Benki ya Dunia yajitoa Rasmi Kufadhili Mradi wa REGROW Kwa Madai ya Ukiukwaji wa Haki za Wananchi Wanaozunguka Hifadhi ya Ruaha

Benki ya Dunia yajitoa Rasmi Kufadhili Mradi wa REGROW Kwa Madai ya Ukiukwaji wa Haki za Wananchi Wanaozunguka Hifadhi ya Ruaha

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Kwa mujibu wa taarifa ya Oakland Institute kama ilivyonukuliwa na MongaBay ni kwamba Wananchi wa eneo la hifadhi ya Ruaha walipeleka malalamiko Benki ya Dunia Kisha kufunguliwa Kwa kesi Kwa manyanyaso waliyofanyiwa na maafisa wa TANAPA ikiwemo kuporwa mifugo Yao kwenye zoezi la kutaka kupanua eneo la hifadhi ya Ruaha ambapo zaidi ya wana Vijiji 21,000 wangepoteza Makazi Yao pamoja na Mali nyingine.

World Bank cancels $150m tourism project in Tanzania after abuse claims World Bank cancels $150m tourism project in Tanzania after abuse claims

Benki ya Dunia wamethibitisha hili: Factsheet on Tanzania’s REGROW project and next steps

Swali:
Yaani Kituo Cha Haki za Binadamu Tanzania na TLS hawaoni haya Ili wawasaidie Wananchi Hadi Wazungu ndio waje? Au hizo taasisi wenyewe kwao Wanasiasa wa CHADEMA ndio wanastahili Huduma zao pekee? Pre GE2025 - LHRC watoa tamko: Wataka Haki ya dhamana ya Dkt. Slaa Isihujumiwe

Mradi wa REGROW ulikuwa ni ufadhili wa Benki ya Dunia wa $150mln( Takribani Bilioni 350) uliolenga kukuza Utalii hifadhi za Kusini.

Soma zaidi hapa Kamati ya Bunge Yaridhishwa na Mradi wa REGROW Hifadhi ya Taifa Ruaha

My Take:
Kama taarifa hii ni kweli basi naishauri Serikali kama inataka kuongeza Ukubwa wa eneo la hifadhi ya Ruaha iwahamishe Wananchi Kwa Staha kama wanavyofanya huko Ngorongoro badala ya kuwafurusha.

Ngorongoro wanahamishwa kaya pamoja na mifugo Yao ,wanalipwa fidia na wanapewa maeneo,Kwa nini wasifanye hivi Ruaha?

Aidha Serikali iwachukulie hatua Askari wa TANAPA ambao walishiriki kuwatendea ndivyo sivyo Wanavijiji Hadi kutufikisha hapa Kwa kukosa weledi.

Pia soma Benki ya Dunia Yatoa "Ultimatum" ya Siku 30 Kwa Tanzania Kumaliza Mgogoro wa Ukiukwaji wa Haki za Binadamu kwenye Mradi wa Regrow
 
Endeleeni kuomba mapambio ya kumsifu mama Abdul, kwa mahakama za Tanzania hata TLS wangefungua kesi unafikiri wangeshinda?
Kwa nini wasishinde? Walifingua kesi wakashindwa?

Hao ni wapuuzi tuu kazi Yao ni kutetea Machadema hawana maana kabisa kulipwa mishahara na Serikali.

CCM na Rais ndio aliwatuma Game Rangers wa TANAPA wawafanyie mambo yasiyofaa Wananchi?
 
Kwa nini wasishinde? Walifingua kesi wakashindwa?

Hao ni wapuuzi tuu kazi Yao ni kutetea Machadema hawana maana kabisa kulipwa mishahara na Serikali
Rejea kesi ya DP world pamoja na kwamba kesi haikufunguliwa na TLS lakini waliofungua wkikumbwa na misukosuko mbalimbali, kesi ya polisi dhidi ya utekaji na bado utekaji unaendelea.
 
Kwa nini wasishinde? Walifingua kesi wakashindwa?

Hao ni wapuuzi tuu kazi Yao ni kutetea Machadema hawana maana kabisa kulipwa mishahara na Serikali.

CCM na Rais ndio aliwatuma Game Rangers wawafanyie mambo yasiyofaa Wananchi?
Kwani Machadema siyo matanzania?.
Kumbuka vyama vya siasa vinapita tu, ila Tanzania itadumu..Tumia akili.
 
Kwanza kule wale si askari wa game, game ni tawa, wale ni tanapa. Pili hakuna askari nchi hii anafanya mambo kama hayo bila orders kutoka ngazi za juu. Wamepokea command
wanatekeleza
Hiyo ishu ina baraka za viongozi waaay back
Orders kutoka ngazi za Juu ni Kisingizio,Kwa nini wasifanye kazi Kwa weledi?
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Oakland Institute ni kwamba Wananchi wa eneo la hifadhi ya Ruaha walipeleka malalamiko WB Kisha kufunguliwa Kwa kesi Kwa manyanyaso waliyofanyiwa na maafisa wa TANAPA ikiwemo kuporwa mifugo Yao kwenye zoezi la kutaka kupanua eneo la hifadhi ya Ruaha ambapo zaidi ya wana Vijiji 21,000 wangepoteza Makazi Yao pamoja na Mali zingine.
World Bank cancels $150m tourism project in Tanzania after abuse claims World Bank cancels $150m tourism project in Tanzania after abuse claims

Swali.
Yaani Kituo Cha Haki za Binadamu Tanzania na TLS hawaoni haya Ili wawasaidie Wananchi Hadi Wazungu ndio waje? Au hizo taasisi wenyewe kwao Wanasiasa wa Chadema ndio wanastahili Huduma zao pekee?

Mradi wa REGROW ulikuwa ni ufadhili wa Benki ya Dunia wa $150mln( Takribani Bilioni 350) uliolenga kukuza Utalii hifadhi za Kusini.

My Take
Serikali kama inataka kuongeza Ukubwa wa eneo la hifadhi ya Ruaha iwahamishe Wananchi Kwa Staha kama wanavyofanya huko Ngorongoro badala ya kuwafurusha.

Ngorongoro wanahamishwa kaya pamoja na mifugo Yao ,wanalipwa fidia na wanapewa maeneo,Kwa nini wasifanye hivi Ruaha?

Aidha Serikali iwachukulie hatua Askari wa TANAPA ambao walishiriki kuwatendea ndivyo sivyo Wanavijiji Hadi kutufikisha hapa Kwa kukosa weledi.

Pia soma Benki ya Dunia Yatoa "Ultimatum" ya Siku 30 Kwa Tanzania Kumaliza Mgogoro wa Ukiukwaji wa Haki za Binadamu kwenye Mradi wa Regrow
Hawa wazungu waonevu tu hawa... Mkuu isijekua Lissu Kashaanza kutuharibia maana waheshimiwa waliridhika kabisa na mradi huu...

Lissu Nahisi Hatufai Ameshaanza Mambo Yake..
 
Kwa nini wasishinde? Walifingua kesi wakashindwa?

Hao ni wapuuzi tuu kazi Yao ni kutetea Machadema hawana maana kabisa kulipwa mishahara na Serikali.

CCM na Rais ndio aliwatuma Game Rangers wawafanyie mambo yasiyofaa Wananchi?
Machadema ni kitu gani ndugu. Nikukumbushe tu kuwa vyama vya kisiasa vipo vipo kwa mujibu wa sheria na katiba ya JMT. Ndio maana vimepewa usajili na mamlaka husika baada ya kutimiza masharti yaliwekwa kwa mujibu wa sheria ya vyama. Jipe muda utafakari walau kidogo
 
Kwa hiyo kazi ya TLS na Kituo Cha Haki za binadamu ni kutetea Machadema tuu si ndio?
 
Hawa wazungu waonevu tu hawa... Mkuu isijekua Lissu Kashaanza kutuharibia maana waheshimiwa waliridhika kabisa na mradi huu...

Lissu Nahisi Hatufai Ameshaanza Mambo Yake..
Mradi ulikuwa suspended na uchunguzi ulikuwa unaendelea so Hadi Kamati inaongea hayo mradi ukoshanza utekelezaji na ukifikia hatua hizo.

Hii ni taarifa ya January mwaka huu 2025 na hiyo ya Kamati ni ya mwaka Jana.
 
Back
Top Bottom