Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Tsh. Trilioni 1.2 za Miradi ya Maji na Afya

Naungana na wewe katika hili. Hii mikopo hailengi kwenye uzalishaji wa kutukwamua kiuchumi mbeleni bali kutukwamisha kwa kuwa mzigo mkubwa wa madeni huko mbeleni bila kuwa na uwezo wa kulipa kwa kuwa hailengi kwenye kuongeza uzalishaji bali ulaji (consumption) Mikopo inayolenga kwenye uzalishaji ndiyo itatusaidia mbeleni, mfano inakwenda kwa wawekezaji wa uzalishaji katika kufungua mashamba makubwa ya kilimo, kupanua umwagiliaji, viwanda vya uongezaji wa thamani mazao yetu n.k. Huu mkopo hautaleta tija! World bank, kwa matakwa ya wakubwa, wanajua wanachokifanya! Sisi tunajitambua kujua aina ya mikopo inayotufaa? Afya ya mama na mtoto inatushinda nini? Mazingira vijijini maanake nini, kupanda miti kunahitaji mkopo wa world bank? Nipisheni 🚶🚶
 
Tunahitaji mkopo wa benki ya dunia kuboresha usafi? ...🚶🚶🚶
 
Unajua accessibility ya maji Rural na Town Kwa Sasa au unaropoka tuu?
 
Akili Yako wewe inajua uzalishaji ni kwenda shambani tuu..

Bila maji ya uhakika huo uzalishaji hasa wa viwanda utatoka wapi? Utakuwa unasubiria masika?
 
Kukopa siyo tatizo, tatizo ni kule kupokea taarifa za CAG zikibaini upigaji kwenye fedha za mikopo na kuyapuuza mapendekezo yake. Anyway mbuzi wa bwana heri nisisahau CAG kweli nae analipwa kwa fedha hizohizo anazoo-odit asante.
Pesa ya mkopo sio sawa na pesa ya Halmashauri,hii ni mikopo specific kwenye miradi na inafanyiwa monitoring na mkopeshaji imf/wb
 
Ukiambiwa na nani na wapi kwamba zimemaliza matatizo? Leta ushahidi
 
Mikopo ni mizuri hasa kama ina masharti nafuu...ila awamu hii wapigaji ni wengi balaa kitakachofika kwa wananchi ni % 50 yaani pasu kwa pasu kudadek!.
73% ya deni la Nchi yetu ni mikopo ya masharti nafuu yaani consessional
 
Hakuna anayeandika proposal za vyoo Bali hivyo vyoo ni sehemu ya component ya mradi.

Kwani wewe choo unakichukuliaje mbona kama unapata shida sana.
 
Hakuna anayeandika proposal za vyoo Bali hivyo vyoo ni sehemu ya component ya mradi.

Kwani wewe choo unakichukuliaje mbona kama unapata shida sana.
Napata shida kwa sababu mimi mwenyewe muhangaikaji mwananchi wa kawaida nimejenga nyumba yenye vyoo viwili ndani na bafu na bado nikajenga choo kingine nje.

Kijijini nako nimejenga the same kama mjini ila sijawahi hata mara moja kukopa ila viongozi wa taifa wanaojipambanua kwamba watatuvusha kwenye lindi la umaskini wanaenda kwa wazungu kukopa hela za kujenga vyoo!!!inakuingia akilini hii?yaani waziri alipoenda kusaini huo mkataba alienda na V8 ambayo ukipiga hesabu ya bei yake kuinunua itajenga vyoo vya kutosha mkoa mmoja.

Hovyo kabisa na ni aibu!
 
Wewe unahusumia familia serikali inahudumia jamii,hayo ya V8 sijui nini hata wakiacha kununua Changamoto hazitakwisha ,Taja Nchi walikomaliza Changamoto.
 
Akili Yako wewe inajua uzalishaji ni kwenda shambani tuu..

Bila maji ya uhakika huo uzalishaji hasa wa viwanda utatoka wapi? Utakuwa unasubiria masika?
Umechangia jambo hili kwa uwezo wako mzuri! 🚶🚶
 
"Mpango endelevu wa maji na usafi wa mazingira vijijinj utapokea Sh689.51bilioni ambao ni mkopo wa masharti nafuu wa IDA, eneo la mradi wa afya ya mama na mtoto litapokea Sh574.59 bilioni," amesem Dk Nchemba.
Hayo maneno ndiyo yanatumika kutupotezea mwelekeo mwisho wa siku wanatupiga
 
Chonde Chonde Pesa Zisijetoka Kwa Watu Wa Upinde Wa Mvua Ikawa Heka Heka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…