Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Tayari ushaharibu majadala.unabisha bisha tu kama juha
Kwa hivyo ukiongea lugha ya kashifa na matusi ndio hoja yako inakuwa na nguvu?
Hivi unadhihirisha uwezo mdogo wa kujenga hoja na ukosefu wa hekima, unadhihirisha ulipata malezi duni.
Kuonesha ukomavu na akili kubwa unaweka hapa ushahidi wa maandishi ya wapi serikali ilikopa pesa kulipa mishahara bajeti ya 206/2017, 2017/2018, 2018/2019.Uwe unasoma bajeti, makusanyo, matumizi ya mishahara, matumizi ya malipo ya madeni ya nyuma na matumizi mengine kabla ya mikopo uone kabla ya mikopo hua tunajitosheleza kwa asilimia ngapi.
Ukifanya hivyo ndio unaeleweka kirahisi sio kwa kutukana au kukashifu watu.
Akili ndogo ya kukimbilia matusi, kejeli, na kashifa ndio ujuha.
Kama taarifa za kibunge zipo kwenye kumbukumbu za vitabu vya michango ya bungeni lazima zipo kwenye tovuti, wewe weka rejea link yake hapa, taja kabisa na kifungu kipi au ukurasa wa ngapi.
Tena unaweza na kuweka screeshot kabisa kunikomesha nisiongeze hata neno kukubishia.
Si unataka kunifundisha jinsi ya kupinga hoja basi nioneshe kwa mifano weka ushahidi wa nyaraka, au viambatanisho vya kufanyia rejea hoja yako.
Maneno matupu na hisia zako siyo ushahidi wa tuhuma au hoja zako.