Kama serikali inahitaji sana huu mkopo basi ikubali masharti kuwa watoto wakipata mimba na kuzaa warudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi ambao hawajapata mimba na kuzaa kama ambavyo wanaharakati na baadhi ya wanasiasa kama Zitto wanavyotaka!
Yaani, msichana akijisikia kupata mimba anapata na kuzaa halafu baadaye anarudi tena kwenye darasa lake na kuendelea na masomo pamoja na wanafunzi wengine!
Hili suala sio rahisi kama ambavyo baadhi ya washabiki wa wanasiasa wanavyoshangilia ndio maana CHADEMA wameamua kukaa kimya kwa sababu wanajua ugumu wake kijamii na kiimani ya dini!