Lugha anayoongea Membe ya ' utaratibu wa ovyo ushamba na upumbavu' siyo lugha yenye taadhima kwa mtu tunayeambiwa eti ni mwanadiplomasia aliyebobea.Kwa kweli anavyoongea ni mtu aliyekata tamaa kabisa ambapo nadhani huko baadae atahitajika kupata tiba ya kisasikologia. Huu mfumo ndani ya chama cha mapinduzi wakati wa kuchukua fomu katika awamu ya miaka mitano ya mwisho ya urais haujaanzia kwa Magufuli.Membe anaongea kwa hisia na chuki kali sana wakati mfumo huo walikaa nao kwa miaka yote.Kwa hili Membe nia yake ni kuleta fujo tu.Kwa nini asingeenda basi Dodoma awaambie wampe fomu kwa sababu anadai hajafukuzwa kwenye chama? yeye si anajinasibu kwamba ni mtu anayejiamini ? Sidhani ,Membe ni Mwoga tu.Kama ana hao wafuasi wengi si ameshakaribishwa kwa Zitto Kabwe aende akagombee huko ?
Kwa kifupi Membe ,Tanzania yote sasa hivi ipo na Magufuli.Hata huko kusini unaposema ni kwenu watakushangaza.Magufuli siyo namba ya kawaida kwa sasa hapa Tanzania.
Tunasikia eti una nasaba na Rais wa awamu ya nne lakini matarajio yako yaligonga mwamba wakati ule na hakuweza kukusaidia kwa lolote.
Badala ya kuongea maneno ambayo hayana taadhima kwa hadhi yako ,nenda chama kingine ujaribu au muombe Mungu wako CCM wakusamehe halafu ujipange kwa 2025 ,siyo mbali ,hapo utajua kwamba unakubalika au vipi kwa sababu mtachukua fomu zaidi ya watia nia 40.Na kwa tabia hii unayoijenga kwa sasa,ukichukua fomu 2025 ndipo utakapojua kwa nini wimbo wa taifa hauna Video.