TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Kwa utumishi wake uliotukuka kwenye taifa hili BM, na serikali iko upande wao, imekuwaje kifo chake kitangazwe haraka haraka hivi?
Mtu amefariki sijui saa 12 saa 5 asubuhi taarifa zimeshazangaa nchini na kwingineko,

Je Born to Town hana mkono kweli kwenye hili ili aweke anayemtaka yeye 2025 kitini?
Maswali ni mengi mda mchachee. Yaan full vurugu match [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Kambi ya watu wema wasiokufa imepata msiba mzito!
 
Hivi sio mwanachama la wale ambao hawafi kama tulivyowahi kuambiwa na mzee Yusufu?
Hivi yule aliyetabiriwa kufa kwa kisu akaamua kujificha, lakini bado alikufa kwa Kisu licha ya kujifungia, ilikuwa kwenye hadithi za Abunuwasi
 
Back
Top Bottom