Benki za kwenye simu ni zaidi ya Benki Kuu!

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
1,726
Reaction score
3,391
Hivi kuna mtu nyuma anaangalia kama watu kama Songesha, Nivushe na watoa mikopo kwenye simu kama hizo hela wanazokopesha wanazo keshi?

Kwa picha ya fasta fasta hawa jamaa ni zaidi ya benki kuu. Hawahangaiki hata kuchapa pesa kama benki kuu, wanachapa tu codes, tunakopeshana keshi wenyewe halafu wanadaka faida!

Bonge moja ya business. Ukiangalia hata mtu akishindwa kulipa wao hawawezi kupata hasara.
 
Hii sayansi ndio ambayo hutumika:-
Unapoweka fedha halisia 'bank' au kwenye mihamala, ile fedha inageuzwa kuwa 'digital', na unapotaka fedha halisi, ile digital inageuzwa kuwa fedha halisi ''physical money'' kwa kile kiwango utakachotaka kutoa.
Kwa hiyo unapoomba mikopo mitandaoni, ina maana wao wanabadilisha zile fedha zao kuwa digital, ndipo wanakupatia; ila kiuhalisia lazima wao wawe na pesa halisia, noti.​
 
Hii nchi watu wanashangaza Sana

Nimeshangaa kuna watu wanasema unaweza kopesha hela ambayo hauna.
 
Hii sayansi ndio ambayo hutumika:-
Unapoweka fedha halisia 'bank' au kwenye mihamala, ile fedha inageuzwa kuwa 'digital', na unapotaka fedha halisi, ile digital inageuzwa kuwa fedha halisi ''physical money'' kwa kile kiwango utakachotaka kutoa.
Kwa hiyo unapoomba mikopo mitandaoni, ina maana wao wanabadilisha zile fedha zao kuwa digital, ndipo wanakupatia; ila kiuhalisia lazima wao wawe na pesa halisia, noti.​
Nini kinawazuia kuingiza digital money hewa? Maana wao hawatoi keshi, ni mawakala ndiyo wanaokupa keshi. Haiingii akilini waifungie keshi sababu wameikopesha mtandaoni!! Vipi mtu akishindwa kulipa, wao kama wakopeshaji wanapata hasara gani?
 
Ulishawahi kwenda kwenye kibanda cha wakala, ukawapa labda laki, wakakuwekea zaidi?
Wakikuwekea zaidi, wao ndio watapata hasara; wakikuwekea pungufu wao ndio watapata faida, na wewe hautokuwa tayari kupokea pungufu.
 
Back
Top Bottom