Uchaguzi 2020 Bernard Membe alijitoa kugombea Urais kupitia ACT-Wazalendo tangu Septemba 24. Barua yake ilikataliwa

Uchaguzi 2020 Bernard Membe alijitoa kugombea Urais kupitia ACT-Wazalendo tangu Septemba 24. Barua yake ilikataliwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Aliyekuwa mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo aliandika barua kujiondoa rasmi kugombea nafasi hiyo. Hata hivyo, barua yake ilikataliwa.

Barua ambayo imesambaa mtandaoni imeonyesha hivyo na Kiongozi wa chama, Zitto Kabwe ameithibitishia JamiiForums kuwa ni barua ya kweli na kuwa iliandikwa baada ya kuafikiana kama chama juu ya kugombea nafasi ya Urais tangu mwishoni mwezi Septemba mwaka huu.

Hata hivyo, baada ya kumtafuta Ndg. Bernard Membe, amekiri barua aliiandika kweli lakini ilikataliwa.

556485FC-01A3-48AD-8D40-7702916170B1.jpeg


Tumemtafuta Bernard Membe na amesema atatoa ufafanuzi mwenyewe kupitia akaunti yake ya Twitter.

UPDATE:

DED6BDA5-FE8A-4EEB-9130-8D00DD33894E.jpeg
 
Daaah kumbe walishajipanga kumwachia Lissu kivingine. Ila barua mbona ni ya toka 24th September? Tume haikujulisha wananchi?

Ila nimeona wanachama wengi ACT na bendera zao wakiwa mikutano ya Lissu. Siasa ni kiboko.
 
Nikishasaini Kwa Kalamu Nyekundu Pale Taifa
Nakwenda Kula Chakula Kitamu Na Mke Wangu Hotel
Maalim Seif Na Zito Walishaona Mbali Wakasema Kura Apewe Lissu, Anajitoa Saa Hizi Wakati Dakika Ya 89 Bado

Ukiwa Pandikizi Unaishi Kwa Tabu Sana, Sasa Afanye Arudi Ccm Haraka Sana Awahi Teuzi Kule!!😁😂😅😄😏
Niguse Ninuke!!😀😁😂 Hujatisha Ila Umejitweza
 
Back
Top Bottom