TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Kama Taifa tunatakiwa tutoke kwenye siasa hizi za chuki zilizozalishwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Baada ya Uchaguzi ule na John Pombe Magufuli kuingia madarakani, kulitokea uhasama mkubwa sana kati ya watu waliokuwa wanamuunga mkono na wale waliokuwa wanapingana na staili yake ya utawala.

Leo Baada ya kutangazwa kwa Kifo cha Bernard Camilius Membe, unaona kabisa limeibuka kundi la watu humu JF ni kama wanahanikiza furaha yao kwa kifo cha Membe. Watu hao ambao wanajificha nyuma ya kuonesha furaha kwamba Cyprian Musiba hatalipa tena hela alizotakiwa kumlipa Membe, lakini kwa undani unaona kinachowafurahisha zaidi ni kuona mmojawapo wa wapinzani wa Magufuli naye Kafariki.

Wakumbuke kwamba ni wao waliokuwa wanasema wakati wa msiba wa Magufuli kwamba "hakuna atakayeishi milele" na Leo ni ushahidi mwingine kwamba hakuna atakayeishi milele.

Watu wafanye maridhiano dhidi ya nafsi zao!!
Mungu ailaze roho ya BM marahali pema peponi. Tukiwa tunaomboleza msiba wa BM, bado tunakumbuka sana kauli chafu na mbaya za Mbunge wa Mtama (Nape) aliposema kifo cha Dkt Magufuli eti kaamua Mungu ugomvi, na Mzee Makamba aliposema wazee walifika wakasema sasa basi inatosha na wazuri hawafi. Nadhani Nape huko alipo keshajibiwa jibu lake na Mungu kuwa aliyoyatamta kuwa Mungu kaamua ugomvi basi na yeye mtu wake wa karibu aliyekuwa na ugomvi na Musiba kimemtokea hicho hicho. Na tulishaonya hapa jukwaani muda sana kuhusu hii tabia na kibaya zaidi Rais Dkt Samia anawachekea tu hawa waropoka ovyo kiasi kwamba hata yeye anaonekana alishangilia kifo cha Dkt Magufuli. Rais Dkt Samia kifo cha BM kiwe fundisho kwake, apige marufuku dhihaka dhidi ya Dkt Magufuli, na hii tabia ya kushangilia vifo vya viongozi ikomeshwe. Nategemea humu jukwaani memba wale BAN wanaoshangilia kifo cha Dkt Magufuli na BM. Na hii habari tulishasema wanaompenda Dkt Magufuli ni wengi sana tena sana.
 
Duuuh, Mungu huwa anashangaza sana

Binafsi sikuwahi kutegemea kama viongozi wakubwa hawa

- Samwel Sitta, JPM, Benard Membe wangeondoka wamuache EDWARD LOWASSA akiwa Hai

KIFO ni Ibada, tusisahau hilo, Tupendane na Tutendeane mema

Mungu anaamua yupi aondoke kwa muda gani na HAKIKA Pesa, Jina na Umaarufu sio kigezo cha kuwa Hai

Mungu awafariji wafiwa wote.
Kweli.
Wakati Kigogo na wengine wengi wakitabiri msiba unatokea kwa mstaafu wa monduli, unatokea pasipo tarajiwa!
 
Kama Taifa tunatakiwa tutoke kwenye siasa hizi za chuki zilizozalishwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Baada ya Uchaguzi ule na John Pombe Magufuli kuingia madarakani, kulitokea uhasama mkubwa sana kati ya watu waliokuwa wanamuunga mkono na wale waliokuwa wanapingana na staili yake ya utawala.

Leo Baada ya kutangazwa kwa Kifo cha Bernard Camilius Membe, unaona kabisa limeibuka kundi la watu humu JF ni kama wanahanikiza furaha yao kwa kifo cha Membe. Watu hao ambao wanajificha nyuma ya kuonesha furaha kwamba Cyprian Musiba hatalipa tena hela alizotakiwa kumlipa Membe, lakini kwa undani unaona kinachowafurahisha zaidi ni kuona mmojawapo wa wapinzani wa Magufuli naye Kafariki.

Wakumbuke kwamba ni wao waliokuwa wanasema wakati wa msiba wa Magufuli kwamba "hakuna atakayeishi milele" na Leo ni ushahidi mwingine kwamba hakuna atakayeishi milele.

Watu wafanye maridhiano dhidi ya nafsi zao!!
Ni kweli kwamba,"Hakuna atakayeishi milele" lakini akifa dhalimu watu hufurahi,Membe kafa peke yake hajabeba mizigo ya watu kafa kifo chema cha miaka 70 maana yake SABATO ikiwa na lengo la Kazi nimeimaliza acha nipumzike kwa amani nifurahie matunda ya kazi yangu.
 
Mbona wewe ulifurahia kifo cha Magufuli kwani wewe sio Expected dead?
Una ushahidi wowote kwamba Mimi nilifurahia kifo Cha Magufuli?
Kama upo nadhani ungeambatanisha hapa wakati unaandika hii post Kama haupo Ni tafsiri kwamba wewe una tabia za kusingizia ili kuifurahisha nafsi yako!

Nina mashaka na umri wako na namna ulivyokutana naambo hapa dunianiani na kujufunza ya ulimwengu huu!

Jifunze Sana kuishi na watu kuliko hisia zako
 
Back
Top Bottom