Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Eeh kama unavyojua kuimba kupokezana, tuwaache Magu jazz band watumbuize jukwaa lao leo 🤣🤣🤣So tuwaacha watu wapasue nyongo mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Eeh kama unavyojua kuimba kupokezana, tuwaache Magu jazz band watumbuize jukwaa lao leo 🤣🤣🤣So tuwaacha watu wapasue nyongo mkuu.
Hapana kaka kucheka kupokezana ila cha muhimu wema hawafiUsilipize ubaya kwa ubaya ndugu yakupasa uwaombee wale wanaobehave kama wanyama kitu pekee kinachotutofautisha binadamu na wanyama ni uwezo wa kutambua mema na mabaya vinginevyo tutakuwa hatuna tofauti na punda.
Mzoga utasafilishwa auMnatupigia kelele na mzoga wenu.
Kiukweli kabisa tangu nizaliwe hakuna msiba niliouona watu wanasherehekea na kumsifu na kumshukuru mungu kama kifo cha magufuli,mfano mtaani kwetu kuna daktari alichinja mbuzi kama shukrani
Maneno hayo ungewaambia kwanza walamba asali, hembu tutolee uchuro hapa, walamba asali walifurahi hadi kwenye mikutano ya chama chao walikuwa wanafurahi na kuimba mapambio na hatukusikia ukilalamika, wazuri hawafi mkuu babu yako alisema.Wanaoshangilia kifo ni wajinga. Kifo hata ushangilie kwa adui yako bado na wewe utakufa tu iwe leo au kesho. Sioni sababu ya kushangilia kufo maana wote tutakufa
Tuyasahau tu mkuu.Hapana kaka kucheka kupokezana ila cha muhimu wema hawafi
Daaah! Nawaona wamekaba kila kona mkuu.Eeh kama unavyojua kuimba kupokezana, tuwaache Magu jazz band watumbuize jukwaa lao leo 🤣🤣🤣
Bado huyu!
Mpaka aende mwingine ile timu yao huyu sisi ni kama maiga agustino jasusi wetu ko bado wengineTuyasahau tu mkuu.
Du nilishamsahau Mabere Marando kama yupoMembe amezaliwa mwaka 1953 na amefariki mwaka 2023, ni miaka 70 net.
Huyo tayari amekula chumvi na anaweza kufa kwa pressure tu katika umri huo, na ni bora ufe kuliko pressure ikuletee major stroke ni mateso matupu kwako na familia yako, unaanza kuhudumiwa kama mtoto Mchanga kubadilishwa pampas na kulishwa.
Kwa tuliopoteza wapendwa wetu kwa maumivu makali, Membe amekufa kifo chema bila mateso wala familia kuteseka.
Ni unafki tu unatusumbuwa lakini wengi tunatamani mwisho mwema kama wa Membe, ni wachache wanaopata bahati hiyo.
Mabere Marando yupo hai lakini ni sawa na mfuko tu, sasa yote ya nini hayo?
Kuna kiongozi hajawakosea watanzania?Mkuu achaa nipate ban, moja ya watu wajinga nchii hii wenye vichwa venye funza niwewe, whenever you type inaonyesha you are so confused stupid na pia always grabbing attention stupid ass. Haiwezekani sabaya ,musiba na so your type hawajakosea wa Tanzania.
Nilijua kabisa hutanielewa. Basi tusubiriMahakama ikiamua utalipa tu, mbona kina Mbowe walipigwa fine ya million 300 na wakaambiwa walipe au wafungwe!!?
Kama hauna una file bankruptcy Mali zako zipigwe mnada au mshtakiwa anaweza kukupeleka jela mpaka ulipe!!
Mahakama Haina ujuaji ni haki bin haki
Sasa hiyo CV mlio iweka hapa anaenda kuomba kazi huko PEPONIView attachment 2618772
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.
Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.
Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe.
Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.
#Elimu
1962 – 1968: Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.
1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi
1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora
1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais
1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika ofisi ya rais
1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law)
1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi wa mambo ya ulinzi na usalama
#Mafunzo.
Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitimu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.
Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza. Aidha, mwaka 1980, Ndugu Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam.
#Familia.
Mwaka 1986, Ndugu Bernard Membe alifunga ndoa Takatifu na Dorcas Richard Masanche, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Ndugu Membe na mama Dorcas wamejaliwa kupata watoto watatu, Cecilia, Richard na Denis.
#Siasa.
Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.
Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.
Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.
Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyekuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo.
Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.
#Mafanikio:
Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.
Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.
#Uchumi:
Bernard Membe amesimamia vema utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya uchumi ili kuwezesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuininua hali za wananchi wake. Ni katika kipindi chake, nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika eneo la viwanda, gesi, makaa ya mawe, kilimo na utalii. Chini ya uongozi wa Ndugu Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilipata tuzo ya utendaji bora iliyotolewa na sekta binafsi kwa kutambua mchango mkubwa wa Wizara katika kukuza sekta binafsi Tanzania.
Kudumisha mahusiano kimataifa: Katika kipindi chake, Tanzania imefanikiwa kuipaisha Diplomasia yake katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali mashuhuri kama, Marais George W. Bush na Baraka Obama wote wa Marekani, Xi Jinping wa Uchina, Joachim Gauck wa Ujerumani, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Piere Nkuruzinza wa Burundi, Joseph Kabila wa DRC, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Mwana wa Mfalme wa Malkia wa Uiengereza, na Mwana wa Mfalme wa Japan.
Pia chini ya uongozi Ndugu Bernard Membe Tanzania imefanikiwa kupanua wigo wa mahusiano yake Kaimataifa kwa kufunguwa Balozi mpya katika nchi za Malaysia, Brazil, Comoro, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait. Aidha, Wizara imefanikiwa kufungua upya Ubalozi wa Tanzania the Hague, Uholanzi uliofungwa mwaka 1994. Kadhalika Balozi Mpya za Brazil, Oman, Uturuki, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Namibia zilifunguliwa hapa nchini.
#Kutambuliwa:
Kwa kutambua mchango wake katika kurejesha hali ya amani na utulivu katika Visiwa vya Comoro, mwaka 2008, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa watanzania waliotunukiwa Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro na rais Jakaya Mrisho Kikwete.
#Uozefu:
2006 – hadi sasa: Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC
2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM
2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
2006 – Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa
2013 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth
2014 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
06/08/2020- Membe alijiunga na ACT-Wazalendo baada ya kufukuzwa katika chama tawala CCM.
02 Januari 2021 - 2021Alijitoa ACT baada ya kuahidi kwamba angejiuzulu nafasi yake ya ushauri mkuu wa ACT-Wazalando na uanachama wa chama hicho kwa mpigo.
Amekuwa mjumbe wa kamati za usuluhishi katika migogoro kwenye nchi za Sudan ya Kusini, Madagascan na katika mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
Pia Tanzania imefanikiwa kushiriki katika zoezi la Uangalizi wa chaguzi kwa niaba ya SADCC katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagasca, Kenya, Comoro na Afrika ya Kusini.
Kazikwe naye Chato kama inakuuma sana.Unacheka kama shoga!
Mzoga wako upo hapa Lugalo unasubiri kuzikwa wiki ijayo mkuu!!Kazikwe naye Chato kama inakuuma sana.
Naaah sio wangu, sipo CCM Mimi haunihusu.Mzoga wako upo hapa Lugalo unasubiri kuzikwa wiki ijayo mkuu!!
Mungu fundi kama umeumizwa kazikwe nae rondo. Wazuri hawafi bwanaNatumaini mnafaidika sana na hizi kuni mnazozichochea.
Nilimpenda JPM lakini sikuwa na amani kwa namna alivyokuwa anashughulikia waliompinga
Membe ni alama ya ushujaa kwa sababu yeye na Fatma Karume ndiyo walioudhihirishia umma kuwa awamu iliyopita ilitumia rasilimali za nchi kuwasakama na kuwatisha waliomkosoa mtawala. Sote tuliona matokeo.
Leo unaposimama kuzidisha uchochezi kuwa vifo vya hawa viongozi wetu vina timu za ushabiki ni wazi hata wewe ni mmoja wa wanaosheherekea vifo vya watu uliotofautiana nao.
This must stop
Lala pema Membe
Poleni sana kwa kuondokewa na ankoli, na pia hongera sana kwa kupambania mjomba azikwe kwa heshima zote nyumbaniMimi Mwili ukiwasili tu nitauagia hapa hapa Dar es Salaam na kwa wale Wazanaki mliopo Busegwe Wilayani Butiama na mlio njiani sasa kuelekea huko Musoma Mkoani Mara na Kaka Mkubwa aliyetangulia Kijijini mtaniwakilisha katika Maziko kwani nina Msiba mwingine wa Kuuhudhuria wa Mmwela Mkwere wa ghafla Jana.
Cc: Bujibuji Simba Nyamaume na Dr Matola PhD
Sikuoni hapa Kijijini Londo Mkuu.Kwa sasa tutulie tuzike kwanza mpendwa wetu,huku kujibizana hapa hakutuondolei machungu ya kupigwa na kitu kizito kichwani na Mungu.Kazikwe naye Chato kama inakuuma sana.