Kikwete anawazidi wote Lissu, Magufuli, Membe..
Charisma na mvuto Tz since independence ni Nyerere na Kikwete
Waliosalia wote wanababia babia
Mkuu huu mchango wangu unaweza kuwa mgumu sana kwa wengi kuuelewa lakini nimeupata kwa Magwiji wa masuala ya communication na bahati mbaya sio watanzanaia, na waliniambia hivi.
" mawasiliano ya ueleweke na uaminike kisiasa inategemea uko wapi? unaongea na nani? na wakati gani? wewe ni nani?"
Huyu mtu wenu anaongea kama ni mshamba anaaminika zaidi na washamba wote na wa makabila yote kuliko wale wenye kuongea kimjini. Yuko kama wao, anafanana nao, anazungumza kama wao,wamekutana na watu wengine wanao fanana nae. Atapata taabu kama asili ya watu anakotoka ni watu hawaaminiki lakini kama kabila au sehemu anayotoka ni jamii isiyo na mawaa, wasikilizaji watakuwa wanamfananisha na tabia ama nzuri, ama mbaya kufuatana na jamii anayotoka.
Ukiwa mu-Ibbo watakufananisha na wa-Ibbo wanafahamika kivipi. kama ni wezi utahesabiwa na wewe ni mwizi, kama ni wema na wewe utahesabiwa hivyo hivyo.
Ndio maana wahubiri dunia nzima wana mfumo wa kuhubiri ambao unawavuta watu na kuwaamini.
Makasisi- wana mfumo na sauti ya kuwasiliana na flock ambao wata waamini na kuwavutika. Na nikapewa mifano mingi tuu.
Kwa hiyo kulitawala jukwaa inategemea wew ni nani na jamii unayo ongea nayo.
Nikaambiwa ushishangae Mzee Kikwete anaweza akashindwa vibaya kwa washamba kuliko huyo mshamba wako unae muona hawezi kuongea vizuri anapo ongea na washamba wenzake.
Nikaulizwa kabila nikasema wakasema inakuwaje? Nikawaambia sisi Upareni ukiongea Kiswahili bila lafudhi ya Kipare, huitwa Myika huyo. Na maana halisi ya Mnyika ni mtu yeyote ambae hayuko kama sisi, kwa hiyo lazima jihadhari nae kwa kuwa hufanani nae na humjui.