The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
View: https://www.youtube.com/live/nvKNTGAG-9Q?si=H3CYz7QBr2c2gMz9
Sasa unaweza kuelewa ni kwanini hawa jamaa wa wanaojiita G55 ni wajinga wa kiwango cha huyu mzee Benson Kigaila..
Akataa katakata kujibu swali la mke wake kuwa miongoni mwa wale wabunge 19 na kwamba kama ni yeye ndiye aliyesaini fomu za NEC na kuzipeleka Tume ya Uchaguzi. Aidha, kidogo akimbie 🏃🏃🏃🏃🏃studio alipovamiwa na swali hili🤔🤔
Akubali kuwa agenda ya NO REFORMS NO ELECTION ni ya chama, lakini hawakuwa na mkakati wa kuitekeleza. Alipowekewa video yake ya siku za nyuma akisisitiza NO REFORMS NO ELECTION na chama kuzuia uchaguzi, alinywea, akachanganyikiwa na kubabaika kwa kiwango cha juu sana na kuiona studio chungu...!
Duuh, hata sijui alipata wapi ujasiri wa kwenda kuanika ujinga na upumbavu wake waziwazi kiasi hiki..
Sasa wana CHADEMA, eleweni kuwa hizi ndo akili na ufahamu wa hawa jamaa wajiitao G55...!
