TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Mungu ailaze roho ya BM marahali pema peponi. Tukiwa tunaomboleza msiba wa BM, bado tunakumbuka sana kauli chafu na mbaya za Mbunge wa Mtama (Nape) aliposema kifo cha Dkt Magufuli eti kaamua Mungu ugomvi, na Mzee Makamba aliposema wazee walifika wakasema sasa basi inatosha na wazuri hawafi. Nape huko alipo keshajibiwa jibu lake na Mungu kuwa aliyoyatamta kuwa Mungu kaamua ugomvi basi na yeye mtu wake wa karibu aliyekuwa na ugomvi na Musiba kimemtokea hicho hicho. Na tulishaonya hapa jukwaani muda sana kuhusu hii tabia na kibaya zaidi Rais Dkt Samia anawachekea tu hawa waropoka ovyo kiasi kwamba hata yeye anaonekana alishangilia kifo cha Dkt Magufuli. Rais Dkt Samia kifo cha BM kiwe fundisho kwake, apige marufuku dhihaka dhidi ya Dkt Magufuli, na hii tabia ya kushangilia vifo vya viongozi ikomeshwe. Nategemea humu jukwaani memba wale BAN wanaoshangilia kifo cha Dkt Magufuli na BM. Na hii habari tulishasema wanaompenda Dkt Magufuli ni wengi sana tena sana.
 
Wakiendelea kumdai musiba wataputika wote,waachane na huo ujinga
Serikali hailogwi he must pay and he will pay! Hakuna Justification kwamba Musiba amehusika na kifo Cha BM,amekufa natural death! The only thin Deni lisilipwe Ni Msiba na familia yake yote kids au kusamehewa
 
Buriani Membe. Aliugua ghafla usiku au ilikuwa ni maradhi ya siku nyingi?
Lakini kwa umri wake miaka 70 huwezi kumwita kijana.
Halafu yenye ni kiongozi wa Kitaifa lakini hakwenda hospitali ya Mzena ingawa ipo equidistant na Kairuki kutoka pale nyumbani kwake.
 
Hata kama Membe kafa, deni liko pale pale. Na msimamizi wa mirathi hataweza kumsamehe Musiba kama ambavyo angefanya Membe mwenyewe.

Hivyo, kifo cha Membe ni kibaya zaidi kwa Musiba hata kama atakuwa "anachekelea" sasa
Wishful thinking
 
Narudia shimo la kwako bado lipo pale pale! Huyu kaziba lake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] km umeumia sanaa ungana nae huyo Membe wako mzikwe wotee.

Nitoleee kelele zakooo, liaa wee ukichoka futa machozi, afu utuletee ratiba ya mazishi.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Changamoto ya upumuaji bado IPO. Mwezi huu wanne ilipamba Moto Sana. Binafsi ilitupitia watu wawili nikiwemo Mimi tarehe 24/4-9 May nikawa Sawa. Nilipambania za hospital na kienyeji Ila ukweli mziki wake si wa kitoto. Kinga ilikuwa inashuka kwa speed ya radi sema nikawa napambana kuhakilisha nakula immune boosting stuff. Ila ya safari hii haikunipiga kama Ile ya August 2021 maana kipigo kile kulikuwa kibaya mno.
Rest in Eternal Life Ben. Pesa yako Kwa msiba itaendekea kudaiwa na familia yako maana hukumu ilishatoka. Hivyo hakuna case closed maana ilikuwa imeshaamuliwa.
Mkuu mimi kama mtaalamu wa afya nakushauri usichanganye dawa za kienyeji na hospitali

Utapata shida moja kubwa sana ambayo hutojua ufanye nini

Nmekushauri unaweza kuchukua ushauri au kuupotezea
 
Back
Top Bottom