Bernard Kamilius Membe, aingia 18 za Genge la Cyprian Musiba. Nini tutarajie?

Bernard Kamilius Membe, aingia 18 za Genge la Cyprian Musiba. Nini tutarajie?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Sasa nataka kuona hii ngoma Membe ataichezaje.

Bernard_Membe_2009_(cropped).jpg

Bernard Membe

Baada ya Mahakama kuu ya Tanzania, masijala kuu Dar Es Salaam kumtaka Cyrpian Musiba kumlipa Bernard Membe TZS 9.9 Bilioni, kwa kosa la kumchafua kupitia magazeti yake, Kampuni ya Yono Auction Mart ilipewa Idhini na Mahakama Kupiga Mnada Mali zote za Musiba Ili Kumlipa Membe Fidia inayohitajika baada ya Musiba kudai hana hela za kulipa.

Sasa wale waliokuwa wanamuunga Mkono Musiba na Uchafu wake waliopo kwenye Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Samia Suluhu, Wamekunjua Makucha. Kigogo mmoja wa juu kwenye Mhimili wa Haki amedaiwa kucheza na kesi hii ili kupindua meza.

Kundi la watu ‘wenye nguvu’ wameingilia kati hukumu hiyo na kuwataka YONO wasithubutu kugusa mali yoyote ya Cyprian Musiba kama wanataka kuendelea na Udalali Tanzania. So Wachague moja, kuacha kufanya hiyo kazi au wafutiwe leseni Mazima.

musiba.jpg

Cyprian Musiba

Kwanza hapa tunapoongea, inadaiwa YONO ameshanyang'anywa Leseni yake ya kazi. YONO kakaliwa Kooni anakaguliwa kila kazi alowahi kufanya na kila aina ya Figisu anafanyiwa

Hawa Watendaji wa Serikali ambao nasikia Wanajiita Sukuma Gang, wamemuhakikishia Musiba hakuna baya litamkuta just atulie tu.

Sasa Membe anahaha jinsi ya kukusanya Mabilioni yake kwa sababu aliyepewa kazi ya kukusanya hayo Mabilioni kanyang'anywa Leseni ili ifanyiwe ukaguzi kwa miezi 6.

Baada ya Miezi Sita, Membe atakuta kuna chochote kinamilikiwa na Musiba?

Hapo ndo nimegundua Musiba hayupo peke yake. Kuna kikundi kikubwa cha Watu nyuma yake kikiongozwa na kigogo huyo wa Mhimili wa kutoa Haki.

Je, hawa watu wenye uwezo wa kuingilia Mahakama na Mahakama ikaufyata, watashindwa nini kumchezea figisu Samia ili asigombee 2025?

Hii imetoa nafasi kwa Samia kujua wale wanaompinga ambao anaambatana nao.

Musiba ni Mmiliki wa magazeti yanayotuhumiwa kuchafua watu ya Tanzanite, Fahari Yetu na Tanzania perspective. Magazeti siku nyingi yanalalamikiwa kwa kuandika habari kinyume na maadili ya uandishi.

Pia soma: Chalamila: Katiba Mpya ni muhimu, Katiba ya sasa inawezekana akapatikana Makamu wa Rais mchawi akamroga Rais ili yeye awe Rais wa nchi

2. Jaji Mkuu: Hakuna mtu yeyote anatakiwa kumwingilia au kumpigia simu Hakimu ambaye kesi fulani ipo mbele yake

3. Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua
IMG-20230502-WA0012.jpg
IMG-20230502-WA0013.jpg
IMG-20230502-WA0014.jpg
IMG-20230502-WA0015.jpg
IMG-20230502-WA0016.jpg
 
Je yote yanayofanyika juu ya Mali za MUSIBA kupigwa mnada nikwa amri ya MAHAKAMA?. Au amri ya MEMBE?. Je kuna watu wanaweza watu wengine kutekeleza Maamuzi ya MAHAKAMA, naamini kama wapo basi nae ni mmoja tu ambae ni Raisi wa nchi ambae nae atafanya bila kufata Sheria na Taratibu.
 
Umeandika ukiwa umelewa?
Kwani Mahakama ikitoa hukumu huwa inataja nani auze mali ya mdaiwa?

Hiyo ni kazi ya Membe sio Mahakama, hata kama YONO kazuiwa atatafuta dalali mwingine wa kuuza
Hakika mali za Musiba zitauzwa tu
 
Back
Top Bottom