Benki za Marekani kufeli ni ishara ya nini?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Wiki iliyopita Benki ya Marekani Silicon Valley Bank ilipatwa na bank run(watu wengi kutaka kutoa pesa benki kwa pamoja) na kupelekea kufilisika. Tena benki ya pili, Silvergate, imepatwa na kitu kama hicho.

Haya mambo yanaashiria nini? Tujipangaje?
 
Haya ni mambo ya kitaaluma sio ushabiki wenu wa kindezi.
.
IMG_20230305_122221.jpg
 
ile ilikuwa a classic case ya bank induced panic, walipotoa news kuwa wanataka cash injection from equity markets , hedge funds nyingi zilitoa pesa haraka kupelekea collaspe ya benki.

Ila dont read too much into it, isipokuwa credit suisse , all major banks za dunia i.e Jp morgan , BOA , Goldman sachs ukiangalia reports za financial stress tests na liquidity ratios vs leverage portfolio zao wako sawa currently .
Ila risks to tier 2 banks and below bado zipo
 
Wiki iliyopita Benki ya Marekani Silicon Valley Bank ilipatwa na bank run(watu wengi kutaka kutoa pesa benki kwa pamoja) na kupelekea kufilisika. Tena benki ya pili, Silvergate, imepatwa na kitu kama hicho.

Haya mambo yanaashiria nini? Tujipangaje?
Umesema bank za marekani lakin umeishia kutaja bank moja nilitegemea hata utataja bank kama 5 hivi
 
Wanaoiombe U.S.A mabaya hawajielewi zaidi ya umburula na udini ulioletwa na mwarabu, na hao waarabu wenyewe ni wabaguzi ata wao kwa wao utasikia...
Hii mada ipo nje ya uwezo wako wa uelewa,piga kimya ili usijulikane kua hujui kitu kisha jifunze kupitia wengine,achana na issue za udini hapa sio mahala pake.
 
Kuwa njama zile zilizosambaa wakati wa Uviko-19 kuhusu wakina Bill Gates waweza kuwa kweli?? Mpango wa Uviko-19 na malengo yake kwa jamii zingine, zilizodaiwa katika waraka ule wa njama, hazijafanikiwa??

Maswali ni mengi, majibu hayajitoshelezi.

Uhalisia ni kuwa, Ndio mategemeo ya Ubepari. Pata potea.

Mfunge mikandaaa 😁
 
Silicon valley sio watu walitoa pesa kwa pamoja, walinunua bonds za serikali kwa pesa za watu na mda huo powell kapandisha riba[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nafikiri hilo likafanya balance za benki zisikae sawa. Lakini bado ikawa imesimama. Watu waliposikia vitabu vya benki havipo sawa wakakimbilia kutoa pesa zao, hilo ndilo likaleta kufilisika
 
Wiki iliyopita Benki ya Marekani Silicon Valley Bank ilipatwa na bank run(watu wengi kutaka kutoa pesa benki kwa pamoja) na kupelekea kufilisika. Tena benki ya pili, Silvergate, imepatwa na kitu kama hicho.

Haya mambo yanaashiria nini? Tujipangaje?
Hii inakwambia na wewe kama una pesa zako benki zitowe.

Ukiona mwenzako ananyolewa, tia maji zako.
 
ile ilikuwa a classic case ya bank induced panic, walipotoa news kuwa wanataka cash injection from equity markets , hedge funds nyingi zilitoa pesa haraka kupelekea collaspe ya benki.

Ila dont read too much into it, isipokuwa credit suisse , all major banks za dunia i.e Jp morgan , BOA , Goldman sachs ukiangalia reports za financial stress tests na liquidity ratios vs leverage portfolio zao wako sawa currently .
Ila risks to tier 2 banks and below bado zipo
Shida ni kuwa kitu kama hiki kinaweza sababisha msululu wa bank runs. Na benki hata iwe stable vipi, haiwezi kustahimili hii kitu.
 
Back
Top Bottom