Benki za kwenye simu ni zaidi ya Benki Kuu!

Benki za kwenye simu ni zaidi ya Benki Kuu!

We nae, hiyo msg unayotumiwa ya songesha inapunguza akiba Yao , mfano Voda Wana akiba ya shilling elf 10 waliopata Finca microfinance kwaajili ya songesha, uki songesha 1000 wanakutumia msg lkn wao wanabaki na 9000 jaribu kuelewa
Hujaelewa ninachozungumza
 
Sasa jiulize kwa nn zinakufa then linganisha na alichokiandika mtoa mada ndio utajua unapokopa bank, songesha, mgodi n.k wao wanatoa pesa physical Ila Kwako inakuja kama soft-money mana kilichowaunganisha mpaka ukapata mkopo n simu/akaunti na sio kwamba umepewa mkopo mkononi.
Bank runs ndiyo zinaua benki. Fuatilia kilichotokea hadi kupelekea kuanguka kwa benki ya sillicon valley mwaka jana. Kama benki inamake faida itaendelea kuwepo hata kama kuna watu wanadefault
 
Ndio mara ya kwanza kuona kuna bznes haina hasara.
Asante kwa kunijuza



KAZI ni kipimo cha UTU
Kujifunza hakuna mwisho mkuu. Chukulia reserve bank ya US ambayo ina shareholder kabisa wanaopata gawio. Ile ni biashara isiyo na hasara hata kidogo.
 
Sasa kwann hy 1k isiwe hamna kitu kama mada yako ulivyoiweka?
Wakati wa kucash mkopo ulichukua 10000 kwa wakala. Wakati wa kurudisha, ili ulipe lazima uweke 11000 kwa wakala. Hizi ni pesa halisi. Lakini kampuni iliyokupa mkopo haikumove pesa hata senti.
 
Hizo kampuni ziko kama benki kuu. Hazipati hasara wao ni faida tu. Wanaandika wamekusongesha laki moja. Unaenda kwa wakala unaichukua. Ukilipa unaingiza kwa wakala labda laki na kumi. Wanachukua kumi na kugawana na voda.
Kwa mwezi labda 100milioni hazijalipwa. Lakini milioni 500 zimeingia kama faida. Wanatoa 100m kwenye 500m na kubakiwa na faida 400m.

Huu ni mfano wa wanavyoweza kopesha pesa bila kuwa nazo. Ni zaidi ya benki kuu, maana benki kuu inawabidi wachapishe hizo pesa.
Bank kuu hawawezi kufanya hicho unachokiwaza ....
 
Back
Top Bottom