Benki za Biashara Tanzania zinaogelea kwenye faida. Je, nini kimefanyika awamu ya sita?

Kama Kuna kaukweli,kibongo bongo biashara zinakufaa huku mitaani,tunashindwa kurejesha mikopo ,hizi tafti za Hawa jamaaa hazina uwalisia wa maisha halisi ya mtanzania
Ndugu yangu naomba tu tuungane, huu uchumi wa namba namba hakika kuueleza kuwa umekua/umeongezeka ni rahisi.

Kiu yangu nataka tafsiri itokee kwetu mitaani, tuone mabadiliko katika maisha, uwezo wa kununua mahitaji ya msingi ya nyumbani, tuone uwiano wa bidhaa tunazouza na zile tunazonunua. Mfano upaaji wa bei za vifaa ujenzi: misumari,bati, saruji vs mauzo na bei za mazao (bidhaa mama kwa wananchi scale kubwa)

Vinginevyo kwa namba hizi na madai ya kukua nahisi mwandishi unatupiga
 
Hamna hata haja ya kusoma hizo porojo za ccm propagandists. Nyie ni watu wanaojipendekeza kila rais akija mnafanya kazi ya kumtungia stori feki za kumpamba maanake kwa akili yenu fupi mnafikiri watu wote ni wajinga tu.

Wakati wa Magufuli pia kwa kutaka kumfurahisha, mkabumba eti Dodoma inaongoza kwa mapato..!! na mkabumba tena kwamba mkoa wa Geita ni maskini sana ili tu wawe na uhalali wa kupewa mgawo mkubwa kutoka kwenye bajeti ya nchi.

Nyie ni watu wa hovyo sana na sasa mmeanza kumdanganya na maushungi pia. You people are very useless.
 

Na makato Yameongezeka zaidi

 
Baada ya watumishi kuongezewa mishahara kutokana na kupanda kwa madaraja, wengi walikimbilia kukopa hivyo inawezekana hii ni moja ya sababu iwapo taarifa hii ni ya kweli na sio propaganda za kisiasa.
 
Kwa akili zako mkopo wa bank ni sawa na ule unaochukua duka la Mangi, unakopa bidhaa leo unalipa baada ya siku mbali tatu.

Kama kweli kuna mafanikio hayo basi credit zinaenda kwa hayati, ina maana baada ya kutoa ufisadi na kuyumbisha mapato rahisi rahisi ya Banks. Jamaa walijipanga na kufanya biashara kwa umaskini na haya ndio matunda.

Kuna wasaa muwe mnafikiria aina ya post za kitoto kama hizi; na hayo magazeti uchwara, yenye kuchochea ufisadi.
 
Zinaanza namba then hali halisi mkuu, Subiri utaona matokeo ila fanya kazi kwa bidii
 
Khaaa yaani miaka mitano yote bila bila
 
Khaaa yaani miaka mitano yote bila bila
Ndio tofauti yetu ilipo wewe kama chawa upo kutafuta mlo ata ikibidi kuandika uongo.

Halafu kinachoshangaza kwani amuwezi sifia tu without showing ‘binary opposite’ ya Samia na Magufuli; hiyo vita ya popularity awezi shinda kwenye jamii.

Mama abaki kama mama tu kuliko kulinganisha uongozi wake na wamtangulizi wake.
 
Hapa nakupinga mkuu,

Refence ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu,

Hapa sio kwamba mwandishi kwa nilivyoelewa anamkashifu au kumdhalilisha JPM no anafanya "Comparative analysis " ambayo hata JPM mwenyewe kwa kinywa chake ameifanya sana rejelea hotuba zake zote,

Why leo kwa Rais Samia iwe Haramu??!!
 
Maana yake pesa iko kwa wingi,

Hongera Rais wangu,

Nampenda sana mama Samia ✍🏿✍🏿
 
Policy za samia ndio zibadili faida ndani ya miezi 6?? Sababu ya haya mabadiliko ni hii document ya BOT. Sera za Samia na faida zake zitaonekana mwaka wa Fedha ujao sio huu. Tusimpambe sana

 
Mtakumbuka kwamara ya mwisho mabank yetu ya biashara hapa Tanzania kurekodi faida ya kihistoria ya tangu uhuru ilikuwa ni mwaka 2015 pale
Pesa chafu, zilizofichwa, inflow toka nje ruksa, hakuna kuchukngulia accounts, freezone magendo madawa, fake fungulia mbwa pia inafaida zake.
 
Baada ya watumishi kuongezewa mishahara kutokana na kupanda kwa madaraja, wengi walikimbilia kukopa hivyo inawezekana hii ni moja ya sababu iwapo taarifa hii ni ya kweli na sio propaganda za kisiasa.
Wamepanda madaraja mwaka huu!! Mfano mtu kakopa million 20 mwezi wa kwanza hyo faida ya mkopo wake inaweza kuwa reflected ndani ya miezi 6? Wakati hata principle tu haijalipwa hta robo bado!!

Mie naweza ipa credit BOT sababu ilimwaga trillion kwa mabenki kujikimu baada ya Covid pia ilipunguza masharti mfano reserve requirement BOT na masharti ya agency banking n.k But Samia hana impact yoyote ndani ya miezi 9 ya kibenki so hizo faida za Samia labda kuanzia mwakani.
 

Ni wivu tu
 
Ni wivu tu
Wivu ukwapi hapo? Ni sawa useme faida za tozo zionekane mwezi huu??? Uchumi ni process hata Mama Samia kasema atamwaga trillion 5 kwa uchumi wa ndani lakini unadhani zitaingizwa kwa mkupuo mmoja?? Hapana inaweza chukua hta miaka 3 mpka ziwe zimezungushwa kwa uchumi!!

BOT imetoa trillion nzima kwa mabenki af mnajiuliza faida wametoa wapi?? Then credit kwa Samia wakati alikua makamu tu by then?? Get real
 

inamaanisha kwamba kuna pesa nyingi sana kwenye mzunguko kwa sababu izo pesa zmetoka kwa wananchi, kwenye scenario kama hii unaangalia na hali ya wananchi ikoje, kama hakuna complains nyingi basi moja kwa moja ina maanisha uchumi umeharibika, kuna uwezekano BOT waliongeza kiasi kingi sana cha pesa kwenye mzunguko, kwa TSH anytime inaweza kushuka thamani tena against USD, na baada ya mwaka uchumi unaweza ukawa hatarini kama kusipokua na hatua za kupunguza pesa zilizopo kwenye mzunguko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…