Tetesi: Bernard Kamilius Membe Meets CHADEMA top officials, The 2020 election tops the agenda

Mwache aje tuu,Mbona hiyo poa sand,chadema ni chama making kama tulivyokuwa nayo kwenye Ukawa na kina watu making wanaojitambua.
Lowasa alikuja na kaondoka,Sumaye kaja naye kaondoka na wall Chadema haikuyumba.
Tunamshukuru sana Lowasa kwa kutuongezea kura za Uraisi ambazo zimetupatia ruzuku ya kutosha kuendeshea shughuli za chama.
Na yeye Membe Anakaribishwa ,sisi sote ni Watanzania tuna haki ya kuenda katik chama chochote kile tukipendacho bila ya kizuizi ili kushiriki siasa kwa mujuibu wa sheria. Chadema ni njema atakaye na aje. Mbona wengi tuu walituacha njiani na bado tupo poa isiasa hadi wanaamua kutupiga risasi na kutuvunja viungo kwa kipigo, na bado tuko imara? Watatengenez kila aina ya majungu lakini wajue chama ni watu na watuw wetu hasa viongozi wanjitambua na wako makini.
Tatizo la nchi hii ni kutokuwepo ruhusa ya Mgombea Binafsi ,Kama ingelikuwepo ruhusa hiyo nahisi wengi wangelitumia Ushawishi wao kugombea Uraisi bila ya chama. Nadhani huko mbele CCM wanweza kuweka kipengele hicho wakiamini kuwa kitawasaidia kubaki katika dola milele, ikiwa mwaka huu watavuka.

Tuishi kama Ndugu wa Nchi Moja ,tusiwe kama CCM na ubaya wao na hofu ya kutolewa madarakani ,wakiona mtu anawakwaza wanamtimua,na kumyima haki yake ya msingi ya kushiriki siasa nchini.
na wakiona upinzani umeimarika wanatumiahelanyingi na nguvu kubwa ili kudhoofisha.
Wanaogopa mabadiliko.
 
Mimi nawashauri Chadema wajifunze kutengeneza viongozi wao wa baadaye. Chadema inatakiwa ijikite zaidi kwenye masuala ya kufundisha itikadi na maadili ya kiuongozi kwa vijana ili baadaye iwe na hazina kubwa ya viongozi. Hii tabia ya kutegemea makapi kutoka vyama vingine ili kugombea nafasi kubwa za uongozi inashusha hadhi ya chama. Wanachama wa chadema bado wana maumivu ya makosa yaliyo fanyika mwaka 2015 ya kumuunga na kumkaribisha Mh. Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea Urais na kisha baadaye baada ya kushindwa ameachana na chama kurudi kwenye chama chake cha zamani ambacho kilimnyima fursa adimu na yenye heshima ya kugombea Urais.
 
Reactions: amu
Acha kiherehere mwanalumumba, mnakesha mitandaoni kuongopea, CHADEMA ipo imara haitetereshwi na story zenu za kutungwa popoma ww
 


This shall never ever come to pass
 
Kwanza JPM sio jabali kama unavyombatiza. JPM hajawahi kuwa jabali na hatakuwa jabali! Inaonekana hujui historia ya haya mambo. JPM aliteswa ubunge tu na mkulima huko Biharamulo na salama yake ikawa figisu za kukatwa kwa jimbo ndipo alipopata ubunge. Uchaguzi Mkuu 2015 JPM alikuwa na asilimia 58 ya kura. Usichokijua kwa miaka 5 tangu alipoingia madarakani kumekuwepo na kampeni kubwa ya kutumia media ku brand (kampeni ambayo imewanasa na watu wa aina yako) mkaanza kumwona jabali wakati sio jabali. Utafiti uliofanyika baada ya kuwa Ikulu ulionyesha umaarufu wake ulishuka zaidi, kwa maana ya kwamba hata zile asimilia 58 alizopata kwenye uchaguzi mkuu zilishuka, na ndipo walipowafurusha TWAWEZA na kumbambika kesi ya kutokuwa raia mkurugenzi wake.

Nikurudishe kwenye mstari sasa. JPM hakubaliki ndani na nje. Achana na kelele za makundi mawili-kundi la wasio na uelewa wa kutosha, au wanaoelewa polepole ambao wanaona JPM amejenga madaraja ya juu wakati ile ni miradi na maono ya JK, wale ambao wanamwona JPM amejenga uwanja wa ndege terminal 111 wakati yale ni maono ya JK aliyoyakuta. Wale wanaomwona JPM amewafanya wanaume watulipe hela isiyofika kwenye ile ahadi ya kishika uchumba, lakini wasielewe mkataba wenye wa madini imebaki kuwa siri hata wawakilishi wao hawajui...na mambo kama hayo.

Achana pia na kundi la pili, linaloongozwa na akina gavana wa Dar-kundi la watu wanaojilia mpaka kuvimbewa ambalo tayari limempa JPM hadhi ya kuwa yesu.Hawa hawana nguvu yoyote, wenye nguvu ni wale ambao hawataki utawala wa kiimla, unaofanya kikundi kidogo cha watu waamue juu ya taifa hili. Huo ndio mgangano uliopo. Kwahiyo kilichopo hapa sio dhana uliyonayo wewe ya kubadilisha chama, bali ni kuondoa uhuni uliozingira urais...hivyo yoyote anaweza kuongoza vita vya kuondoa wahuni katika utawala wa nchi!
 
Mkuu, Chabusalu, Kwanza asante Kwa uchambuzi wako

Uchambuzi wako huu kwangu Mimi naweza kuuita ni uchambuzi usiokuwa na kiini cha kuonyesha udhaifu wa umarufu wa JPm ama pengine unayonia ya kutaka kuonesha udhaifu wa umatufu wa Magufuli Ila umeshindwa, eidher Kwa yeye amekuibia hoja zote ambazo ungeweza kuxibainisha hapa,

Ni kweli, Kwa temu hii ukiambiwa uoneshe udhaifu wa Magufuli, na serikali yake, kinyume na serikali zilizopita ambazo takribani kila eneo zilikuwa zimepwaya vibaya, usipotaja Neno Democrasia pekee, unaweza Anza kutafuta madhaifu mengine Kwa tochi

Ngoja nikurudishe nyuma, uchaguzi wa 2015 ndio ulikuwa uchaguzi mgumu kuliko chaguzi zote zilizowahi fanyika nchini mwetu Chini ya vyama vingi nchini

Sio Siri, Baada tu ya Mh E.lowassa kuondolewa kwenye kinyang'lo cha kugombea Uraisi, CCM iligawika makundimakundi hata kabla E.lowassa hajahamia upande wa pili, iliwapa shida Sana CCM kipindi hicho

Na baada ya maamzi ya Mh lowassa kutangaza kuhamia upinzani, wengi tuliamini huo ndio ulikuwa mwisho wa ccm, CCM washukuru kwamba waliyekuwa wamempitisha kuwa ndio mpeperusha bendera ya Uraisi, alibebwa na sifa zake binafs na sifa zake hizo ndizo zilizoibeba Ccm badala ya CCM kumbeba Magufuli, JPM ndio aliibeba CCM, na ndio maana hata Kampeni zake ilikuwa ( Chagua Magufuli) na si chagua CCM

Maana yake Huyu JpM alijibeba mwenyewe,

Nikurudishe kwenye hoja yako unayomshambulia JPm kwamba, eti alivyovifanya Vyote vilikuwa ni maono ya Jk, wewe unachokisahau ni kimoja tu na sina hakika unakisahau au tu Kwa sababu ya uharaka wa kuona makosa bila kujiuliza ni Nani anastahili kubebeshwa laumu hizo (makosa hayo)

Chama huandaa Ilani ya miaka mitano mitano, na nilazima Wakati wanaandaa Ilani hizo wajiridhishe kwamba zitatekerezwa zote Kwa kipindi hicho cha miaka mitano!!!

Sjui unanielewa, baada ya Ilani hizo kukamilika, hupew la anayewania nafasi ya Rais ili kunadi Sera hizo akiwa na uhakika atazifanya, sasa ikitokea hakuna utekerezaji wa Ilani hiyo, ama utekerezaji umekuwa busu, bado mambo hayo yaliyoahidiwa yatabaki kuwa deni Kwa Chama na si Kwa aliyekuwa Raisi,. Ni lazima ahadi hizo zitekerezwe Kwa awamu itakayofuata, na ndicho alichokifanya Mh JPM, alipewa viporo vilivyowashinda awamu iliyopita na mambo mapya mengine ya kutekerezwa

Sasa unapokuja kumlaumu Magufuli eti kwamba hajafanya zaidi Sana kafanya mambo ya kikwete ni kumwonea, Abayetakiwa kulaumiwa ni huyo Kikwete kwamba, Kwa nini hakuyafanya ktk vipindi vyake ikiwa Ilani ya uchaguzi huwa na vitu fanywa vya miaka mitanomitano??

Licha ya kufanya viporo lakini pia karibu asilimia zote kafanya yote aliyokuwa akiyanadi kuwa atayafanya, na ameenda mbali zaidi kufanya hata Yale ambayo hayakuwa kwenye Ilani ya CCM, utamlaumje huyu mtu

Kwenye swala la ujenzi na usimamizi, wa fedha, kivyovyote Mimi Magufuli namweka kuwa ndiye Raisi pekee Tanzania aliyeweza kusimamia vizuri kuliko maraisi wote Tanzania Kwa sasa

Swala la Nani atashindana naye ktk uchaguzi mwaka huu, Kwa kifupi na Kwa haraka Sana, atakayepatikana Kutokea upinzani yeyote Yule, hamuupendi ukweli, sasa nakwambia na nasisitiza kwamba, Watashindana lakini hawatashinda, shikilia Hilo mkuu, wembe ni uleule uliombeba JpM Kwa uchapa kazi wake ndio huo tena utambeba, Asante
 
kama ni kweli,Chadema watakuwa wamefanya uwamuzi wa KIPUMBAVU.
 
unamtaka wewe na nani? watu wa kyeboard mnashida sana
 
Magazeti ya kujisaidia chooni bwana. Sasa huu utumbo nao mods mmeuacga humu??
 
A bulk junk of waste

Jr[emoji769]
 
Chadema bhana,si ajabu wakabadili gia angani.
DEREVA MJANJA SIKU ZOTE HATUMII USUKANI WALA KUTEGEMEA MATAIRI YA GARI LAKE KUENDESHEA GARI,ILA HUTUMIA INJINI ISIYO NA MAFUTA KULIFANYA GARI LAKE LIKAPAA KULIKO KUTEMBEA,DEREVA HUYO HUYO,DEREVA HUYO HUYO ANAPOONGOZA MELI BAHARINI,HUELEKEA UPANDE AMBAO KUNA PAPA NA SIYO KUWAKWEPA POMBOO.
 
Anachopanga Mbowe wafuasi hamna la kupinga
Akifanya ya 2015 atapiga kura mwenyewe.
Ni bora ampe Nyarandu kuliko Membe kwani Nyarandu amefanya kazi kubwa kuijenga CHADEMA kanda ya kati.
Wafanye utafiti ni nani wanachama wa kawaida wanamuhitaji. Niwahakikishie this time akimpokea Membe atazomewa kwenye kampeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…