Benki ya NMB imenitumia Shilingi 10,024,061,002,406 kimakosa

Benki ya NMB imenitumia Shilingi 10,024,061,002,406 kimakosa

NMB plz msiniingize majalibuni na Sina tamaa Kwa pesa ambayo siyo haki yangu na jasho langu,kuweni makini mtakuja kukosea Kwa vishoka hatimae kiwe kilio kwenu. Jana mmenitumia TZS 10,024,061,002,406 = Shilingi trilioni 10.024 (takribani) na sikutoa hata mia ndani ya dakika 45 hivi ndo mkairudisha.

Jana nimekuwa trionea Kwa nusu saa Asante sana NMB

View attachment 3646499
Mbona baina ya 6 na 1 kuna gepu hiyo ni mil 1 ila imejirudia mara mbili siyo trillion...wewe huoni 🏃‍♂️😁
 
Mbona ni Milioni Moja Na elfumbili kazaa iliorudiwa kutokea mara mbili katika balance yako??
 
Hela Za Nmb za watu wote walioweka ni Tril 12 , technically uliwekewa karibu fedha zote za Nmb na hapohapo ukawa mtu tajiri zaidi Tanzania ukiwa unautajiri mara mbili ya Mo pia ukawa miongoni mwa top 10 matajiri Africa mashariki na kati na ukawa kwenye 3000 bora richest men in the world nusu saa tu imebadilisha historia ya maisha yako.
 
Huwa Inatokea mara kadhaa kwahiyo usijione ajabu sana.

Ni makosa tu ya kiufundi kwenye mifumo ila huwezi toa fedha zaidi ya uliyonayo kwenye akaunti yako.
 
Hata salio likisoma 1trilion huwezi kuzitoa ama kuhamisha. Kwani system mpya ya bank waliyohamia sasa huwa na tabia ya unapofanya muamala kabla ya pesa kutoka huwa inaji-reconcile within seconds then ndo muamala unafanyika.
 
Hapo zimepita tu kama zilikuwa zako na zimeenda kwa mlengwa
Hela za kutakatishwa hizo
Acha ziende tu
 
NMB plz msiniingize majalibuni na Sina tamaa Kwa pesa ambayo siyo haki yangu na jasho langu,kuweni makini mtakuja kukosea Kwa vishoka hatimae kiwe kilio kwenu. Jana mmenitumia TZS 10,024,061,002,406 = Shilingi trilioni 10.024 (takribani) na sikutoa hata mia ndani ya dakika 45 hivi ndo mkairudisha.

Jana nimekuwa trionea Kwa nusu saa Asante sana NMB

View attachment 3646499
View attachment 3646535
Hii ni chai. Ukiangalia muda ulipoangalia salio ukakùta kuna 10bn na muda ulioangalia salio na kukuta 1m ni uleule: 19:28:58

Kwenye text umeandika hizo pesa NMB walizirudisha baada ya dakika 45. Kwa hiyo risiti ya pili ilitakiwa isome siyo chini ya: 20:14. 58
Verdict:
Kawapumbaze wapuuzi wenzako
 
Back
Top Bottom