Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

hakuna kitu kibaya kama kutokua na msimamo katika maisha, tukirusu wanafunzi wenye mimba kuendelea na masomo maana yake tukakua tunarusu uasherati kwa wanafunzi. sijui kama watu wanaangalia madhara ya hii kitu kwa mda mrefu ujao. tukikosa msimamo tukakubali tutaletewa na ushenzi mwingine wa viongozi wawe mashoga ndo tupate misaada. lazima ifike wakati tuwe na mipaka kwenye maisha yetu
 
Mkuu haki ya elimu haiwezi kufutwa kwa kushika mimba.Kushika Mimba hakumfanyi mtoto apoteze haki ya kupata elimu.Naamini kabisa kwamba sio tatizo iwapo mtoto huyu ataruhusiwa kusoma baada ya kuzaa.Jambo la muhimu ni kutoa elimu ya kutosha juu ya uzazi wa mpango,ngono na afya salama.Pili ni kuweka utaratibu wa namna ambayo watoto hawa wataweza kuendelea na masomo ikiwamo kwa mfumo wa aina tofauti ya elimu kama vile mfumo wa elimu ya watu wazima(QT) .Jambo la muhimu ni kuhakii=kisha kwamba mabinti zetu wanapata elimu come rain or sunshine
Na aliyefeli mtihani hana haki ya kupata elimu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimi unaponza kichwa....zamani mtoto alipokuwa anapata mimba akiwa shuleni tulikuwa hatauhangaiki naye..kwa kuwa haukuwa utamaduni wetu wa mtoto kubeba mimba kisa akaingia darasan basi mtoto huyo alikuwa anajiondoa mwenyewe shuleni bila hata kufukuzwa...na hata ingebainika akiwa shuleni basi alikuwa anaadhibiwa kimya kimya mambo yanaenda.....songombingo lilianzia pale amabapo Rais Magufuli aliutangazia ulimwengu kuwa yeye hasomeshi wajawazito..ulimi umeponza kichwa...leo wanaandamwa wapinzani kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo umenena! Tatizo ni huyu kiongozi wetu ni mropokaji sana. Tangu enzi za Nyerere wanafunzi waliopata mimba walifukuzwa ama wao wenyewe walijitoa kimya kimya. Mataifa yote na mashirika ya kimataifa yalifahamu hilo lakini hayakutilia maanani kwani ilionekana kama siyo sera ya nchi! Sasa baada ya kiongozi wetu mkuu kutangaza rasmi wakaona isiwe shida wakachukua hatua. Matokea yake tumebaki kulaumiana na kulialia hovyo! Wacha tule jeuri yetu!
 
Naona hapa ni siasa ambazo hazina misingi yoyote, miaka yote mwanafunzi akipata mimba anasimamishwa kuendelea na wenzie, na siyo mimba tu hata ukijurukana unajihusisha na mapenzi walikuwa wasimamishwa kwa mda kama adhabu, kama hilo halitoshi familia nyingi mtoto wa kike/mwanafunzi akipata mimba wanamwambia aondoke nyumbani aende alikoipata mimba.

Sasa iweje saizi serikali ibebeshwe mzigo wa kusema inawanyanyapaa waliopata mimba wakati wewe mwenyewe mtoto akija na mimba unamkana hapo nyumbani kwako.

Naungana na serikali mwanafunzi aliyepata mimba asimamishwe kuendelea na darasa akasome darasa la wakubwa.

Wakiruhusiwa haohao wanaharakati wataanza kudai haki za huyo mtoto kuwa karibu na mama yake matokeo yake huko mbele tutaanza kuandaa madawati yenye sehemu ya kukaa mama na ya kukaa mtoto akisubiri kupata huduma kwa mama yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GUSSIE, Mimi sikubaliani na haya mambo ya kuwapokea shuleni watoto ambao tayari wamezaa ama wajawazito.

Sababu ni hii.
Jukumu la kumtunza mtoto ni la mzazi, wakati mama zao wako shule, mtoto wake atatunzwa na nani???

Kuna kosamoja naliona hapa Rais Magufuli alikuwa na sababu gani ya kuliongelea hadharani ikiwa hakutaka kuwasomesha wasichana/wazazi?

Mkuu angenyamaza mambo yangejiendea na mkopo tungepewa ilivyo kawaida.

Namuomba mkuu asiwe anazungumzia kila jambo kwa sababu baadae nchi haitafaidika na kauli zake za kibabe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hata sielewi si juzi tu Mzee alisema anahela nyingi za kuendesha nchi miezi zaidi ya sita bila tatizo sasa mikopo ya nn tena? Kama hawataki basi tuachane nao sisi ni matajiri sana
 
Yaani hata sielewi si juzi tu Mzee alisema anahela nyingi za kuendesha nchi miezi zaidi ya sita bila tatizo sasa mikopo ya nn tena? Kama hawataki basi tuachane nao sisi ni matajiri sana
Tuko vzr mkuu.
Screenshot_2019-12-21-09-59-03-1.jpeg


dodge
 
Nafkiri jamaa wameshtukia hizo pesa zingukuja yatajiriha hayo mafisisiem....na kupeleka kuwanyayasa wapinzani kwenye uchaguzi .

Nasema hivi
.. WB kamateni hapohapo...msiachie.

Tunyooke wote. Tusagie meno wotee.
 
Hili Tatizo sio dogo wala la kisiasa. Kabla hatujawazuia watoto kusoma shule kwa mimba tuangalieni vyanzo vya mimba utotoni. Tumekuwa na jamii ambayo ni wepisi kulaumu watoto bila kulaumu mila za kizamani na zisizo na maendeleo sehemu nyingine.

Kuna jamii wanaruhusu watoto waolewe wakiwa wadogo sasa serikali hiyo hiyo inasema lazima mtoto asome na serikali hiyo hiyo inasema huwezi kusoma na mimba. Hatutaweza kutatua matatizo kama serikali inafumbua macho mila zetu hasa vijijini. Pili hili Tatizo Vilevile ni la nafasi watoto wa masikini tu ndiyo wataahidwa kusoma.

Ni lazima tuweke sheria ngumu lakini mila zingine nazo tusiziache tu. Hebu tuonyesheni wangapi walio jela kwasababu ya mimba za utotoni!
Mkuu hapo umenigusa. Mazingira ya watoto wetu ktk kupata elimu siyo rafiki. Hapo nazungumzia umbali wa shule zetu za sekondari za Kata. Umbali ule unachangia sana watoto wetu kujikuta wakikumbana na vishawishi kwani wanapotoka shuleni hadi nyumbani huwachukua hadi saa tatu hadi nne kufika.

Niwape mfano. Siku moja asubuhi ya saa 12 natoka mnjini Arusha kwenda nchini Kenya kwa usafiri binafsi kupitia barabara ya Namanga. Nilipofika eneo liitwalo Sakina karibu na machinjioni niliwakuta wanafunzi wa sekondari na walinisimamisha kwa nia yakuhitaji lifti. Nilisimama na kuwapakia niloweza kuwabeba kulingana na uwezo wa gari langu. Niliwahoji sana lkn kifupi ni kwamba walipangiwa shule moja ya sekondari iliyopo sehemu wanaita Oldonyosambu. Ni kama km 10-15 kutoka nilikowapakia. Je wakati wa kwenda kama mkikosa gari mnafanyaje? Wakasema wanarudi majumbani. Je wakati wa kutoka shule mkikosa mnabaki shuleni? Hapana tunalazimika kutembea.

Kwa mazingira hayo mtoto hata kama ni wa kwako kweli akipata ujauzito tena ya mpita njia yaani dereva wa lori la mizigo utamhukumu binti yule kweli?? Hapo sijasema kila mtoto anaepata mimba basi ni mazingira hapana bali nimejaribu kuwekea msisitizo kwenye kujua nini hasa chanzo cha mimba kisha ndipo hatua zichukuliwe.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaowapa mimba wanafunzi wanapewa adhabu gani? Especially kama ni wanafunzi pia,,dhana ya kwamba binti ajitunze mpaka amalize shule imepitwa na wakati na kinachotakiwa ni elimu ya ngono salama.

Watoto wakibalehe wanakua sexually active lakini hawapewi elimu ya ngono salama pamoja na uzazi wa mpango especially matumizi ya condom . Hatua zinatakiwa zichukuliwe kabla mabinti hawajabeba mimba,pia kama akijifungua arudi shule bila vikwazo.

Kuwalaumu mabinti kwamba wanaendekeza umalaya badala ya kusoma ni ujinga wa hali ya juu kwa sababu wanawake wana shawishiwa,rubuniwa na wengine ni wahanga wa ukatili wa kingono . Msimamo wa serikali hauko sahihi na watu wapaaze sauti zao mpaka kieleweke,hatuhutaji wazungu ili kutambua kwamba tuna tatizo la kisera .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wanafanya ngono na wala tusijifanye hatulijui hilo,bora waelimishwe jinsi ya kujilinda maisha yaendelee.
hakuna kitu kibaya kama kutokua na msimamo katika maisha, tukirusu wanafunzi wenye mimba kuendelea na masomo maana yake tukakua tunarusu uasherati kwa wanafunzi. sijui kama watu wanaangalia madhara ya hii kitu kwa mda mrefu ujao.. tukikosa msimamo tukakubali tutaletewa na ushenzi mwingine wa viongozi wawe mashoga ndo tupate misaada. lazima ifike wakati tuwe na mipaka kwenye maisha yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom