Beno Kakolanya imeinajisi kazi yake

Beno Kakolanya imeinajisi kazi yake

beno ana familia.inamtegemea na ile ni kazi yake
hata messi akiona mambo hayaendi vizuri kwenye mikataba uwa anagoma.
dawq ni kumlipa hela zake.
sio mshahara elewa ni hela ya usajili ,familia itakufaje njaa kwa hela ya usajili wakati mshahara anapata
 
FAMILIA YAKE UTAIHAMISHIA CHUMBAN KWAKO UWAPE MALAZI AMA.MNAKODOA NA JF ILIMRADI MSOMEKE .......

ACHENI UPUUZI WAKUSAJILI WATU UWEZO HAMNA WAKUWALIPA YUKO WAPI NGOMA KAPUMZIKA ANAKULA.MSHAHARA MWAKA.MZIMA MNADANGANYA ANAUMWA KUMBE ANATAKA CHAKE NA UNAJUA YANGA WALIISHIA KUMLIPA SH NGAPI

MNAPOANDIKA ANGALIA UNGEKUWA WEWE N FAMILIA YAKK.MNGEFANYAJE MUHIMU SANA.....

MFIKE WAKATI MJUE KUSAJILI NA KULIPA WACHEZAJI MISHAHARA VITU VYA KUANDALIWA SIO KUKURUPUKA MWONEKANE
Ziko njia nyingi za kulalamika, lakini kugoma kucheza sio mojawapo Kwa mchezaji, maana kazi ya mchezaji inaimarika kadri anavyopata mechi nyingi. Wachezaji wengi wanaojitambua hawagomei mechi bali wanagomea mkataba mpya au huomba kuvunja mkataba katikati ya mkataba na msimu.
Ukiona mchezaji anakwenda kujificha siku ya mechi kama njia ya kuwasilisha malalamiko yake mchezaji huyo hawezi kufika mbali kisoka hata kama angekuwa na kipaji kama mchwa. Yeye ni short sighted kwelikweli, hand to mouth, tumbo street. Yaani kafika hapo alipofika. Nina uhakika hata yeye sasa hivi anajutia kwanini alitumia njia Ile ya kudai na kuisahau profession yake.
 
Hakuna mchezaji wa ligi kuu -TPL aliyenyanyaswa na yanga kama kama beno, apo alipo anadaiwa milioni 5 na timu aliyokuwa amesajiriwa nayo baada ya kutangaziwa na yanga kuwa anaachwa, apo alipo kwenye mkono wake wa kulia kuna mkataba wa milioni30 kutoka simba ambao bado hajausaini, mkono wa kushoto ana madeni chungu mzima yaliyo sababishwa na yanga na wanayanga tumeshindwa kumchangia japo milioni10 ili kumbakisha lakini kwa yondani iliwezekana.......alooo mistake tufunguke hapa yasiyo paswa....
Itapendeza zaidi kama ukianza na hata tulaki tu moja.
 
Aaaa! Beno hasomi alama za nyakati, kazi yake ya ugolikipa ni kazi takatifu haitaki vitendo kama hivyo alivyofanya. Hii ni sawa na kuitia najisi kazi yake ya ugolikipa.

Hakuna timu makini duniani itapenda golikipa mwenye historia ya tabia kama hiyo ya kugoma anapokuwa na shida hasa ya kifedha. Hii inamaanisha kuwa golikipa kama Beno ana uwezo wa kuchukua fedha kutoka timu pinzani na kuiuza mechi ili kukidhi shida yake ya kifedha ambayo mwajiri ameshindwa kuiona au kuitimiza.

Aliyemshauri Beno kufanya hivyo alikosea sana kupita kiasi. Beno hataaminika pahala popote duniani kucheza kama golikipa, maana hawatajua akikasirishwa na uongozi atachukuwa hatua gani kama sehemu suluhisho ya shida yake.

Namshauri Beno aende Yanga akapige magoti kuomba msamaha kwa alichofanya ili kujisafisha. Yeye bado mdogo sana, anazo kesho nyingi sana ambazo zitahitaji umakini na trust ya hali ya juu wa wadau mbalimbali anaowafahamu na asiowafahamu.
tungefungwa angetulipa nini?
 
Wengi wanaoshabikia ni simba ambayo walimshawishi agome ili mechi za mikoani yanga ifungwe bahati mbaya kwao ilo halikuwezekana.
Sasa hv anajuta maana hatocheza na dirisha dogo ndio linafungwa hivyo.
 
Mna kipa pazia tu mchukueni Beno
Ugolikipa ni namba takatifu haitaki najisi kama hii. Rafiki wa adui yako ni adui yako pia, Beno hawezi kuwa na meneja shabiki wa Simba halafu akaachiwa adakie Yanga, kufanya hivyo ni ujuha wa hali ya juu. Zahera ana akili nyingi sana kupita kiasi kwa kumkataa Beno kurudi Yanga.
 
Wengi wanaoshabikia ni simba ambayo walimshawishi agome ili mechi za mikoani yanga ifungwe bahati mbaya kwao ilo halikuwezekana.
Sasa hv anajuta maana hatocheza na dirisha dogo ndio linafungwa hivyo.
Atapata muda mzuri wa kukaa na familia yake iliyosababisha amgomee kocha wake. Atagundua kuwa pesa sio kila kitu kwenye football. Kama kuna mwanachama na shabiki wa Yanga mwenye pesa au mbinu ya kuboresha kipato cha Yanga aupeleke mchango wake kwenye club ikasaidia kutatua shida za club na sio kutafuta kick kwa wachezaji wanaogomea mechi, kufanya hivyo ni sawa na kulipa kikombozi kwa maharamia ili wawaachie mateka wao, kesho watateka wengine ili kulipwa tena, na maharamia wengine zaidi wanaweza kuibuka kuteka watu kama njia ya kujipatia fedha.

Hebu fikiria iingekuwaje kama Yanga ingefungwa mechi zote ambazo Beno aligomea kucheza?

Hafai
 
Back
Top Bottom