Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

Hawajataja mkoa hapo😋, songea hiyo elfu Saba unatumia kufanya nn, elfu 3 tosha kabisa...maisha mazuri
Songea chakula cha kueleweka kinaanzia elfu 3. Bado wapo sahihi.
 
Hawalipi kodi labda makato kwenye mauzo ya pamba. Kodi wanailipaje au wanalipa nini, hawana biashara yoyote.

Naona uhamini lakini iko hivyo.
Hakuna jamii inayolima pamba watu hawalipi kodi, labda ungezungumzia Wahadzabe. Tatizo la Watanzania wengi wanafikiri kodi ni ile inayolipwa directly tu, VAT ni kodi inayolipwa na walaji wa mwisho bidhaa na huduma, tozo na ushuru ni kodi pia.
 
 
Hakuna jamii inayolima pamba watu hawalipi kodi, labda ungezungumzia Wahadzabe.
Vile vijiji havina zahanati, kuna shule msingi basi. Hakuna umeme wala maji ndio wanaambiwa watapata awamu ijayo rea bado wanapima, na maji mbunge anashughulikia.
Hata josho la mifugo hakuna kijijini.
 
Wanajua kuwa Tanzania ina watu wanaotumia hicho kiasi kwa mwezi?
Wanawapa jina gani?
 
Nimesema kodi ipo kwenye kuuza pamba tu, lakini sijaona kodi nyingine yoyote.
Jamii zinazolima pamba zinajulikana vizuri sana, walishavuka kiwango cha barter trade mahitaji yao mengi kama sio yote wananua cash, wanatumia magari na bajaji kwa wingi sana sio hata punda. Kwa kuanzia tu mbegu, dawa na mbolea za pamba wanafuata kwa bodaboda au magari na wanalipa cash.
 
Jamii zinazolima pamba zinajulikana vizuri sana, walishavuka kiwango cha barter trade mahitaji yao mengi kama sio yote wananua cash, wanatumia magari na bajaji kwa wingi sana sio hata punda.
Ok sawa,
 
Vile vijiji havina zahanati, kuna shule msingi basi. Hakuna umeme wala maji ndio wanaambiwa watapata awamu ijayo rea bado wanapima, na maji mbunge anashughulikia.
Hata josho la mifugo hakuna kijijini.
Shule na zahanati sio lazima viwepo kijijini, vinaweza kuwepo kwenye kata nyingine au wilayani. Umeme na maji hakuna sehemu nyingi tu Tanzania na huo ndio umaskini wenyewe unaozungumziwa wa watu kuishi kwa vibatari na maji ya madimbwi.
 
Kwa tusio na magari wala pikipiki binafsi, weka gharama za usafiri za siku, vocha, umeme, maji ,kodi ya nyumba na chakula ukijikuta uko chini ya dola tatu staafu🤣
 
Shule na zahanati sio lazima viwepo kijijini, vinaweza kuwepo kwenye kata nyingine au wilayani. Umeme na maji hakuna sehemu nyingi tu Tanzania na huo ndio umaskini wenyewe unaozungumziwa wa watu kuishi kwa vibatari na maji ya madimbwi.
Sasa hao watu wanalipa kodi lwa kipato gani?
 
Sasa hao watu wanalipa kodi lwa kipato gani?
Hiyo buku 2 wanayutumiwa na watoto wao mjini kwa M-pesa wakitoa inakatwa kodi,
Sukari robo wanayonunua ina VAT, buku 2 ya boda wanayolipia kama nauli kwenda kuchukua mbegu za pamba ina kodi ya mafuta ndani yake, mafuta ya kibatari na sabuni vina kodi.
 
Hahaha unajua huelewi unalazimisha iwe hivyo, nikasema sawa.

Pamba tunatumia mbegu tunazotunza kila mwaka.

Sukari ya nini kule?

Boda inaishia vijiji vya jirani.
 
Hahaha unajua huelewi unalazimisha iwe hivyo, nikasema sawa.

Pamba tunatumia mbegu tunazotunza kila mwaka.

Sukari ya nini kule?

Boda inaishia vijiji vya jirani.
Hizi ni fiction, nilifikiri hiko kijiji kweli kipo, uliharibu uliposema wanalima pamba🤣, vijiji vinavyolima mazao ya biashara pure, barter trade walishaachana nayo kabisa, kijiji wanacholima pamba haki fit hypothetical zako kabisa. Labda ungesema hicho kijiji wanalima hata uwele na ulezi.
 
Mimi natumia 1,500/=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…