganya na wale ambao hawajaamua kuwa wazazi? Tabia "chafu" ni contagious, sio vizuri kuchanganya haya makundi japo sio wote walichagua kuzalishwa wengine walibakwa!(waliobakwa kuna njia za kuwakinga na mimba wakiwahi kwenye huduma za afya)
Watu mnaandika vitu kama vile Tanzania imebadilika na kua Marekani.
Hoja kwamba kuwachanganya watoto wenye mimba na wasio na mimba itasababisha watoto wasio na mimba kutamani kua na mimba ni hoja ya hovyo sana na inatolewa na watu wasiotumia akili kufikiri. Kwani watoto wanaishi Dunia yao peke yao hawaoni watu wenye mimba hadi watakapowaona shuleni watatamani kua na mimba pia?
Hoja ya kuwafukuza watoto shule kisa wana mimba ni hoja ya hovyo sana. Nchi jirani na sisi kama Kenya, Malawi, n huo ujinga haupo mbona hatuoni watoto wote wamepata ujauzito?
Kua na watu wasiofikiri na ukawapa nafasi ya kuongoza nchi haya ndio matokeo yake.