Sema ukweli tu kwamba wewe ni kati ya walioumizwa na kifo cha kipindi kile na sasa umeufurahishwa na kifo cha sasa hivi ila unajaribu kufanya ni ku present kwa namna ya kubalance ila lengo kuu wajitokeze wenzako kushangilia kupitia uzi huu.
Ila ujue tu kwamba, unao watafuta wala hawakuwahi kuwa upande wa Membe, ilitokea tu wakayaonga mkono madai na misimamo yake dhidi ya mtu wenu.
Kwa kujaribu kulazimisha kumuinua Membe ili mjisikie faraja inadhihirisha ninyi na mtu wenu mlikua ni Public enemies ndiyo maana hamjui ni wakati gani hasa wale mliowaumiza na wao mtawaona wakiumia na labda ndiyo maana sasa hivi kila matukio ya kuumiza watu yakitokea mnashangilia.
Wananchi wakilalamikia tozo mnaishia kusema ndiyo, lipeni tozo, si mliona mwendazake hafai?
Mkiona ajali zinawaumiza watu mnafurahia.
Vitu vikipanda bei na kuwaumiza watu mnafurahia.
Watu wakiuawa mnafuahia.
Huduma zikiwa mbovu na kuumiza watu mnafurahia.
Chochote kibaya sasa hivi mnakifurahia ili mradi kiumize watu.
Hii yote ni sababu washiriki wa utawala ule na wafuasi wao wote walikua ni public enemies.