Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Tsh. Trilioni 1.2 za Miradi ya Maji na Afya

Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Tsh. Trilioni 1.2 za Miradi ya Maji na Afya

Mikopo itatutokea puani!
Yaani
msaada wa jumla ya dola za Marekani 29.93 milioni (Sh68.78 bilioni)
10% ya👇
Sh689.51bilioni ambao ni mkopo wa masharti nafuu

mkopo wa Dola mil. 560 sawa na shilingi Trilioni 1.
zitatutoka....puani puani

Billioni 68 Shilingi kwa mkopo wa Trillioni 1 Shilingi na takribani nusu yake 680 billioni Shilingi ndiye yenye masharti nafuu!
kwa msaada wa 68 billioni Shilingi. Msaada ambao hauna masharti maalum. Lazima nijigonge kichwa.
 
Tunakopa na muda huo huo hatukusanyi mapato ipasavyo.

Hivyo vijisenti vinaweza patikana hapa hapa tukiwa serious.
 
Siku watanzania tukijitambua tutapiga hatua kubwa
 
Hii nchi ni kama haina mwenyewe make na raia tushageuka kuwa mashabiki wa wapigaji, kwamba mkopo wa WB unaenda kufanya kazi ya usafi wa mazingira vijijini, aisee inachekesha sana kuhuzunisha sana.

Nchi inaliwa sana hii na mbaya zaidi sisi raia tunashangilia ila hii mikopo haitalipwa na Mwigulu wala Samia wala Majaliwa bali ni sisi choka mbaya ndio tutapandishiwa bei ya vitu kulipa hii mikopo.

Haiingii akilini kwamba hizo pesa zipo zitakazoenda vijijini kuboresha usafi wa mazingira.

Screenshot_20230228_220118.jpg
 
Kazi inaendelea,

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania na Wizara ya Fedha Kupitia Waziri Mwigulu zimesaini mkopo wa Dola mil. 560 sawa na shilingi Trilioni 1.3.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa ni kwamba mkopo huo ni kwa ajili ya Miradi ya Maji na Afya ya mama na mtoto.

====

View attachment 2532628View attachment 2532629

Wizara ya Fedha na Mipango, imesaini mikataba wa miwili na Benki ya Dunia (WB), yenye thamani ya Sh1.264 trilioni kwa ajili ya kuboresha huduma endelevu za maji, usafi wa mazingira vijijini pamoja na afya ya mama na mtoto.

Mkataba huo umesaini leo Jumanne Februari 28, 2023 kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, Mkurugenzi Mkazi wa WB, Nathan Belete na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Amour Suleiman Mohamed.

Dk Nchemba amesema mkataba huo umekwenda sambamba na msaada wa jumla ya dola za Marekani 29.93 milioni (Sh68.78 bilioni) zitakazotekeleza miradi hiyo kwa mustakabali wa maendeleo ya Watanzania.

"Mpango endelevu wa maji na usafi wa mazingira vijijinj utapokea Sh689.51bilioni ambao ni mkopo wa masharti nafuu wa IDA, eneo la mradi wa afya ya mama na mtoto litapokea Sh574.59 bilioni," amesem Dk Nchemba.

Belete amesema WB inajisikia faraja kuisadia Tanzania katika kuboresha sekta hizo ikiwemo ya afya ili kuhakikisha Taifa hili linafikia malengo yake hasa kuwezesha huduma bora ya afya ya mama na mtoto.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema fedha hizo zitaboresha huduma za afya mama na mtoto, pamoja na ujenzi wa vituo vya upasuaji sambamba na kuwajenga uwezo watumishi wa kada ya afya.

Naye, Dk Mohamed amesema fedha hizo zitaleta mabadiliko katika sekta ya afya Zanzibar hasa katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto visiwani humo vinavyotokana na changamoto za afya
Mama na madilu wake wanazidi kutuingiza kwenye madeni. Hivi siku hizi hakuna miradi tunaweza bila kukopa? Awamu ya 5 benki ya dunia hawakutupenda maana tulitaka mikopo kwa miundombinu ya kimkakati ya reli na bwawa la nyerere na kadhalika, wakati wao hawajapanga tanzania tufanye miradi kama hiyo. Ila kwa miradi hii ya maji ambapo hela inapigwa na vigogo na makandarasi uchwara hela wanatoa kirahisi. Zamani miradi ya maji walikua hata hawajengi ila ubabaishaji na kula hela ya umma tu huku nchi inabakiwa na deni benki ya dunia.
Wengine tulisema siku nyingi kwamba benki ya dunia inafanya biashara kama beni zingine isitoshe kwa miaka mingi ni mkono wa nchi za kibeberu. Wanakukopesha kwa miradi fulani tu ambapo wawekezaji kutoka nchi zao watafaidika kwenye uwekezaji wao.
 
Hii nchi ni kama haina mwenyewe make na raia tusha geuka kuwa mashabiki wa wapigaji, kwamba mkopo wa WB unaenda kufanya kazi ya usafi wa mazingira vijijini, aisee inachekesha sana kuhuzunisha sana.

Nchi inaliwa sana hii na mbaya zaidi sisi raia tunashangilia ila hii mikopo haitalipwa na Mwigulu wala Samia wala Majaliwa bali ni sisi choka mbaya ndio tutapandishiwa bei ya vitu kulipa hii mikopo.

Haiingii akilini kwamba hizo pesa zipo zitakazo enda vijijini kuboresha usafi wa mazingira.View attachment 2533055
Vipi mkuu, una wasiwasi gani? Unaona hiyo miradi sio sahihi au kukopa hiyo fedha sio sahihi au Miradi lengwa sio ya kipaumbele katika jamii? Au ni nini hasa hoja yako.
Hebu funguka zaidi.
 
Tatizo hujaimgia kiundani ukajua inakuwaje. Iko hv hiyo fedha inaenda kuboresha Mambo matatu.
1. Ushambazaji wa maji vijijini. Kwanini maji? Kwa sababu kama Hamna maji Hamna usafi kwenye taasisi na kaya zetu hususani kwenye ishu ya sanitation
2. Uboreshaji miundombinu ya vyoo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kwenye Shule za msingi
3. Uboreshaji wa hali ya usafi kwenye taasisi za elimu na afya. Lakini lazima ujue huu mpango hautafaidisha wote kwa kiwango sawa kwenye halmashauri zetu Bali Halmashauri zitakazokuwa na watendaji wenye bidii kutimiza vigezo vya uboreshaji hiyo miundombinu na usambazaji wa maji ndio watakaovuna fedha kwa ajili ya kupanua huduma. Yaan unavuna kwa kadri utakavyo perform. Kwa uchache ndio hvyo
 
Kongole mkuu kwa ufafanuzi muafaka.
 
Ifike mahali tujue kwani nchii hii kipaombele ni kipi?
 
Tatizo hujaimgia kiundani ukajua inakuwaje. Iko hv hiyo fedha inaenda kuboresha Mambo matatu.
1. Ushambazaji wa maji vijijini. Kwanini maji...
Hivi hiyo #2 ninyi ccm huwa hamsikii aibu kuitaja?

Yaani dunia ipo 21 century lakini ninyi hela ya kuboresha vyoo tena vya sehemu muhimu kama hospital mnaandika kabisa proposal kwa mzungu mpewe hela ya kwenda kuvikarabati,nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba huwa mnaandika kweli dhumuni la matumizi ya hizo hela then muweke sababu hizo.
 
Watu mlioko mijin mna dharau sana sisi watu wa vijijin kwa hiyo kuboresha usafi vivijin haiwezekan? .au wewe usafi kwako unadhan nini? kufagia barabara.Usafi vijijin maana yake uboreshaji ya makazi vivijini.Sio taa za barabaran zinafaa kwenu mijini hata sisi tunaitaji pumbavuuu weeeee
 
Hivi hiyo #2 ninyi ccm huwa hamsikii aibu kuitaja?

Yaani dunia ipo 21 century lakini ninyi hela ya kuboresha vyoo tena vya sehemu muhimu kama hospital mnaandika kabisa proposal kwa mzungu mpewe hela ya kwenda kuvikarabati,nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba huwa mnaandika kweli dhumuni la matumizi ya hizo hela then muweke sababu hizo.
Kwahyo tuache watoto wetu wajisaidie vichakani?
 
Huo mustakabhali, ndio 10%?
Je hayo ni maendeleo au 'man'-endelea?

I read between the lines
A carrot and a stick approach.
Kijiji gani wanapeleka maji!,Mwanza ipo karibu na Ziwa Viktoria lakini mitaani maji hamna!
 
Back
Top Bottom