- Thread starter
-
- #161
Tatizo la Afrika siyo wachina wala wazungu ni viongozi wetu wenyewe, tusitegemee mchina wala mzungu aje Afrika kutusaidia never kuja kwao ni kutafuta faida ya ziada na kuipeleke kwao.Aliwahi. Alipotujengea TAZARA tukashindwa kuiendesha sisi wenyewe.
Aliwahi, mChina wa wakati huo alitusaidia katika mapambano ya kulikomboa bara letu.
Tuwazungumzie hawa waChina wa leo.
Lakini hata wao mimi siwalaumu sana maanake hata wakitugonga wanafanya hivyo kwa upuuzi wetu wenyewe.
Nalaumu sisi wenyewe tusiopenda kubadilika. Tunabaki kuwa kama watoto tuuu miaka nenda miaka rudi! Ni vipi hatuwezi sisi wenyewe kujua zuri au baya mpaka tuambiwe na wengine?
Ni vipi tukubali kuingia kwenye mikataba tunayojua haina faida kwetu? Haya ndiyo maswali tunayotakiwa kuwauliza viongozi wetu na sisi wenyewe. Tuache kuhamishia lawama kila mara kwa wengine. Tunajionyesha kuwa kama mazuzu vile.
Tusipoanza kubadilika sisi wenyewe kifikra na kimitazamo na kuwa na viongozi wazalendo haswa wanaopenda nchi zao na watu wao Afrika itaendelea kuwa bara la mataifa mengine kuja kujichumia.