TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Duuuh, Mungu huwa anashangaza sana

Binafsi sikuwahi kutegemea kama viongozi wakubwa hawa

- Samwel Sitta, JPM, Benard Membe wangeondoka wamuache EDWARD LOWASSA akiwa Hai

KIFO ni Ibada, tusisahau hilo, Tupendane na Tutendeane mema

Mungu anaamua yupi aondoke kwa muda gani na KWA HAKIKA Pesa, Jina na Umaarufu sio kigezo cha kuwa Hai

Mungu awafariji wafiwa wote.
 
Kutoka Mwibara...
1683889175000.jpg
 
Sijui sheria ila nataka kujua kama mahakama ikiamua A amlipe B kiasi C, B akifa, A atamlipa nani?
Swali zuri.

B anapokufa mrithi wake uhuisha mambo yote ya kisheria. Yaani kama Marehemu anadaiwa basi mrithi anawajibika kulipa na kama anadai mrithi ndiye atakayelipwa.

Kwa maana nyingine hukumu ya Mahakama husimama hata kama Marehemu hana ndugu au watoto. Wasii Kabidhi Mkuu ndiye husimama kwa niaba ya Marehemu kama hajaacha watu wa Karibu baada ya kifo chake.
 
Tumefika hapa kwasababu wapo wajuaji waliogoma kusahau yaliyopita, wayaache yaende, hawa wakajiona wamekaa juu wamefika, wao kila siku ikawa ni kumuimba marehemu mtangulizi, wasikumbuke nae alikuwa na wapendwa wake, wakajisahau wakidhani kifo kina undugu au urafiki, leo kifo kimewakumbusha hakina mwenyewe, sote tunapita.

Sio wakati wa kulaumiana tena, maisha ni fumbo, tujifunze kuyaacha yaliyopita yapite, lakini sio kujisahau na kujipachika majina ya ajabu kama wazuri hawafi au Mungu fundi, leo majina hayo hayo yanarudishwa upande wa pili, ni vyema wahusika wayapokee kwa mikono miwili kama walivyoanza kuwapa wenzao, time to feel a test of your own medicine.
Hii ntaiscreen shot nimtumie Nape na Makamba
 
Alimpiga vita sana Lowassa pamoja na Sitta.
Wapite hivi
Kutofautiana kwenye maisha ni swala la kawaida, hizi habari za kumsema mtu aliyetangulia kwamba alikuwa na ugomvi na flani au flani hazifai kabisa.

Na sidhani kama kuna mtu ataondoka kwenye hii dunia akiwa amepatana na watu wote, hata mitume wa Mungu waliondoka wakiwa na ugomvi na watu wengi waliowaacha.

Cha msingi ni kujitahidi kuishi kwa amani na kuombeana safari ikifika.
 
Labda kafanya mavitu yake kule kijijini aliokuwa amejichimbia. Ni muda sasa atarudi mjini toka huko mafichoni.
Aje alipe deni; kachelewesha mpaka muathirika kafa, ikibidi familia imuongezee madai ya kuchelewesha kulipa!!
tunaingia episode 2
 
Back
Top Bottom