TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
View attachment 2618749
TANZIA: Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Bernard Kamilius Membe, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye kufariki.

Kwa taarifa zaidi endelea kuwa nasi

#RIPMembe
#ITVUpdates
Walimwengu washamuua kwa shirki kulinda maslahi ya watu.. Tanzania na shirki ni kama kaka na dada.. RIP Membe..
 
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Benard Membe pia alikuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14
Apumzine kwa Amani
 
Ila watu walimwambia aachane na Musibu hasa wazee wa Kanisa
 
Kuhusu deni lake Musiba atakesha baa leo
Hapana hawezi kukesha kwa sababu Ile Ni amri ya Mahakama na Kuna Sheria ya Urithi na mirathi kaisome vizuri! Kuna kipengele "kukusanya Mali na madeni ya marehemu" pale Ni pagumu hasa ukizingatia Membe kwenye Kesi ya Msingi alijumuisha familia yake na kwa maana hiyo atakayetake charge kwa niaba ya baba ataorodhesha pia miongoni mwa watu ambao baba anawadai Ni Musiba na iko clear kwamba kuna hukumu ya kimahakama! Labda familia imsamehe! Lakini bado Yuko Liable to pay!
 
Back
Top Bottom