TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.

Taarifa za hivi punde zinasema Benard Memba aliyewahi kua Waziri wa Mambo ya nje amefariki Dunia katika hospital ya Kairuki alipopelekwa baada ya kuugua kifua kwa muda mfupi.

Souce: ITV
Kifua Kwa muda mfupi eehh !!! Tayari!!.

Vita kaishinda Musiba !!, haiwezekan Cyprian Musiba, Akina Makonda, Kazi kubwa waloifanyia Taifa hili Kwa Miaka mitano.

Et Leo, Utake kuwaumiza, na ubaki hai?. Haiwezekani .

Kwa maoni yangu Mimi, Mtu yoyote anayejaribu kusaliti Nchi na Juhudi za Nchi kusonga mbele, huyo mtu Hafai Kuishi !!.
 
Kwani jamani WE
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.

Kwani WEMA NAO HUFARIKI?
 
Bush lawyer, pesa za marehemu ni mirathi ya familia, vitu vikipigwa mnada pesa inakwenda kwenye account ya mahakama, baada ya mirathi Msimamizi wa mirathi anajaza fomu ya kugawanya pesa za marehemu zilizopo kwenye bank zote kwa wanufaika wa mirathi.

Endeleeni kudanganyana, Membe amejenga msingi mzuri wa kuwatia adabu waropokaji wote.
Nani atanunua tena mali ya Musiba? Huo mnada ushakuwa kimavi!
 
Back
Top Bottom