Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Hatoki mtu hapa kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Septemba 15 kinaanza kimbunga kumbakumba

Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Hatoki mtu hapa kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Septemba 15 kinaanza kimbunga kumbakumba

KWAKWELI NAWAPONGEZA CCM KWA KUMFUKUZA KWENYE CHAMA HUYU JAMAA. FIKILIA LEO HII TUNGEKUWA NA MGOMBEA HUYU KWENYE CHAMA CHETU CHA CCM, MBONA TUNGETIA HURUMA KAMA CHADEMA. YAANI NI AFADHALI UMSIKILIZE HASHIM LUNGWE WA CHAUMA, KULIKO HUYU JAMAA.
PONGEZI ZIWAENDEE CCM KWA KUMTIMUA MAPEMA
 
Mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo ambaye hapo kabla alikuwa mwanachama wa CCM Bernard Membe ametema nyongo baada ya maneno kuwa mengi yakimtaka aachie nafasi ya kinyang'anyiro cha urais na kumuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Tundu Antipas Lissu ambaye amemuunga mkono mgombea wa ACT upande wa Zanzibar Maalim Seif Shalif Hamad.

Kupitia maneno kuwa mengi leo shushushu mbobezi kama wanavyomuita amefunguka na kusema "HATOKI MTU HAPA!"

View attachment 1564225

"wote wanaodhani kuwa Nitajiondoa katika kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, wanaota ndoto za Mchana. Kimbunga kitakachoanza tarehe 15 September 2020 October ni Kimbunga kumba-kumba! Watanzania kaeni chonjo!"

Maneno hayo yanaonyesha kuna kitu kikubwa ambacho wafuatiliaji wa siasa za ndani hasa kipindi hiki cha uchaguzi wanasubiri kwa hamu na kutaka kujua kulikoni!.

Aidha ni wale vigogo/vizito zaidi ya saba ambao aliahidi wanaondoka CCM na kwenda kumpa nguvu pale alipo au ni kitu gani kipya kinaenda kukumba kampeni hizi nzito za mwaka huu 2020!.
Kibaraka tu huyo atupishe
 
Kuna game linatengenezwa ambalo ndiyo kaburi rasmi ya CCM before 28th October.

Stay turned... kauli ya Lissu Zanzibar na ukimya wa ACT si mwa bahati mbaya
ukiona choo ndotoni usikitumie
 
Ujio wa Lissu nchini, na kitendo cha Lowasa kuwasaliti wapenda mabadiliko, kumechangia sana kufifishwa kwa nyota ya Mh. Bernad Membe.
 
Kuna game linatengenezwa ambalo ndiyo kaburi rasmi ya CCM before 28th October.

Stay turned... kauli ya Lissu Zanzibar na ukimya wa ACT si mwa bahati mbaya
Nakuelewa mkuu ngoja tusubiri ni kesho tu...
 
HATOKI MTU HAPA! Wale wote wanaodhani kuwa Nitajiondoa katika kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, wanaota ndoto za Mchana. Kimbunga kitakachoanza tarehe 15 September 2020 October ni Kimbunga kumbakumba! Watanzania kaeni chonjo!

Kaza buti twende baba.
 
Sioni kwanini Membe amuunge mkono Lisu. Hawa watu wa ccm ndio huwa wanavuruga upinzani. Nimefurahi sana yeye kugoma kumuunga mkono Lissu, maana huko mbele ya safari ndio huwa wanaingia kwenye vikao vya siri vya chadema na kujifanya ni washirika wa upinzani, kumbe ni mashushu uchwara wa CCM.

Mtu kaitumikia CCM zaidi ya miaka 40 leo mnataka awe sehemu ya upinzani!

Hata huko Zanzibar anayeungwa mkono na CHADEMA ni Maalim Seif, kwakuwa ni mpinzani wa kweli na sio chama cha ACT.
Tundu na wafuasi wa CHADEMA ndio wanalialia Membe awasaidie
 
HATOKI MTU HAPA! Wale wote wanaodhani kuwa Nitajiondoa katika kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, wanaota ndoto za Mchana. Kimbunga kitakachoanza tarehe 15 September 2020 October ni Kimbunga kumbakumba! Watanzania kaeni chonjo!

Kimbunga gani? Hiki ndio kimbunga?
 

Attachments

  • 2508706_65516dc9-4f6f-4565-aabf-2d87c35b06e5.jpg
    2508706_65516dc9-4f6f-4565-aabf-2d87c35b06e5.jpg
    50.2 KB · Views: 1
Bahati nzuri Membe ana sura nzuri Mashaallah lau kana sura yake imeanza kusawajika na kupoteza nuru siku za hivi karibuni ila Bahati mbaya sana Membe huyohuyo hana mvuto kabisa wa kisisasa.Jina lake lilivyokuwa linavuma kwa siku nyingi ni tofauti kabisa na mtu mwenyewe alivyo kwa sasa. Inawezekana huyu siyo mwanasiasa kabisa ila mtu wa kukaaa ofisini tu . Hata kama kuna mtu aliyembeba miaka yote hiyo katka utendaji wake ninampongeaza sana.

Kutokana na wanasiasa wengi wa ccm kutegemea vyombo vya dola, inakuwa ngumu kwa wanasiasa kutoka ccm kuweza kufanya siasa, nje ya mbeleko ya vyombo vya dola. Sio kwamba hawawezi, ila ni ngumu sana kwao kufanya siasa zisizo na upendeleo.
 
Back
Top Bottom