Aaaa! Beno hasomi alama za nyakati, kazi yake ya ugolikipa ni kazi takatifu haitaki vitendo kama hivyo alivyofanya. Hii ni sawa na kuitia najisi kazi yake ya ugolikipa.
Hakuna timu makini duniani itapenda golikipa mwenye historia ya tabia kama hiyo ya kugoma anapokuwa na shida hasa ya kifedha. Hii inamaanisha kuwa golikipa kama Beno ana uwezo wa kuchukua fedha kutoka timu pinzani na kuiuza mechi ili kukidhi shida yake ya kifedha ambayo mwajiri ameshindwa kuiona au kuitimiza.
Aliyemshauri Beno kufanya hivyo alikosea sana kupita kiasi. Beno hataaminika pahala popote duniani kucheza kama golikipa, maana hawatajua akikasirishwa na uongozi atachukuwa hatua gani kama sehemu suluhisho ya shida yake.
Namshauri Beno aende Yanga akapige magoti kuomba msamaha kwa alichofanya ili kujisafisha. Yeye bado mdogo sana, anazo kesho nyingi sana ambazo zitahitaji umakini na trust ya hali ya juu wa wadau mbalimbali anaowafahamu na asiowafahamu.