Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Ulimi unaponza kichwa....zamani mtoto alipokuwa anapata mimba akiwa shuleni tulikuwa hatauhangaiki naye..kwa kuwa haukuwa utamaduni wetu wa mtoto kubeba mimba kisa akaingia darasan basi mtoto huyo alikuwa anajiondoa mwenyewe shuleni bila hata kufukuzwa...na hata ingebainika akiwa shuleni basi alikuwa anaadhibiwa kimya kimya mambo yanaenda.....songombingo lilianzia pale amabapo Rais Magufuli aliutangazia ulimwengu kuwa yeye hasomeshi wajawazito..ulimi umeponza kichwa...leo wanaandamwa wapinzani kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app

Yani haya mambo yalikuwa kimya kimya yanajisolve yenyewe hakukuwa na tatizo lolote na wachache ninaowajua baada ya kujifungua walitafuta shule nyingine na waliendelea,kweli mdomo huponza kichwa [emoji87]
 
Nchi yetu imesharasimisha ujinga. Hivi kuna shida gani mtoto aliyejifungua kurudi shule na kuitafuta elimu?
Sad kwamba karne ya 21 bado tuna watu wenye mawazo kama haya. Wengi humu ni wazazi. Leo hii mtoto wako akipata mimba ana miaka 15 utamuacha akae nyumbani? Wengi tutawapeleka hata shule za maana Zaidi.

Ninajua kigogo aliyepeleka mtoto kwa Trump baada ya kupata uja uzito bongo. Endeleeni kuwandanganya hao hao wapiga kura wasiojielewa. Wengine tulifuta ujinga kwa hisani ya Mwalimu Nyerere!

Ndugu au Raia mjinga ni mzigo wa familia na taifa!
 
Black Mirror,
Umeandika nilichotaka kuandika. Hivi ni tangu lini mtoto wa kike alipata ujauzito nchi hii na akaendelea na masomo katika mfumo rasmi, miaka na miaka binti akibainika tu ni mjamzito yeye mwenyewe anajiengua kimya kimya au anasimamishwa kimya kimya wala hakuna lawama wala kelele, sasa mheshimiwa yeye akaona awashtue mabeberu hahahaaa!
 
Masanja,
Ndio huo utaratibu mbadala uwepo ila kwa gharama za mzazi sio za serikali! Hamna aliyekataza mtoto kupata elimu.
 
Masanja,
Ndio huo utaratibu mbadala uwepo ila kwa gharama za mzazi sio za serikali! Hamna aliyekataza mtoto kupata elimu.

Kiongozi tutake tusitake kuna vitu haviepukiki. Kwa yeyote aliyekwenda shule, anajua kabisa Tanzania (viongozi wetu) wanapigana "loosing battle". Tena nikwambie sasa...Ameanza WB usije shangaa hii kitu inasambaa kwa mashirika mengine. Tanzania (ukiacha maneno wanasiasa wanayowaaminisha wale wenye akili fupi kama zao), hatuna jeuri ya kuwagomea donors (read western countries).

Hii sera ya watoto wa kike haijaanza jana. Lakini tawala zilizopita zilijua namna ya kula na kipofu. Ulikuwa hujawahi kumsikia Mkapa au Kikwete anautangazia ulimwengu kwamba tunaenda kufanya hili au lile. Ilikuwa ni domestic policy but very much passive. Hata hao wanaharakati wanajua. Hata mimi najua-wewe unajua- kwamba miaka yote Tanzania ukipata uja uzito..you go home!

Kinachotukwamisha ni jinsi gani viongozi wetu wanapenda kujimwambafai. Kuropoka.

Hivi mfano issue ya ushoga. Najua kabisa wengi humu (wengi) hatuupendi ushoga. By the way hata western countries wapo ambao hawapendi hii kitu. Lakini ni nchi gani Zaidi ya Makonda na wenye akili kama zake CCM, walishaenda kuutangazia ulimwengu kwamba tunakwenda kuwasaka na kuwatia jela hawa jamaa?

In all matatizo mengi ya Tanzania..ni ya kijinga na tunayatafuta wenyewe. Tunachokisahau kwa maksudi, wanaharakati wana nguvu sana kuliko hata serikali zetu. Na hata huu mkopo, nchi wanachama wa Benki ya Dunia wangependa waipe pesa Tanzania lakini..wataficha sura zao wapi? Na tusisahau...hizi pesa tunapewa za wahisani ni kodi za watu hata hao hao mashoga tunaotaka wakaozee jela! Go figure!

Its a reality check. Serikali iwe makini na matamshi ya viongozi wake. Lakini kikubwa tujue kwamba dunia imebadilika. Tunategemeana. Unaweza kumchagua Rafiki, lakini huwezi kumchagua jirani! ni kanuni ya Maisha! Mwisho wa siku jirani ndo wa muhimu Zaidi. wenye akili tunaelewana.

Mwisho wa siku kama maskini huwezi kumsaidia zawadi kubwa ya kumpa "leave him/her alone)!
 
Bams,
Kwa hiyo hizo sheria kali zimepunguza mimba za utotoni? Nope!

Nimesema suala la mimba za utotoni ni mjadala mpana sana katika jamii yetu ambayo mila na desturi bado ni sehemu ya maisha!

Ni ukweli kuwa wazazi wengi hawataki watoto wao wasome darasa moja na wasichana ambao wamejifungua.

Ni ukweli kuwa Tanzania bado ni conservative country wakati Banki ya Dunia ina sera za uliberali.
Jambo la kujiuliza, hii conservatism yetu imekuwa na faida au hasara? Kama ina faida tuendelee kuikumbatia. Lakini kama ina hasara kwetu kama Taifa au kwa jamii au kundi fulani, basi ni lazima tuipige vita, sawa na tunavyopiga vita ukeketaji. Nayo iwekwe kwenye mila potofu.

Mila au conservatism inayotakiwa kuenziwa ni ile tu inayotusaidia kama jamii.

Binadamu, kila mmoja, wakati fulani, hufanya makosa. Na ukikosea, ukajutia, unaweza kubadilika, na baadaye ukafanya mambo makubwa.

Wanaopata mimba wakiwa mashuleni, wanatakiwa kupewa mafunzo maalum ili kuwafanya watambue uhalisia na ubaya wa kile walichokifanya kwenye muda usio sahihi. Lakini wapewe nafasi tena kusoma.
 
Hakimu Mfawidhi,
Ha ha ha haaa nacheka kwa dharau,
Hawa bank ya Dunia wasitutishe kwanza walitubania zile za barabara ya ubungo, hatubabaika na tukapeta na mambo yako poa.

Sasa hili la elimu pia tunawaambia WASITUPANGIE KWENYE SERIKARI YETU YA AWAMU YA 5,
Ukiskia mabepari ndio hawaaa
 
Hivi donors kantri ndio ilishakufaga.. 😂😂😂 nchi inavituko hii sijawahi ona kwakeli.
 
Hakimu Mfawidhi,
Asante sana Benki ya Dunia kwa kuushtukia ulaghai wa CCM wa kutafuta fedha za kuvurugia uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020. Kwanza muelewe kuwa fedha hizi hazijaidhinishwa na bunge; ni fedha za dili kama zile za Kange Lugola. Tatizo maCCM wanafanya kazi kwa kuviziana kama mafisi pori. Fisi pori wakigawana nyama ikiisha wanaanza kugawanana wenyewe kwa wenyewe....wanamtafuta aliye dhaifu kati yao wanamla nyama. Hii ndio misingi ambayo maCCM hufanya kazi.

Jamani msipende kudandia mambo. Ukimsikiliza vizuri Zitto Kabwe hapo chini utagundua kuwa CCM wanafanya ujanja wa kupata fedha za kugawana na kushinda uchaguzi. Hapa hakuna mkopo zaidi ya ushenzi. Mkopo huu sio kwa ajili ya watanzania bali ni kwa ajili ya CCM ilhali riba ya mkopo italipwa na watanzania wote waliomo CCM na wasiokuwamo. Kama mnataka mkopo huu upite, basi yawekwe masharti kwamba watakaolipa riba ya mkopo wawe ni wanaCCM tu na sio watanzania wote. Hatuwezi kukubali kubebeshana mzigo kwa maslahi ya kikundi kidogo cha wachumiatumbo wachache katika nchi hii. Never ever!!!

 
Kama serikali inahitaji sana huu mkopo basi ikubali masharti kuwa watoto wakipata mimba na kuzaa warudi tena kwenye darasa lenye wanafunzi ambao hawajapata mimba na kuzaa kama ambavyo wanaharakati na baadhi ya wanasiasa kama Zitto wanavyotaka!
Hii hoja ya wajawazito imetumika tu kama cover, naona kuna mengi ndani!
 
Wakuu, habari
Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza, serikali ya JMT imeomba mkopo wa USD 500M kutoka WB kwa ajili ya kuboresha elimu.

Serikali hii hii ndiyo inayonunua ndege kwa "cash" ilhali ingeweza kukopa ndege hizo.

Ndege ni investment, na JPM Mara zote amekuwa akituambia kuwa biashara ya ndege inalipa na mpaka Sasa imeshaingiza faida kubwa sana. Na hapa ndipo nnapopendekeza serikali ya awamu ya tano iingie kwenye maajabu ya dunia. Kama ndege ni investment inayolipa, kwanini tusikope ndege kwa kuwa itajilipia deni halafu pesa za ndege ziende kuboresha elimu?

Hesabu zilikuwa nyepesi Sana. Kopa kwenye investment tumia cash kwenye matumizi ya kuboresha elimu.
 
herzegovina,
Nauliza tu.... kwani huwezi kutumia cash kui-invest (mfano; kwenye ndege) kisha baadaye ukatumia cash uliyopata kwenye investment kama matumizi mf.kuboresha elimu......?
 
Faiza maana ya "postponed" kwa lugha ya WB hiyo ajenda haina sifa ya kujadiliwa.

Kwa uhalisia nchi hii imekosa sifa ya kukopeshwa.
 
Yaani, msichana akijisikia kupata mimba anapata na kuzaa halafu baadaye anarudi tena kwenye darasa lake na kuendelea na masomo pamoja na wanafunzi wengine!
Kumbe wasichana hupata mimba kwa sababu "wanajisikia"?
Hii unaamini kweli kile unachoandika?
Si kwa sababu wanabakwa, au hawakufundishwa kuhusu miili yao ?

Unaamini kweli itabadilisha kitu kama mmoja anafukuzwa darasani? Wengine hawako tena hatarini kubakwa?

Na nchi ambako wasichana hawafukuzwi kuna kuongezeka kwa mimba?(namba zote nilizoona ni kinyume)
 
Back
Top Bottom