Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,264
- 10,535
Zamani wakati bado naishi nyumbani alikuja paka mdogo kuomba hifadhi mimi nikamchukua, japo wazazi hawakutaka mwanzo ila baada ya muda wakampenda na kila mtu likawa jukumu lake kumuangalia,
Paka yule alikua akiniona nipo down nina stress basi atafanya juu chini niwe sawa na hatotoka chumbani siku nzima, alikua ni bestfriend wangu, nilizungumza nae mambo mengi, siku aliyokufa nililia sana, baba yangu akamzika kwa heshima,
Nilipoanza kuishi mwenyewe sikuweza kufuga Paka sababu ya uangalizi na sasa familia imekua nina tarajia kua na Paka, mnyama huyu mzuri, msafi na mwenye akili sio wa kukaa nae mbali.