The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Bank ya Dunia imeahirisha kupiga kura ya kuikopesha Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za kimarekani milioni 500 sawa na shilingi trillioni 1.3 za kitanzania kwa ajili ya kufadhili elimu.
Kama mnakumbuka Benki ya Dunia ilikuwa ipige kura wiki hii kuamua kama iikopeshe Tanzania au la kutokana na sheria ya kuwanyima watoto wa kike waliopata mimba haki ya kusoma, Serikali ikaahidi kuwa imeandaa njia mbadala wa hao watoto kupata elimu ila sio katika shule za umma, na hata Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Kabudi jana tarehe 27 kwenye kuapisha mabalozi na mawaziri aligusia hilo neno na kuwalaumu baadhi ya wanaharakati na wanasiasa kupotosha nia ya serikali.
Wanaharakati na wanasiasa kadhaa wa Tazania waliaandika barua Benki ya Dunia kuitaka kusitisha mkopo au kuinyima Tanzania mkopo kwakuwa Tanzania ina sera za ubaguzi kwenye elimu kwa watoto wa kike wanaopata ujauzito hivyo haistahili kupewa mkopo.
Benki imeamua kusitisha ama kuahirisha kujadili hilo jambo hadi hapo baadaye. Jana Mheshimiwa Rais alisema Benki ya Dunia watatoa pesa kwa kuwa wanajua msimamo wa Tanzania.
Je, Benki imesikiliza maoni ya wanaharakati na wanasiasa ama ina sababu zake nyingine?
Soma hapa👇.
edition.cnn.com
BARUA YA CSOs:

World Bank delays vote on $500 million loan for Tanzania after activist pressure over ban on pregnant schoolgirls | CNN
The World Bank has postponed its decision on granting Tanzania a $500 million loan, following pressure from activists who oppose the country's policy of banning pregnant girls and young mothers from attending state school.
BARUA YA CSOs: