Bernard Membe rasmi ACT Wazalendo, kutambulishwa kesho

Bernard Membe rasmi ACT Wazalendo, kutambulishwa kesho

Atakula mkong'oto huyu mpk Piko anayopaka kichwani itaisha.

BTW huyu si amekuja kufanya divide&rule hatapewa kashikashi zozote nzito.
Si mlisema akiguswa ananuka? Huko ndio kunuka kwenyewe ama? [emoji23][emoji23][emoji23]
Bongo raha sanA

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Hayo ya kunuka itakua mliyasema huko Ccm kwny kikao cha NEC.
Mlikuwa mnamshabikia na kumpa kichwa kwamba yeye ni kachero mbobevu hakuna wa kumgusa. Huku yeye akichagiza huku twitter kwamba niguse ninuke,!
Je, kunuka kwenyewe ndio huko?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Mlikuwa mnamshabikia na kumpa kichwa kwamba yeye ni kachero mbobevu hakuna wa kumgusa. Huku yeye akichagiza huku twitter kwamba niguse ninuke,!
Je, kunuka kwenyewe ndio huko?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
Wana CCM Mlikua mnamshabikia sana mkisema huyu jamaa ni mbobevu huku mkilalamika mmechoka kuburuzwa na Mwenyekiti wenu bora jamaa nae achukue form ila bahati mbaya chama kika-print form 1.
 
Zitto anatapatapa kuokoteza magarasa. Tulimwona alipomtembelea Lissu huko Ubelgiji na kutuaminisha kwamba Lissu atajiunga na ACT. Sasa kampata Membe kuchuana na Lissu kwenye ugombea urais. Tusubiri tuone nani atapata kura nyingi kati ya Membe na Lissu kati ya hizo asilimia 1% ambazo JPM atakuwa amewaachia.
 
Yaani CDM Ilijiandaa kutorudia ya EL lakini toka awali ACT ilionesha nia ya kuungana na CDM sahizi membe anaenda kupitishwa ACT. Utata utibuka mgombea wa chama gani aungwe mkono?

Tamaa ya hela inaweza pelekea CDM kuunga kwa mgombea wa ACT Kitu ambacho kitakuwa wamekwepa kuipokea zero
 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika ukurasa wake wa Twitter amepakia picha akiwa anatabasamu huku akiwa ameshika Katiba ya chama cha ACT Wazalendo . Je, inaashiria kwamba amehamia katika chama hiki? Ikumbukwe Membe amefukuzwa kwenye chama cha Mapinduzi siku za hivi karibuni.

Amenukuliwa mara kwa mara akitaka kugombea Urais wa JMT.

View attachment 1507326


=====================================​
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameweka wazi kuwa kesho Julai 16, 2020 watamtambulisha rasmi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho baada ya kufukuzwa na chama chake cha zamani (CCM).

Zitto ameweka wazi hayo kwenye ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa twitter akiwa ameweka picha ya Membe huku akiwa ameshikilia kitabu cha ACT-Wazalendo.

Kwa muda mrefu sasa Bernard Membe amekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye chama cha ACT wazalendo baada ya kufukuzwa CCM baada ya kukiuka baadhi ya taratibu za chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mwanahalisi Membe atatambulishwa kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mlimani City mbele ya wanachama wa chama hicho.
Barakoa zitaweza kuhimili moshi na pilipili? Na umeme utakuwepo?
 
Back
Top Bottom