Benki za kwenye simu ni zaidi ya Benki Kuu!

Benki za kwenye simu ni zaidi ya Benki Kuu!

Hivi kuna mtu nyuma anaangalia kama watu kama Songesha, Nivushe na watoa mikopo kwenye simu kama hizo hela wanazokopesha wanazo keshi?

Kwa picha ya fasta fasta hawa jamaa ni zaidi ya benki kuu. Hawahangaiki hata kuchapa pesa kama benki kuu, wanachapa tu codes, tunakopeshana keshi wenyewe halafu wanadaka faida!

Bonge moja ya business. Ukiangalia hata mtu akishindwa kulipa wao hawawezi kupata hasara.
Hujui unaloongelea japo una pointi
 
Wakala anaingiaje hapa? Wakala ananunua float kwa pesa zake. Anavyoenda kuibadili kuwa cash ni pesa yake anaibadili.

Sasa wewe unakopa Songesha lakini unaenda kuchukua pesa za wakala wa simu pesa ambaye anakupa pesa yake. Huendi kuchukua kwenye ofisi za Songesha. Hivyo Songesha wametoa mkopo bila kutoa pesa.
Ww jamaa n kichwa ngumu kwa kweli.

Wakala hajui kuwa hiyo pesa umeipata kwa njia gani hy kitu haimuhusu yeye.

Songesha wanakukopesha digital money Kwako inakuja kama mkopo (negative -) Ila Ukienda kuibadilisha huo mkopo ambao ni pesa negative wakala anapokea kama pesa physical yani Pesa positive + Na Kwako kunabaki na negative vilevile Mpaka utakapoweka Pesa physical kureplace Ile - au ukope tena pesa digital (negative -) Ili kuzidisha kiwango cha negative.

Kama hujaelewa hapa, bc umeamua kuchagua upande wa ubishi mana wengi wamekupa elimu ila umegoma kuichukua.
 
Hivi ndio Benki wanavyotengeneza pesa kutoka from this air...., Banks n.k.wanaruhusiwa kukopesha hata zaidi ya pesa waliyonayo wewe ukikopa elfu kumi kwamba wamekupa sio lazima kwamba ile elfu kumi ipo kwenye safe kwa wakati huo ila wewe utakaporudisha elfu 10 na mia tano baada ya kuuza machungwa yako ni kwamba umewaongezea 500 kama faida na wao kuongeza elfu 10 katika mzunguko.... (FIAT Money pesa inazalishwa kwa njia ya credit ) na sio kwamba watu wanaamua kuchomoa printer yao kwamba tuongeze matrilioni kadhaa kwenye mzunguko.....
Tufanye hiyo elfu kumi umetokomea nayo hujalipa, waliokukopeshaje wataipata vp hy pesa ambayo ww umeipata physical.?
 
Mtoa mada wanamweleza kisomi sana ndo maana hawaelewi sana ila kwakuwa mimi nilitengenezwa kuja kuwa teacher kabla sijaingia ubia na pusher ngoja nikueleweshe.

Iko hivi

Kabla hujaanza biashara ya miamala unatakiwa uitafute pesa ya maandishi ambayo inahamishika bilakutumia mafuta.
Unazipata wapi hizi pesa

Hizi pisa zianauzwa benk kuu. Siyo kwamba zinaandikwa tu kama namba kwenye simu yako. Kwa hiyo ukienda na milioni kumi wanakupa milioni kumi ya mandishi. Sasa hiyo ndo unaanza kuigawa kwa wadau wako ambao wewe unawaita mawakala na mgao utaendana na kile mdau alichotoa

Mfano umepewa milioni kumi benki kuu na ukagawa laki moja kwa mawakala mia pesa yako ya keshi uliyotoa benk itakuwa imerudi yote na wewe hutokuwa na pesa ya maandishi maana umewapa yote hao mawakala.

Unayokopesha itatoka wapi

Kwa mfumo wa mfano wangu unayemkopesha nae anakuwa mdau wako ila hana tasilimu ya kukupa hivyo unachukua tena milioni kumi unawapa benk wanakupa ile hela ya maandishi halafu unakuja kuwapa hao wadau wako ambao hawana hela ya kesh. Kwahiyo we unabaki huna taslimu na ile ya mandishi huna. Sasa mtu uliyemkopesha hela ya mandishi anatakiwa akayanunue yale mandishi kwa wale watu wako wa kwanza ambao wao ili wampe mandishi lazima awape pesa. Sasa akishawapa pesà wakampa mandishi wewe ndo unayakata kwa liba sambamba na makubaliano. Kwahiyo unaanza iurudisha mandishi yako ambayo ukiyarudisha kule benki wanakupa pesa yako. Kama yale mandishi yatarudi yote yakiwa na riba ya 10% basi we utapeleka benk yakiwa yanasoma milion 11 na hiyo benk ndiyo hela watakayokupa. Kwahiyo utakuwa umepata milioni moja kama faida
 
Tufanye hiyo elfu kumi umetokomea nayo hujalipa, waliokukopeshaje wataipata vp hy pesa ambayo ww umeipata physical.?
Katika mfumo wa kukopeshwa wanaangalia faida yao kupitia wewe mwenyewe. Nikupe mfano

Mi nauza unga kwa tsh 1000 kwa kilo. Lakini unga wangu hufika saiti ya soko kwa gharama ya tsh900 hivyo kila nikiuza kilo moja napata faida ya tsh 100. Sasa wewe ni mteja wangu na kwa wiki ninauhakika unanunuaga kilo kumi. Hivyo kila wiki ninauhakika wa kufaidika na wewe kwa tsh 1000. Hivyo nikakupa nafasi ya kukopa unga ulipe kwa liba na sheria ni kuwa mwisho wa kukopa kwa wiki nzima ni nusu kilo. Na wewe kutokana na changamoto za kimaisha unakuja kukopa kweli nusu kilo. Kwahiyo ntakup hiyo nusu kilo ambayo ni tsh500 kiasi kwamba hata ukitokomea nayo nilishafaidika na wewe kwa majuma ya nyuma ila ukinilipa unanilipa tsh 600 kama liba ya mkopo
 
Sasa c ndo ili ihesabike kuwa h n faida maana ake hapo kuna nyongeza ya pesa kutoka kwenye pesa ya awali ambayo ilikuwa n mkopo.

Tunarudi kule kule, unapokopa hy pesa inaweka cashless tena ikiwa negative mana huwezi kuonana na mhusika ana kwa ana (ni sawa ww upo Mtwara unamtumia mtu yupo Tanga pesa itaingia cashless 'digital money' ila kwako ilikuwa cash 'money physical') ila wakati wa kurudisha mkopo ni lazima iwe positive nikimaanisha iwe zaidi ya ile ya awali ya mkopo ili kuua ile negative.

Sasa usipolipa hy n hasara (negative) Kwa yule aliyekukopesha mana yeye alitoa/alikupa mkopo kwake ikiwa mfumo wa cash (positive)
 
Pesa inayozunguka haijawahi kuwa backed na real money kikamilifu. Benki kuu yenyewe wanachapisha pesa inayokuja na riba. Hivyo pesa tu inapochapwa inakuwa imepangwa irudi zaidi ya iliyochapwa. Yaani mzunguko unategemewa kuwa mkubwa kuliko kiasi halisi cha pesa. Sasa kwa ilivyo hii mikopo ya simu ni zaidi ya benki kuu. Wanakupa mkopo bila ya kuwa na keshi halafu wanategemea faida.
Hiyo riba ya kwenye mzunguko iko backed na real cash inayotoka kwa mtumiaji. Mtumiaji atatoa ile interest in real cash ambayo itaongezwa kwenye digital cash. Waliotengeneza hizo algorithm wapewe maua yao maana hakuna any money inayokuwa made just from no where.
Pesa yote iliyo kwenye mobile wallets iko backed na really cash na maana mwisho wa siku watu wakisema wanatoa pesa yote na mawakala wanaenda kubadilisha float kuwa cash, mtandao utakachobaki nacho ni zile profit tu ambazo walizitengeneza na ambazo zilitokana na watumiaji ambao nao walitoa real cash.
Nitakupa mfano mmoja, ushawahi jiuliza kwanini hizi remittance apps kama NALA au Grey huwa zinafanya fund raising ya mtaji ili ziweze kufanya kazi, ni kwa sababu ela unayotuma via mfano NALA iko backed na really cash ambayo itakuwa settled baadaye kwa channels ambazo zimehusika kukufikishia pesa. Ingekuwa tu wanatengeneza digital money kwanini wafanye fund raising?
 
Huu uzi umenifanya nicheke sana maana siamini ninayo yasoma humu.

Hawa wanaungana na mtoa uzi kutetea hoja yake kama sio wanafunzi wa kidato cha pili Nanjirinji sec school na okatokea ni watu wazima basi nchi hii itakuwa na wananchi wenye uelewa mdogo sana
Yani watanzania hatuna uelewa na mambo mengi
 
Hiyo riba ya kwenye mzunguko iko backed na real cash inayotoka kwa mtumiaji. Mtumiaji atatoa ile interest in real cash ambayo itaongezwa kwenye digital cash. Waliotengeneza hizo algorithm wapewe maua yao maana hakuna any money inayokuwa made just from no where.
Pesa yote iliyo kwenye mobile wallets iko backed na really cash na maana mwisho wa siku watu wakisema wanatoa pesa yote na mawakala wanaenda kubadilisha float kuwa cash, mtandao utakachobaki nacho ni zile profit tu ambazo walizitengeneza na ambazo zilitokana na watumiaji ambao nao walitoa real cash.
Nitakupa mfano mmoja, ushawahi jiuliza kwanini hizi remittance apps kama NALA au Grey huwa zinafanya fund raising ya mtaji ili ziweze kufanya kazi, ni kwa sababu ela unayotuma via mfano NALA iko backed na really cash ambayo itakuwa settle baadaye kwa channels ambazo zimehusika kukufikishia pesa. Ingekuwa tu wanatengeneza digital money kwanini wafanye fund raising?
Mkuu biashara ya ukopeshaji huwa haiwi backed na real money za kiasi kile kile. Ndiyo maana hakuna benki inaweza kuhimili bank run(Watu wote kutoa pesa zao kwa pamoja). Hata wakopesha mtandaoni hawawezi kuhimili. Sasa kiasi cha pesa zinazoback mikopo hutofautiana. Benki kuu haina chochote inachoback pesa wanazochapa na kukopesha. Inaonekana ipo hivyo kwa hawa wakopesha mitandaoni.
 
We JAMA bhana, benki kumbka inakua na reserve benki kuu, sio kwamba inakopesha tu, money can't be just created from thin air. Project za crypto currency mfano Bitcoin ndio zlizoweza kutengeneza Pesa from thin air lkn pia znamfumo unaozipa hizo cryto currency valua mfano Bitcoin ina "proof of work" which is achieved through mining , unajikuta umetumia bitminer kama 100 na umeme wa million hamsin kupata Bitcoin Moja, kwahiyo yenyew Kuna gharama kibao znazotumika kutengeneza Bitcoin Moja. Nothing is for free. Hawawez kukukopesha Pesa ambayo hawana. Benk wanafanya investments ili kuzalisha Pesa ambazo unaweka akiba , ndio maana tatizo linaloitwa "bank run" likitokea hawawez kua na Pesa kwa wakat huo. " Bank run ni wakat ambapo wateja wote wanataka kutoa Pesa zao kwa muda huo.
Nini kiwazuie wakopesha mitandaoni kukukopesha pesa ambazo hawana? Maana wanakuandikia mkopo lakini keshi unaenda kuchukua kwa wakala. Wao hawatoi hata mia.
 
Mkuu biashara ya ukopeshaji huwa haiwi backed na real money za kiasi kile kile. Ndiyo maana hakuna benki inaweza kuhimili bank run(Watu wote kutoa pesa zao kwa pamoja). Hata wakopesha mtandaoni hawawezi kuhimili. Sasa kiasi cha pesa zinazoback mikopo hutofautiana. Benki kuu haina chochote inachoback pesa wanazochapa na kukopesha. Inaonekana ipo hivyo kwa hawa wakopesha mitandaoni.
Serikali haiwezi kukuruhusu utengeneze pesa uingize kwenye mzunguko. Bank haiwezi kuhimili bank run kwa sababu pesa unayoweka wanaikopesha kwa watu wengine hivyo watu wote mkienda kutoa pesa inakuwa pesa yenu haipo imelala tu kwenye safe ikiwasubiri nyingine inakuwa imekopeshwa kwa watu na kwenye uwekezaji mwingine.
Mkuu ungekuwa walau una knowledge kidogo ya programing na algorithm achili mbali uchumi unavyofanya kazi ungeelewa.
Hebu nikupe mfano mdogo tu. Tuseme ninaanzisha microfinance yangu ambayo wewe unaweza kutumia app ukakopa ukapokea pesa kwa njia ya mpesa. My initial capital tuseme ni milion 10. Hivyo hiyo milioni 10,000 nitaipeleka ninunue float sawa na hiyo pesa kutoka kwa mpesa.
So, tuseme kila ukikopa laki moja na charge riba ya 20,000 kwa mwezi na tua ssume pesa yote imekopwa aktika huo mwezi.
Ikiwa ina maana wakopaji walichukua milion kumi yangu kama float wakaenda kutoa kwa wakala kwa kumpa float akawapa hard cash na hiyo hard cash kumbuka mtengeneza app alideposite kwa voda, so alichotoa wakala kitakuja kuwa settled na hard cash ya mtengenezaji aliwaachia voda.
Na baada ya mwezi kila alilyekopa ataenda kwa wakala na hard cash ikiwa ina ongezeko la 20, 000 ya alichokopa apewe float anitumie. So mwisho nitakuwa nina milion 12 ambapo ile milion 2 si kwamba imetoka from no where, imetoka kwenye ongezeko la hard cash ya milioni mbili ambalo wakopaji walideposite kwa kumpa wakala so nalo liko backed na hard cash bado.
So mfumo mzima una chain ya pesa ambayo iko backed na hard cash.
Kwanza ukifuatilia hawa wakopaji wengi ni mabenki na hizi microfinacne ambazo wanaunga tu mifumo yao kwa hii mitandao ya simu na wala hawana umiliki wa hizo mobile wallet money so wanaweka float ili uweze kupata hiyo pesa.
 
Kitendo cha uwepo wa fractional reserve banking ndiyo sababu ya bank run na ni ushahidi kuwa serikali zinaruhusu watu waingize pesa kwenye mzunguko kutoka hewani. Bank ukiwa na mtaji wa 10bln unashangaa unaweza kuruhusiwa kukopesha hadi 50bn. Sasa kama siyo kuetengeneza pesa na kuziingiza kwenye mzunguko ni nini?
Mkuu ungekuwa walau una knowledge kidogo ya programing na algorithm achili mbali uchumi unavyofanya kazi ungeelewa.
Hebu nikupe mfano mdogo tu. Tuseme ninaanzisha microfinance yangu ambayo wewe unaweza kutumia app ukakopa ukapokea pesa kwa njia ya mpesa. My initial capital tuseme ni milion 10. Hivyo hiyo milioni 10,000 nitaipeleka ninunue float sawa na hiyo pesa kutoka kwa mpesa.
So, tuseme kila ukikopa laki moja na charge riba ya 20,000 kwa mwezi na tua ssume pesa yote imekopwa aktika huo mwezi.
Ikiwa ina maana wakopaji walichukua milion kumi yangu kama float wakaenda kutoa kwa wakala kwa kumpa float akawapa hard cash na hiyo hard cash kumbuka mtengeneza app alideposite kwa voda, so alichotoa wakala kitakuja kuwa settled na hard cash ya mtengenezaji aliwaachia voda.
Hapa ndiyo hoja yangu ipo. Kitu gani kinawazuia mpesa na wakopeshaji wa mitandaoni kuandika float ya 10m out of thin air. Watu wakakopa kwa kuchukua keshi kwa mawakala halafu mwisho wa mwezi ukajipatia keshi 2m bila kuwa na mtaji wowote hapo mwanzo.
Na baada ya mwezi kila alilyekopa ataenda kwa wakala na hard cash ikiwa ina ongezeko la 20, 000 ya alichokopa apewe float anitumie. So mwisho nitakuwa nina milion 12 ambapo ile milion 2 si kwamba imetoka from no where, imetoka kwenye ongezeko la hard cash ya milioni mbili ambalo wakopaji walideposite kwa kumpa wakala so nalo liko backed na hard cash bado.
Kama wakopeshaji wanachukuwa pesa kwa wakala. Nini kinawazuia watu kama Songesha kukopesha pesa hewa. Watu wakaenda kuchukua pesa cash kwa wakala halafu mwisho wa mwezi wakairudisha na riba(Pesa halisi) ambayo Songesha wanaiweka kibindoni japokuwa hapo mwanzo hawakuwa hata na mia ya kukopesha.
So mfumo mzima una chain ya pesa ambayo iko backed na hard cash.
Kwanza ukifuatilia hawa wakopaji wengi ni mabenki na hizi microfinacne ambazo wanaunga tu mifumo yao kwa hii mitandao ya simu na wala hawana umiliki wa hizo mobile wallet money so wanaweka float ili uweze kupata hiyo pesa.
Fractional reserve banking inatuambia mfumo haupo backed na hard cash.
 
Back
Top Bottom