Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Unachoandika wala hakieleweki kwa sababu unapinga hoja zangu lakini maelezo yako unakubali hoja zangu.

Lazima uelewe kuwa kujibu hoja siyo muhimu kama hujui mantiki ya kile unachokijibu otherwise utakuwa unajaza saver tu za Jamiiforums with garbage and hocus pocus!

Samahani kama nitakukwaza!
Hujanikwaza kwa sababu nimegundua hujanielewa au hutanielewa kwa vile unatumia moyo kufikiria mambo badala ya ubongo.
Fikiri kwanza jambo ndio ulipende sio unapenda kwanza kufikiri baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usizungumze bila kutafakari.

Tuna sheria kali juu ya wanaume wanaofanya mapenzi na wanafunzi. Na kimsingi tunasema kuwa wanaume hawa wamewabaka wasichana wanafunzi.

Kwa hiyo suala halipo kama wewe unavyoliweka. Ni upotoshaji mkubwa.

Msichana akionekana ana mimba, anatafutwa aliyempa. Aliyempa atakabiliwa na kosa la ubakaji. Akithibitika, adhabu ni jela miaka 30.

Mwanafunzi akijifungua, aendelee na masomo, na wala halitakuwa darasa lile alilokuwemo maana wale wenzake watakuwa walishalimaliza darasa hilo.

Sasa kama kutakuwa na wanaume punguani, wa kuendelea kutaka kuwabaka wanafunzi ili waende jela miaka 30, wataendelea. Lakini nina imani hata kama wasichana waliopata mimba wataendelea na masomo, siyo kweli kuwa mimba zitaongezeka. Maana hakuna mwanaume nwenye akili timamu atakayefurahia kwenda miaka 30 jela.
Kama serikali inahitaji sana huu mkopo basi ikubali masharti kuwa watoto wakipata mimba na kuzaa warudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi ambao hawajapata mimba na kuzaa kama ambavyo wanaharakati na baadhi ya wanasiasa kama Zitto wanavyotaka!

Yaani, msichana akijisikia kupata mimba anapata na kuzaa halafu baadaye anarudi tena kwenye darasa lake na kuendelea na masomo pamoja na wanafunzi wengine!

Hili suala sio rahisi kama ambavyo baadhi ya washabiki wa wanasiasa wanavyoshangilia ndio maana CHADEMA wameamua kukaa kimya kwa sababu wanajua ugumu wake kijamii na kiimani ya dini!
 
Hizo ndio sababu za delays
IMG_20200128_075308.jpeg
IMG_20200128_075349.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujue mambo mengine ya kijinga sana.
Mimi sioni sababu ya kuwakataza kurudi shule. Maana mimba inakaa miezi tisa alafu anajifungua.lakini kumkataza asirudi shule ina maanisha unamnyima haki yake ya kupata elimu..


Sent using Jamii Forums mobile app
nawza pata wapi majina ya hawa wanafunzi wanyonyeshao na wajawazito? mie katika shule yangu nimeamua kutenga darasa maalumu la wanaonyonyesha na wajawazito, nitawawekea na chekechea kwa ajili ya watoto wao, nataka nione hawa wabinti wataendeleaje
 
Bams,
Tusicheleweshe maendeleo, kwanza hao wanafunzi wanyonyeshao wako wangapi? nipeni majina yao nitawadahili katika shule yangu binafsi na watasoma bure, hii agenda inataka kukuzwa tu bila sababu.
 
Bams,
Kwa hiyo hizo sheria kali zimepunguza mimba za utotoni? Nope!

Nimesema suala la mimba za utotoni ni mjadala mpana sana katika jamii yetu ambayo mila na desturi bado ni sehemu ya maisha!

Ni ukweli kuwa wazazi wengi hawataki watoto wao wasome darasa moja na wasichana ambao wamejifungua.

Ni ukweli kuwa Tanzania bado ni conservative country wakati Banki ya Dunia ina sera za uliberali.
 
MsemajiUkweli,
Hivi Tanzania toka mwaka 1961 Kuna musicians amewahi kusoma shule ya umma akiwa analea?Mnisaidie mie sijui au kwa kuwa nimesoma boys schools from form one to six ndo maana sijui? Otherwise msaidieni magufuli ajue si kila kitu kinafaa kwa kiki za kipuuzi kwenye majukwaa ya kisiasa.

Kuna vitu vya kusema na kuna vitu havihitaji kusemwa hadharani na kama koromeo lake halina chujio au kifua chake ni kidogo basi either ajizuie kuongea ongea sana kama alivyoamua kutuepushia aibu taifa kwa kujizuia kusafiri kwenda Ulaya na marekani,hiyo ikishindikana 2020 atuachie nchi yetu kwa hiari kama kweli ni mtanzania mzalendo
 
Mi sioni sababu kwa nini tukope kwa ajili ya elimu. Elimu ni kitu ambacho hatutakiwi kikinasibisha na mikopo ya mabeberu. Katika makusanyo yetu kipaumbele cha kwanza ili kugharamia elimu ili tuepukane na kumtegemea beberu kwenye kulipia elimu yetu.

Mara milioni tukope tununue ndege lakini siyo elimu
 
GUSSIE,
Naungana na hoja yako mkuu,sasa kilichomfanya Magufuli atakupigia kelele hadharani ilikuwa ni nini,wakati yeye akiwa mwalimu na baadae waziri for 20 years hakuwahi kuona watoto waliokifungua wakirudi shule ,aliwashwa na nini? au aliona hao waliokuwa wakitekeleza sera hiyo bila kupiga makelele hawakuwa marais Jiwe?huyu mtu hatufai
 
Mtoto akipewa mimba kuwepo na special schools za wazazi ambazo ni private kama walivyofanya juvenile courts. Wasichanganyikane na wenzao ambao ni fresh.

Na kitendo cha mtoto kupata mimba kinafutia validity ya kuitwa mtoto. Ngumu ku exercise haki za mtoto maana keshakuwa mzazi. Apambane na hali yake maana alipovua chupi alijua kabisa kuwa madhara yake atavimba juu.Tusiendekeze ujinga.
Mkuu haki ya elimu haiwezi kufutwa kwa kushika mimba.Kushika Mimba hakumfanyi mtoto apoteze haki ya kupata elimu.Naamini kabisa kwamba sio tatizo iwapo mtoto huyu ataruhusiwa kusoma baada ya kuzaa.Jambo la muhimu ni kutoa elimu ya kutosha juu ya uzazi wa mpango,ngono na afya salama.Pili ni kuweka utaratibu wa namna ambayo watoto hawa wataweza kuendelea na masomo ikiwamo kwa mfumo wa aina tofauti ya elimu kama vile mfumo wa elimu ya watu wazima(QT) .Jambo la muhimu ni kuhakii=kisha kwamba mabinti zetu wanapata elimu come rain or sunshine
 
Back
Top Bottom