TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Musiba alisema atachukua maamuzi magumu; naona ameamua kuanza na Membe. Bado Zitto Kabwe na January Makamba.
 
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mhe.Bernard Kamilius Membe, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye kufariki.
Changamoto ya upumuaji bado IPO. Mwezi huu wanne ilipamba Moto Sana. Binafsi ilitupitia watu wawili nikiwemo Mimi tarehe 24/4-9 May nikawa Sawa. Nilipambania za hospital na kienyeji Ila ukweli mziki wake si wa kitoto. Kinga ilikuwa inashuka kwa speed ya radi sema nikawa napambana kuhakilisha nakula immune boosting stuff. Ila ya safari hii haikunipiga kama Ile ya August 2021 maana kipigo kile kulikuwa kibaya mno.
Rest in Eternal Life Ben. Pesa yako Kwa msiba itaendekea kudaiwa na familia yako maana hukumu ilishatoka. Hivyo hakuna case closed maana ilikuwa imeshaamuliwa.
 
Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Sasa hapa itakuwaje au ndio Musiba kanusrika hivyo? Wanasheria mliomo humu JF tunaomba mtusaidie kudadavua hili sakata la kisheria.
 
Musiba hahusiki na kifo cha huyu bali ni Mungu ameamua kuonyesha ukuu wake dhidi ya mtu jeuri anaekaidi hadi viongozi wa dini.



Viongozi wa dini ni binadamu wa kawaida na wao wana yao mazito chungu nzima [emoji108]

Imeandikwa; “ yanayofanyika kwa Siri ni aibu hata kuyanena hadharani “

Moyo wa mwanadamu aujue Mungu Muumba
 
Back
Top Bottom