Benki ya Exim ya China kuichukua bandari ya Mombasa endapo Kenya itashindwa kurejesha mkopo iliochukua ili kujenga reli ya kisasa (SGR)

Benki ya Exim ya China kuichukua bandari ya Mombasa endapo Kenya itashindwa kurejesha mkopo iliochukua ili kujenga reli ya kisasa (SGR)

Aliwahi. Alipotujengea TAZARA tukashindwa kuiendesha sisi wenyewe.
Aliwahi, mChina wa wakati huo alitusaidia katika mapambano ya kulikomboa bara letu.

Tuwazungumzie hawa waChina wa leo.

Lakini hata wao mimi siwalaumu sana maanake hata wakitugonga wanafanya hivyo kwa upuuzi wetu wenyewe.

Nalaumu sisi wenyewe tusiopenda kubadilika. Tunabaki kuwa kama watoto tuuu miaka nenda miaka rudi! Ni vipi hatuwezi sisi wenyewe kujua zuri au baya mpaka tuambiwe na wengine?

Ni vipi tukubali kuingia kwenye mikataba tunayojua haina faida kwetu? Haya ndiyo maswali tunayotakiwa kuwauliza viongozi wetu na sisi wenyewe. Tuache kuhamishia lawama kila mara kwa wengine. Tunajionyesha kuwa kama mazuzu vile.
Tatizo la Afrika siyo wachina wala wazungu ni viongozi wetu wenyewe, tusitegemee mchina wala mzungu aje Afrika kutusaidia never kuja kwao ni kutafuta faida ya ziada na kuipeleke kwao.

Tusipoanza kubadilika sisi wenyewe kifikra na kimitazamo na kuwa na viongozi wazalendo haswa wanaopenda nchi zao na watu wao Afrika itaendelea kuwa bara la mataifa mengine kuja kujichumia.
 
Ile MIKATABA 17 ya enzi za jamaa iliyoandikwa kichina mnajua ilizungumzia nini?,yawezekana sisi ni PART OF CHINA MAINLAND sasa hivi
 
Kujenga miundombinu ni kazi ya serikali dunia nzima, sgr wapi utapata mwekezaji ? Ndege ya taifa duniani kote kila nchi INA shirika lake na ni wajibu ili kuuza Utalii au tukubali watalii wapitie kwa wenzetu.
JPM inabidi tumpongeze kwa sababu hata sisi Wachina walishatuingiza mkenge kwenye sgr na bandari ya Bagamoyo, ni JPM aliyepangua akasema tutajenga kwa pesa yetu, kiukweli wengi hatumuelewa sasa ndio akili zimeamka tumeelewa kwa nini alifutilia mbali mikopo ya Wachina.
Lakini najua kwa sababu ya unafikiri wa watz na siasa uchwara za kipuuzi wengi hatuwezi kumpongeza kwa hilo ila ukweli ndio huo JPM katuokoa kutoka makucha ya Wachina
Mengine sawa lakini hilo la kuendesha wenyewe kwetu mtihani. Tumeshuhudia reli ya kati, reli ya tazara na ATC yenyewe.

Wenyewe tukiendesha haya mashirika na reli zitakuwa chalikama ya awali.

Haya yange binafsishwa tu kwa masharti ya kuyaendesha kwa kazi iliyokusudiwa.
 
ATCL hakuna mkopo pale zote zimenunuliwa kwa pesa taslimu na ile SGR Dar-Dodoma pesa ya ndani kama utakumbuka Mh Rais alisemaga kuwa alijaribu kutafuta mkopo lakini mashariti aliyo kapewa yalimshinda akabidi aje ajitutumue yeye na wananchi wake na ndiyo hile inajenga sasa
Mkuu humu JF watu wanafki sana...hata kama Rais wetu ana mapungufu kwenye kweli na sifa zake yapaswa apewe.

Nilitegemea nikute comment kama yako mwanzoni kabisa ili kuonyesha utofauti Wa SGR ya Kenya na SGR ya Tanzania.
 
Kwa Kenya hihiii ya Ukuru Kenyata kipenzi cha wana chadema?
 
Hata sisi hii mikopo itatuumbua tu

Hii miradi mbali na kuongeza deni la Taifa,ukweli ni kwamba hailipi na zaidi ni mzigo tu kwa hizi serikali zetu.

Hii miradi ingeachiwa private sector au serikali ingekuwa na hisa kidogo lakini sio kuimiliki na kuiendesha hii miradi kwa asilimia 100.

Niwaambie tu,SGR na ATCL ni mizigo tutakayoibeba kwa kodi zetu.

Tumekuwa mateka wa fahari ya macho na kupuuza uhalisia-mtu mmoja kwa kutumia cheo na madaraka yake kawafanya watu mazuzu wasione mbele.

Watu wanashangilia na kusifu wakati mikataba inafanywa siri na wala hawajiulizi!!
Pessimistic, prayer of doom, wakatishaji tamaa, etc watu design yako, mnaoona negatives tu, hamkosekaniki, unfortunately huwa mnashindwa.
 
Reli ya Tazara imepita Selou kwa sehemu kubwa ...waliuwa Tembo kibao...Tembo walikuwepo zaidi ya laki tatu sasa hivi aibu
Tembo wamepunguwa kwa tamaa zenu za mano yao si kwa akili reli imepita. Ulisikia lini treni imegonga tembo?
 
Hayo ndo manufaa ya mikopo isiyo na masharti.
Mtu mwenye nia njema lazima akuulize itarudishaje mkopo? Mfano benki hawawezi kukupa mkopo bila kuangalia financial statement yako.

Wale wakopeshaji wa mtaani akijua una nyumba au gari anakupa pesa tena kwa muda mfupi huku akikuandikisha mkataba wa kwamba umemuuzia, nia ya wakopeshaji wa mtaani si kukusaidia bali kuchukua mali zako. Na mkopo wa kichina ndo ulivyo
Hayo maswali ndiyo hatutaki kwani yana harufu ya ubeberu ndani yake.
 
wakati wanaijenga 70's ..nani aliwasimamia...
Tayari imeshagawanywa hii hapa...

China GDP per capita 8,826.99 USD (2017)

Linganisha na yetu...

Tanzania GDP per capita 936.33 USD (2017)

Nani zaidi hapo?
 
Khaa kwa hiyo mkuu basi jpm keshakubali ushoga maana juzi kakopa WB
WB hawa kuwa na kikwazo cha ushoga. Kikwazo chao ni watoto wa like wanaopata mimba kutokuruhusiwa kusomea tena.

Na wakaambiwa wakitaka kuendelea wakasome private.
 
Hayo ndo manufaa ya mikopo isiyo na masharti.
Mtu mwenye nia njema lazima akuulize itarudishaje mkopo? Mfano benki hawawezi kukupa mkopo bila kuangalia financial statement yako.

Wale wakopeshaji wa mtaani akijua una nyumba au gari anakupa pesa tena kwa muda mfupi huku akikuandikisha mkataba wa kwamba umemuuzia, nia ya wakopeshaji wa mtaani si kukusaidia bali kuchukua mali zako. Na mkopo wa kichina ndo ulivyo
Sharti lipo kwenye huo mkopo. Si unaona apo sharti kuwa wakishindwa kulipa mkopo basi wanachukuliwa bandari yao tu. Ukishajua kuwa utapoteza mali yako ndio utafanya bidii kuulipa mkopo wa watu, ila ukiambiwa kama ukishindwa kulipa mkopo basi ukubali kuolewa na hali ya kuwa ni chakula cha watu basi hutofanya bidii ya kuulipa.

Mkopo unapendeza iwe kama hivi, unachukua hela ya watu ukishindwa kurudisha basi na wewe upoteze mali tu.
 
Mengine sawa lakini hilo la kuendesha wenyewe kwetu mtihani. Tumeshuhudia reli ya kati, reli ya tazara na ATC yenyewe.

Wenyewe tukiendesha haya mashirika na reli zitakuwa chalikama ya awali.

Haya yange binafsishwa tu kwa masharti ya kuyaendesha kwa kazi iliyokusudiwa.
Tunajenga kwanza suala la uendeshaji baadae, hata ulaya na USA reli ni ya serikali treni ndio watu binafsi, wanalipia kutumia reli
 
Back
Top Bottom