Bernard Membe rasmi ACT Wazalendo, kutambulishwa kesho

Bernard Membe rasmi ACT Wazalendo, kutambulishwa kesho

Kosea Kuoa Ila Siyo Kuchagua

Ukikosea Kuoa Mke Mnaweza Kuachana Muda Huo Huo
Lakini Ukikosea Kuchagua Hadi Miaka 5 Iishe!!!
😀😁😂😅😄😄😃😃
 
Yale yale ya lowasa baada ya kushindwa mwenyewe atarudi chamani
 
Membe kafukuzwa lowasa hakufukuzwa...
Membe na Lowassa wote wana mangumashi mengi ambayo ili kuyalinda lazima wawe CCM, ngoja "kesi" za Membe and Co. Ltd zianze uone moto wake! Afrika kuna mazingaombwe na sio siasa!
 
Ndugu wana jamvi,

Kuna hiki kinachoendelea ndani ya bongo politics. Tuliyashuhudia ya EL sasa ni zamu ya MB.

Swali la msingi la kujiuliza je kuondoka kwao ccm ni kunafanana kwa maana membe ameondoka km lowasa na atarud km lowasa au kuna tofauti kati yao?
Moja alisema maadui zake watakimbilia nairobi vile sasa sijui yeye atakimbilia zombe
 
Ni haki yake, ila tuseme ukweli kidogo, Membe ana ubongo mzuri, kama umemsikiliza vema akiongea na Mwanahalisi online, IQ yake vizuri, ingawa ameondoka CCM, nimtakie kila la kheri, after all ni maisha, duniani hapa, hivyo Mungu akubariki huko ACT Wazalendo.
 
Hata Kama akirudi ccm poa tu cha msingi amtikise jiwe maana jiwe anajiona yeye ndo mungu wa wadanganyika
 
Wewe umeaje kwamba Zitto hataki ushirikiano?

Nimemsikiliza Membe akihojiwa na Kubenea amesema yupo tayari kumuunga mkono mgombea yoyote anayekubalika zaidi ndani ya upinzani,na Zitto anaongea nauli hiyo hiyo.

Labda CHADEMA haipo tayari kumuunga mkono mgombea wa ACT? Kama ni hivyo huo ni ubinafsi ni bora kila chama kisimame kivyake ili kujijenga. CCM haiwezi kutawala milele nchi hii lazima itadondoka tu.
Hivi wakatinaamviwa hamuwezi kuungana kwani mda hautoshi hamkusikia?

God save us
 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika ukurasa wake wa Twitter amepakia picha akiwa anatabasamu huku akiwa ameshika Katiba ya chama cha ACT Wazalendo . Je, inaashiria kwamba amehamia katika chama hiki? Ikumbukwe Membe amefukuzwa kwenye chama cha Mapinduzi siku za hivi karibuni.

Amenukuliwa mara kwa mara akitaka kugombea Urais wa JMT.

View attachment 1507326


=====================================​
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameweka wazi kuwa kesho Julai 16, 2020 watamtambulisha rasmi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho baada ya kufukuzwa na chama chake cha zamani (CCM).

Zitto ameweka wazi hayo kwenye ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa twitter akiwa ameweka picha ya Membe huku akiwa ameshikilia kitabu cha ACT-Wazalendo.

Kwa muda mrefu sasa Bernard Membe amekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye chama cha ACT wazalendo baada ya kufukuzwa CCM baada ya kukiuka baadhi ya taratibu za chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mwanahalisi Membe atatambulishwa kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mlimani City mbele ya wanachama wa chama hicho.
Cut9c9
 
Back
Top Bottom