Benki ya NMB yaja na huduma ya mkopo ya "NMB Salary Advance" kwa wafanyakazi

Ni 6% ya utakachokopa na sio ya net salary yako. Mfano ukikopa 10,000 utalipa 10,600 mwisho wa mwezi
 
Acha utani rafiki, NMB PLC ni baba la benki zote nchini haiwezi kuiga benki zinazochechemea. Hii ndio benki ya uhakika wa pesa zako hapa nchini.
Ni kweli wameiga CRDB pamoja na kuwa baba la benki.
 
Hicho Ndo Kitu ambacho sikitaki inamaana Unashindwa hata Kudunduliza Ukawa na Kahakiba kako ka 2.5Million au hata 2Million tuu? Tujirekebishe Watumishi.
Troll, hakuna mtu anayependa shida, na hakuna asiyependa jambo zuri. Kuna mabingwa wa kudunduliza, lakini nao yamewashinda awamu hii,wameingia kukopa! Nina rafiki yangu,miaka yote huwekeza kwenye ununuzi na uuzaji wa mazao ili kuboost kipato cha mshahara. Amejenga nyumba na ana gari ndogo ya familia na biashara ndogo ya mkewe. Mwaka jana kanunua mahindi gunia 200 kwa 45'000/= kwa gunia ili auze mwezi huu wa tatu ambapo kawaida bei hupanda even 3x. Sasa hivi,gunia ni 20,000/=, na hakuna mnunuzi!!!. Ameingia benki kukopa fedha ya kulipa karo za wanawe wasifukuzwe shule. Duka dogo la mkewe limeshindikana kuendelea,biashara imekufa,. Juzi walikuwa kwangu kuomba mkopo wa 50,000/= wanunue kioo cha mbele cha gari yao kimecrack na trafiki wanazingua. Tumekubaliana wanirejeshee mwisho wa mwezi jamaa akipokea salary. Hii issue ya kujiwekea akiba ni sawa,but not always under such scenarios
 
Dah, we jamaa ndo unanisimanga huku
 
Ninyi ndo watu ambao mkiulizwa nyanya zinalimwa wapi,mnasema "kwenye friji!"
Ni aina ya watu mnaoishi kwa nadharia za kwenye vitabu na kushindwa kujua uhalisia wa maisha.
Naamini hujawahi kutoa msaada kwa ndugu yeyote labda kwa vile huna ndugu maskini ama unao lakini ni mbinafsi wa hali ya juu!
Si sahihi kudhani nmb wanakusudia kuwatia umaskini wafanyakazi!Kwani mkopo huo ni hiari!Ukitaka unaomba,usipotaka unaacha!
Hizo hesabu zako na uchambuzi ni bure kabisa na inaonekana una roho mbaya sana.Hujui uhalisia wa maisha ya mtumishi na changamoto anazopitia.
Mikopo hiyo ni ukombozi mkubwa na itawapunguzia watumishi aibu ya kukopa laki mbili na kurudisha 260,000
Haya maoni yako ndiyo tunayaita siasa za kijinga!
 
Kaujiriwa ni Umasikini mkubwa sana na kamwe huwezi kuwa na uhulu wa kifedha.

Hiyo mikopo haiwezi masaidia chochote mfanya kazi kujikwamua hakuna kitu hapo.

wanaoshangilia ni wale watumwa
Wewe ukiteuliwa kuwa Balozi WA Tanzania hata hapo Kenya tu, Utakubali au Utakataa?

Ukiteuliwa kuwa Waziri, Utakubali au Utakataa uteuzi?

Hebu nijibu hapo kwanza
 
Shida hapa ni serikali isiyojali na katika hili mlengwa mkubwa ni mwalimu hakika. Walimu wametupwa sana na wengi wanastress sijui wanawafundisha nini watoto. Unakuta kakopa wengi ili wajenge wanakopa maximum sasa mshahara umebaki say 300,000 bodi ya mikopo elimu ya juu wamepita tens na 150,000. Hapo mwalimu mwenye familia anapaswa kuishi na 150,000 kwa mwezi na nyumba haijaisha. Ale,asomeshe,alipe kodi,asaidie wazazi,dharura nk kweli hapo kunamaisha? Serikali inayojali isingeruhusu mwalimu wake kudhalilika kwa kukopakopa mitaani na kufikia kunyang'anywa vitu vya ndani ama kufukuzwa kwenye nyumba za kupanga!! Kenya,Rwanda wamejitahidi lkn so hapa ndo maana tumekosa raha tuko kundi la nchi zilizopitia mauaji ya kimbari. Aibu hii ni ya serikali isojali watu.
 

Mimi naweza kuwa naishi kwa nadharia za kwenye vitabu lakini wewe utakuwa unaishi kwa nadharia za majukwaa.

1. Utamsaidiaje mnyonge kwa riba ya 72% APR?
2. Ikiwa mumetambua kama kuna tatizo la mshahara kutosholeza, solution si kumpa mkopo wa riba iliyopindukia, solution ni kumuongezea mshahara.
3. Ikiwa mfanyakazi kashindwa kutimiza mahitaji yake kwa 100% ya mshahara wake baada ya deductions, atawezaje kujikidhi kwa 60% itakayobaki?
4.ikiwa munatambua kwamba mfanyakazi mshahara haumkidhi, kwa nini anakatwa PAYE kwa income ambayo inamuweka kwenye poverty?
5. Ikiwa munajuwa kwamba kuna unregulated financial tricksters wanaochukuwa advantage ya umasikini wa wananchi, kwa nini musiwashuhulikie hao jamàa wanaotowa mikopo illgally. After all hawalipi taxes from their illegal income.

Based on reality, mtu yoyote anayechukuwa mkopo wa aina hiyo, atakuwa yuko beyond desperation and just short of destitution. Na kuthibitisha point yangu hiyo nakuhakikishia yoyote anayechukuwa mkopo huo basi hawezi kuulizwa uanenda kufanya nini benki akasema naenda kuchukuwa mkopo wa pay slip loan, ni aibuuuu!

Musione watu wote ni wajinga kiasi hicho. I have seen it all and have done most!
 
Hii ni nzuri,pesa njenje
 
Nimegundua tatizo lako ni pale ambapo umeshindwa kutofautisha kati ya nmb na serikali.Nmb si taasisi ya kutoa misaada.Ni taasisi ya kibiashara na kwa hiyo usitarajie kupewa msaada bure.
Taasisi hii kuwa ni ya serikali,haiwezi kumaanisha kuwa ikifanya maamuzi basi ni ya serikali.Taasisi hii ni semi automous,ina wajibu wa kuweka mipango thabiti ili ijiendeshe.
Nashauri usichanganye mambo,serikali bado ina wajibu wa kuhakikisha watumishi wake wanapata maslahi mazuri lakini si kwa kutoa sandakarawe kupitia benki ambayo nayo inatakiwa kulipa gawio la faida serikalini
 
Nimegunduwa kuwa akili zako unazikalia. Lujiendesha kwa taasisi ya fedha lazima itumie njia zenye ethic sio kuchukuwa advantage? Mbona hao wanowakopesha Milioni 100 hawawachaji 6%x idadi ya miezi wanayorudisha hela? Kwa nini umchaji mteja wako 6% wakati ungeweza kumpatia overdraft ya interest free kwa wiki 2 au mwezi mmoja! Inaonesha hujawahi kuvuka mpaka wa bara la Afrika wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…