T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Bailout inatolewa na serikali kwa makampuni makubwa kwenye market fulani ili yalinde market nzima. Ulaya serikali hazinaga wivu kwa biashara zao, sio kama sisi huku.Ndio maana waliunda FDIC Kule Marekani wao ndio insuerer wa hiyo kitu benki ikifaik wana take over kuhakikisha wateja wanalipwa pesa zao na kuendesha hiyo benki au kuuza assets za hiyo benki mpaka sintofahamu itakapoisha ,wamefanya hivyo jana kwa Signature bank , ingawa kwa giants kama city banks ,Morgan Stanley , JP Morgan NK wao ni too big to fail ,wao huwa wanapewa" bailout " au fidia na serikali ili kufidia hiyo pesa ya hao wateja , ndio maana kuna mjadala Marekani wa kwanini zinapofail hizo bank ndogo wao wanafilisiwa lakini banks kubwa wao wanapewa " bailout " ambazo ni pesa za walipa kodi ,
South Korea walikuwa wanatoa bailout kwa Hanjin shipping ili kulinda shipping business iliyokuwa mpya na Hanjin ndio ilikuwa kubwa. Kuiacha Hanjin ife ilikuwa ni sawa na kuacha shipping lines zife, hata hivyo management walikuwa wahuni kampuni ikashindikana na South Korea marais wake wastaafu mara nyingi wanafungwa kwa matatizo yanayotokana conducts za biashara. Au Daewoo nzima inavyolelewa.
Na kampuni nyingine ni matter of national interest. Marekani haiwezi ruhusu shipbuilder kama Huntington Ingalls kufirisika, sasa nani atatengeneza meli kubwa za kivita na aircraft carriers.
Wala Marekani piga ua haiwezi kubali kupoteza market share ya ndege ndio maana Bombardier iliwekewa figisu hadi Wacanada wakaiuza kwa Airbus. Niliyokuwa na wasiwasi nayo ni Embraer ila naona wamejiwahi kujipa security. Na Airbus iko vile kwa sababu ni consortium, Marekani alizembea McDonnell Douglas ikafeli ikanunuliwa na Boeing kwahiyo hakuna mbadala.
Serikali duniani huumia sana kampuni zao kubwa zinapopotea kwenye soko la dunia, Finland maumivu ya Nokia hayawezi isha. Sasa Marekani iwaache wababe kwenye banking kama Chase ili benki moja ifeli iporomoshe uchumi mzima. Mwaka 2008 wale AIG waliokuwa wanaonekana kwenye jezi za Man U muda fulani walikuwa bailed out zaidi ya $80 billion na ndio waliosababisha 2008 Economic Crisis.
Uzuri wa Federal Reserve haifanyagi kazi kisiasa muda ule AIG inakopeshwa tena serikali ilishasema imechoka kukopesha anayekufa afe.
Kwenye COVID-19 nilimuona Jerome Power Chair wa Fed anatangaza stimulus package ya zaidi ya $2 trillion bila kuingiliwa na Rais wala nani serikalini wakati huo tuna Magufuli hapa ananunua ndege mbili serikali nzima inaamia airport kuzipokea.
Na kitu kingine, ili kuondoa risk Marekani haipendi kampuni iwe kubwa kupitiliza au iwe na monopoly. Naamini Marekani haifurahii Apple kukua sana bali inapendelea ingetokea kina AT&T wawe na ushindani pale. Miaka ya nyuma sikumbuki ila ni before WW2 waliivunja Standard Oil ya number one billionaire John D. Rockefeller (mtoto wake alikuwa kiongozi wa New York, mjukuu wake alipotea kwenye misitu ya visiwa fulani akatafutwa hadi na meli za kivita). Standard Oil ilikuwa kubwa kupitiliza, makampuni mengi ya mafuta unayoona leo yana roots kutoka Standard Oil.
Au hata kwenye banking mzee J.P Morgan alikuwa na domination kwenye mabenki na yakavunjwa yanauzwa na kuunganishwa siku hizi mara utasikia JP Morgan Chase, Morgan Stanley