Mtakumbuka kwamara ya mwisho mabank yetu ya biashara hapa Tanzania kurekodi faida ya kihistoria ya tangu uhuru ilikuwa ni mwaka 2015 pale ambapo yaliporekodi Jumla ya faida ikiwa ni baada ya kodi ya Tshs 438BL,
Kwamiaka mitano mfululizo iliyopita mabank haya hayajaweza kuivunja rekodi hii zaidi sana wakati flani faida zao zilishuka mpaka kufikia Jumla ya Tshs 286 yaani mwaka 2017 hii ni Jumla ya faida kwa mabank yote ya biashara nchini,
Leo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tena kwa kipindi cha Jan -Sept tu mabank hayohayo kwenye nchi hii hii yameivunja ile rekodi iliyowekwa na Mzee Jakaya Kikwete ya Tshs 438BL kwa zaidi ya 7.53% na hii ni robo tatu tu ya mwaka,
Kwalugha rahisi miezi michache ya Rais Samia mabank yamevunja rekodi ya faida ya tangu uhuru ambayo ilivunjwa na Mzee Jakaya Kikwete kwa Tshs 438BL leo Samia ameivunja kwa Tshs 471BL na hii ni kwa miezi tu, tunaposema Rais Samia hakamatiki tunamaa hii ndungu zangu Watanzania,
Kwa tathimini iliyofanywa kwa mabank 13 ya kibiashara nchini kati ya 14 yanayotengeneza faida NMB na CRDB wamebeba 80% ya faida yote ya Tshs 471BL kwa kuwa na faida ya Jumla ya Tshs 379BL,Wakati huohuo NPL yaani Non Performing Loans au mikopo " Chechefu " ikishuka na kufikia chini ya 35.7% kwa baadhi ya mabank huku thamani yake ikupungua kutoka tshs 395.69BL mwaka 2020 hadi tshs 392.4BL kwa lugha ya kibank (arrears -zimepungua )
Sababu kubwa yaongezeko hili kubwa la Faida kwa mabank ya biashara nchini zinatajwa kuwa ni Sera nzuri za ki-Uchumi za Serikali ya awamu ya Sita pamoja na miongozo mathubuti toka BOT kama mlezi wa mabank haya hasa kwenye kupunguza vipimo vya risk kwenye utoaji mikopo ikiwa ni pamoja na kutoa fedha maalumu "Stimulating fund " kiasi cha Tshs 1trl ili kuziongezea ukwasi Bank zetu za biashara zilizokaukiwa hii imesaidia sana kuinua sekta ya fedha ambayo utoaji mikopo umepanda toka 2.5% 2020 hadi 9.8% hivi sasa,
Kwamsiofahamu zaidi ya 80% ya faida yote ya mabank ya biashara inabebwa na mikopo na Ukiona mabank yanapata faida sana maana yake yamekopesha sana na wateja wao wameweza kurejesha mikopo yao ( EMI) kwa wakati na ndio tunasema NPL imeshuka au mikopo isiyolipika|chechefu imepungua na ndio sababu faida imepanda na kwa maana hiyo biashara mtaani inakua au inakwenda vizuri ndio maana mteja X aliyekopa bank Y ameweza kuchukua mkopo Bank na kununua bidhaa na kisha kuuza na mwisho kupeleka marejesho ya Bank kwa wakati yaani ( Purchasing Power-Uwezo wa kununua ) umeongezeka Tanzania, Hongera Sana Rais Samia hakika unaupiga mwingi,