Si mlisema akiguswa ananuka? Huko ndio kunuka kwenyewe ama? [emoji23][emoji23][emoji23]Atakula mkong'oto huyu mpk Piko anayopaka kichwani itaisha.
BTW huyu si amekuja kufanya divide&rule hatapewa kashikashi zozote nzito.
Hayo ya kunuka itakua mliyasema huko Ccm kwny kikao cha NEC.Si mlisema akiguswa ananuka? Huko ndio kunuka kwenyewe ama? [emoji23][emoji23][emoji23]
Bongo raha sanA
Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
Mlikuwa mnamshabikia na kumpa kichwa kwamba yeye ni kachero mbobevu hakuna wa kumgusa. Huku yeye akichagiza huku twitter kwamba niguse ninuke,!Hayo ya kunuka itakua mliyasema huko Ccm kwny kikao cha NEC.
Tatizo Watanzania tunapenda mabadiliko Ila hatuwapendi wanaojaribu kutuletea hayo mabadiliko
Wana CCM Mlikua mnamshabikia sana mkisema huyu jamaa ni mbobevu huku mkilalamika mmechoka kuburuzwa na Mwenyekiti wenu bora jamaa nae achukue form ila bahati mbaya chama kika-print form 1.Mlikuwa mnamshabikia na kumpa kichwa kwamba yeye ni kachero mbobevu hakuna wa kumgusa. Huku yeye akichagiza huku twitter kwamba niguse ninuke,!
Je, kunuka kwenyewe ndio huko?
Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
Barakoa zitaweza kuhimili moshi na pilipili? Na umeme utakuwepo?Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika ukurasa wake wa Twitter amepakia picha akiwa anatabasamu huku akiwa ameshika Katiba ya chama cha ACT Wazalendo . Je, inaashiria kwamba amehamia katika chama hiki? Ikumbukwe Membe amefukuzwa kwenye chama cha Mapinduzi siku za hivi karibuni.
Amenukuliwa mara kwa mara akitaka kugombea Urais wa JMT.
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameweka wazi kuwa kesho Julai 16, 2020 watamtambulisha rasmi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho baada ya kufukuzwa na chama chake cha zamani (CCM).
Zitto ameweka wazi hayo kwenye ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa twitter akiwa ameweka picha ya Membe huku akiwa ameshikilia kitabu cha ACT-Wazalendo.
Kwa muda mrefu sasa Bernard Membe amekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye chama cha ACT wazalendo baada ya kufukuzwa CCM baada ya kukiuka baadhi ya taratibu za chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mwanahalisi Membe atatambulishwa kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mlimani City mbele ya wanachama wa chama hicho.