Benki ya Dunia: Zaidi ya dola milioni 680 zimewekwa na watanzania katika mabenki ya kigeni kutokana na kuongezeka kwa mikopo na misaada kutoka nje

Benki ya Dunia: Zaidi ya dola milioni 680 zimewekwa na watanzania katika mabenki ya kigeni kutokana na kuongezeka kwa mikopo na misaada kutoka nje

hata bitcoin sijui inafanyaje kazi, kuna watu mnapenda sana kuamini uongo

Zitto ulitwambia unayo list ya watu walioficha pesa nje sasa ni wakati wako kuiweka hadharani sasa na benki ya dunia wamekusaidia sasa wataje
 
Ukuku huu Kuna baadhi yetu hapa tumekuwa wachangiaji tu wa hela za wenzetu zimewekwa mara huku Mara kule sisi hatuna,nimechoka kujadili wenye mihela nami nayataka hayo mahela nijadiliwe mwe!!!!
 
mimi binafsi sheria ya money laundering kwangu huwa naiona ujinga mtupu

pesa mabilioni zikitoka nchi zetu kwenda kwao sio money laundering wanazipokea wanaziweka kwenye benki zao ziimarishe uchumi wao

Za kwao zikija kwetu tunakomaliwa hadi tukome kuwa ni za money laundering au lazima tuzitolee maelezo

Mungu angenipa uraisi kitu cha kwanza ningefanya ni kuifuta sheria ya money laundering na pili mtu hata awe na mabilioni ya pesa akileta toka nje sihangaiki kumhoji hata kama kabeba kwenye kiroba

hawa watu wanatuchezea sana wanatufanya sisi migambo wa kuwalindia pesa zao zisiingie hovyo kwetu wakati zetu hawatulindii zisiingie hovyo kwenye benki zao.

to hell with money laundering laws
Umeandika kwa hisia kali sana. Sisi ndiyo nimekuwa wajinga tunatumia Sheria ya AML kuwatesea wakosoaji.
 
Back
Top Bottom