Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,320
- 18,852
Huyu jamaa, ‘jasusi mbobezi’, hana kabisa mvuto akiwa jukwaani.
Siasa kwake naona si jambo alilonalo kiasili.
Anajitahidi sana kuongea na kudondosha vibwagizo akiwa jukwaani, lakini wapi! Hamna kitu kabisa.
Maneno hayamtoki mdomoni kiulaini. Linganisha Lissu akiwa jukwaani na huyo Membe, ni usiku na mchana.
Sauti haina mvuto. Hana msamiati wa kutosha wa kuchotea vibwagizo kuendana na hadhira iliyo mbele yake.
Anachokiweza ni vijembe vya kimafumbo huko Twitter.
Hana bashasha......mashamsham wala machejo yoyote.....
Hana amsha amsha kabisa.......hasisimui......