Benki za kwenye simu ni zaidi ya Benki Kuu!

Benki za kwenye simu ni zaidi ya Benki Kuu!

Ni rahisi tu. Ukweli ni kuwa wakala anayekupa pesa kama ukienda kutoa baada ya kusongesha au nivushe ndiye anayekupa mkopo.
Duuh wewe jamaa unazingua.Kwani unapotoa pesa, wakala anajua ni pesa ya songesha? Hujui kuwa anaejua ni pesa ya songesha ni wewe mtoaji tu? Iwe mgodi , mpawa, songesha, akiba tu yako n.k lakini unapotoa pesa lazima ikupeleke kwenye menu ya M.pesa, tigo pesa n.k . Wakala kama hana salio la kutosha hauwezi kutoa hela bila kujali hiyo hela unayotoa ni songesha au la. Sasa unafikiri yeye wakala salio lake analitolea wapi kama hakununua hilo salio kwa cash ?
 
Wakala anaingiaje hapa? Wakala ananunua float kwa pesa zake. Anavyoenda kuibadili kuwa cash ni pesa yake anaibadili.

Sasa wewe unakopa Songesha lakini unaenda kuchukua pesa za wakala wa simu pesa ambaye anakupa pesa yake. Huendi kuchukua kwenye ofisi za Songesha. Hivyo Songesha wametoa mkopo bila kutoa pesa.
Unaonyesha kiwango kikubwa sana cha ujuaji na uelewa duni wa unachojaribu kukijadili, punguza ujuaji.
 
Ni namba tuu wakati inaenda kutolewa mtu anachukua cash
Elimu za watu hizo
Na kuna mdau siku moja alishawahi kutoa elimu hiyo kuhusu kubalance hayo mambo benki kuhusu hela softcopy na hardcopy!

Labda mtoa mada angekuja kwa mtindo wa swali ili apewe elimu ingefaa zaidi kuliko kujifanya ni mtaalamu wa hayo mambo!
 
Hizo kampuni ziko kama benki kuu. Hazipati hasara wao ni faida tu. Wanaandika wamekusongesha laki moja. Unaenda kwa wakala unaichukua. Ukilipa unaingiza kwa wakala labda laki na kumi. Wanachukua kumi na kugawana na voda.
Kwa mwezi labda 100milioni hazijalipwa. Lakini milioni 500 zimeingia kama faida. Wanatoa 100m kwenye 500m na kubakiwa na faida 400m.

Huu ni mfano wa wanavyoweza kopesha pesa bila kuwa nazo. Ni zaidi ya benki kuu, maana benki kuu inawabidi wachapishe hizo pesa.
Ficha hii aibu unayojiletea humu jukwaani.
 
Hicho kiasi unachokopesha kiko backed na pesa halisi kwenye bank. Usidhani hiyo digital float haiko backed na kiasi fulani cha pesa. Ndiyo maana hata wakala ili apate float ya kukutumia anaenda kwa wakala mkuu au bank ana deposite amount hiyo. Au tuseme ni kam USDT kwenye crypto.
Unapotoa mkopo wa Songesha hupewi pesa na benki iliyotoa mkopo, badala yake pesa unayopewa ni ya wakala. Wao kama wana pesa inaback huo mkopo basi haitumiki kabisa. Na hiyo pesa imekaa tu au inatumika huko?
 
We jamaa cha kukusaidia kasome kuhusu:

Digital money
Fractional-reserve banking
Correspondent Bank

Hizo huduma za Songesha na nyingine za kutoa mikopo kwenye mitandao ya simu kuna Bank ndiyo zinatoa hizo pesa kwa kupitia leseni walizopewa na BOT.

Bank of Tanzania na Central Banks nyingine kwa kila nchi ndiyo inayoshikilia Digital money, hakuna mtu au taasisi inaweza kujiandikia tu namba kwasababu kila muamala una taarifa (digital signature): kama mtu akitoa/akikopa 10,000 basi ujue hiyo taarifa kuna mahali ni -10,000.

Digital money ni taarifa. Mfano, bank transfer siyo kwamba ni pesa kweli zinatoka account A kwenda B, au Bank A kwenda B: kinachotokea ni kubadilishana taarifa za miamala na zote hizi zinakuwa regulated na BOT/Central Bank.
Lakini hizo benki hazitumii pesa zao wenyewe kukopesha, zinatumia pesa za mawakala. Maana huko ndiko unaenda kuchukua keshi iwapo umesongesha au umenivushe.
 
Unapotoa mkopo wa Songesha hupewi pesa na benki iliyotoa mkopo, badala yake pesa unayopewa ni ya wakala. Wao kama wana pesa inaback huo mkopo basi haitumiki kabisa. Na hiyo pesa imekaa tu au inatumika huko?
Yani kuna kitu ambacho unabidi ukielewe. Pesa yote iliyo kwenye mzunguko iko backed na real money mahali iwe bank au kwa wakala. Ile float unayorushiwa iwe kwa wakali au na songesha iko backed na hard cash that is how it works.
Hivyo mtandao kama voda wanajua float nzima iliyopo kwa mzunguko ni kiasi fulani na kiko backed na hardcash na ndio maana mpesa wala tigo pesa huwezi hata kuziweka katima kundi la crypros
 
Duuh wewe jamaa unazingua.Kwani unapotoa pesa, wakala anajua ni pesa ya songesha? Hujui kuwa anaejua ni pesa ya songesha ni wewe mtoaji tu? Iwe mgodi , mpawa, songesha, akiba tu yako n.k lakini unapotoa pesa lazima ikupeleke kwenye menu ya M.pesa, tigo pesa n.k . Wakala kama hana salio la kutosha hauwezi kutoa hela bila kujali hiyo hela unayotoa ni songesha au la. Sasa unafikiri yeye wakala salio lake analitolea wapi kama hakununua hilo salio kwa cash ?
Yaani wakala angefahamu pesa anayotoa ni ya mkopo utakaozaa faida angegoma kutoa mpaka apewe na yeye chake. Maana anawakopeshea watu pesa, kwa kutumia keshi zake alizozipata kwa jasho.

Yaani ipo hivi. Ni kama wewe mtu aje kwako kukopa 10,000. Unamwandikia mkopo halafu unamwambia akachukue dukani kwa Mangi, riba ni 1,000. Akilipa unaenda kwa mangi unachukua riba yako 1,000. Unampa Mangi labda 100 ya usumbufu. We mwenyewe hauna hata mia ya mtaji. Ndiyo kinachofanyika mikopo ya simu.
 
Yani kuna kitu ambacho unabidi ukielewe. Pesa yote iliyo kwenye mzunguko iko backed na real money mahali iwe bank au kwa wakala. Ile float unayorushiwa iwe kwa wakali au na songesha iko backed na hard cash that is how it works.
Hivyo mtandao kama voda wanajua float nzima iliyopo kwa mzunguko ni kiasi fulani na kiko backed na hardcash na ndio maana mpesa wala tigo pesa huwezi hata kuziweka katima kundi la crypros
Pesa inayozunguka haijawahi kuwa backed na real money kikamilifu. Benki kuu yenyewe wanachapisha pesa inayokuja na riba. Hivyo pesa tu inapochapwa inakuwa imepangwa irudi zaidi ya iliyochapwa. Yaani mzunguko unategemewa kuwa mkubwa kuliko kiasi halisi cha pesa. Sasa kwa ilivyo hii mikopo ya simu ni zaidi ya benki kuu. Wanakupa mkopo bila ya kuwa na keshi halafu wanategemea faida.
 
Hivi kuna mtu nyuma anaangalia kama watu kama Songesha, Nivushe na watoa mikopo kwenye simu kama hizo hela wanazokopesha wanazo keshi?

Kwa picha ya fasta fasta hawa jamaa ni zaidi ya benki kuu. Hawahangaiki hata kuchapa pesa kama benki kuu, wanachapa tu codes, tunakopeshana keshi wenyewe halafu wanadaka faida!

Bonge moja ya business. Ukiangalia hata mtu akishindwa kulipa wao hawawezi kupata hasara.
That's a Spot BOT currently not regulating I think. so they really should enjoy it until they no longer can't
 
Ndio maana ukajiita wakili wa shetani benki kuu sio wehu kama unavyofikiri weka akilini hilo.....kingine ukita akili ikae sawa nenda kachukue riport yako ya NIDA yako mwenyewe kutoka credit bureau ambao wanafanya kazi chini ya bot ndio utajua kua taaarifa ziko uchi hakuna muamala ambao pesa yake haipo BOT never
 
Kama benki? Maana benki inaruhusiwa kukopesha nadhani hadi mara kumi ya pesa walizonazo. So hizo benki zinaingiza kiasi kidogo kwenye akaunti ya Songesha au Nivushe na kuendelea kukopesha?
We JAMA bhana, benki kumbka inakua na reserve benki kuu, sio kwamba inakopesha tu, money can't be just created from thin air. Project za crypto currency mfano Bitcoin ndio zlizoweza kutengeneza Pesa from thin air lkn pia znamfumo unaozipa hizo cryto currency valua mfano Bitcoin ina "proof of work" which is achieved through mining , unajikuta umetumia bitminer kama 100 na umeme wa million hamsin kupata Bitcoin Moja, kwahiyo yenyew Kuna gharama kibao znazotumika kutengeneza Bitcoin Moja. Nothing is for free. Hawawez kukukopesha Pesa ambayo hawana. Benk wanafanya investments ili kuzalisha Pesa ambazo unaweka akiba , ndio maana tatizo linaloitwa "bank run" likitokea hawawez kua na Pesa kwa wakat huo. " Bank run ni wakat ambapo wateja wote wanataka kutoa Pesa zao kwa muda huo.
 
Huu uzi umenifanya nicheke sana maana siamini ninayo yasoma humu.

Hawa wanaungana na mtoa uzi kutetea hoja yake kama sio wanafunzi wa kidato cha pili Nanjirinji sec school na okatokea ni watu wazima basi nchi hii itakuwa na wananchi wenye uelewa mdogo sana
 
Back
Top Bottom