Bernard Membe: Tanzania diplomasia imeshuka awamu hii. Tutatengwa na majirani wakiona hatufuati vigezo vya WHO kupambana na COVID19

Bernard Membe: Tanzania diplomasia imeshuka awamu hii. Tutatengwa na majirani wakiona hatufuati vigezo vya WHO kupambana na COVID19

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,427
Reaction score
4,944
Akihojiwa na DW, waziri wa zamani wa mambo ya nje mheshimiwa Bernard Camilius Membe amesema katika awamu hii ya utawala wa Magufuli, diplomasia imeshuka mno.

Membe anaonya kwamba, tanzania awamu hii inajiendeshea mambo kivyakevyake nje ya utaratibu wa jumuia ya kimataifa.

Akoingelea suala la korona, Membe amedai kuwa Tanzania haiheshimu na imejitenga na miiko ya shirika la afya WHO.

Chanzo: DW
=====

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amezungumzia uhusiano wa Kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na nchi za jirani katika kipindi hiki cha mlipuko wa #COVID19

Amesema kwasasa nchi zipo katika mapambanao dhidi ya #CoronaVirus na dio maana nchi kama Zambia zinafunga mipaka yake na kuzuia watu waziende ikiwa ni njia ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo kutoka sehemu moja

Amesema "Kama Zambia wamefunga mpaka wake na kuzuia magari yasipite, huo ni mkakati na hatua ya kuzuia maambukizi ya #COVID19 na ndio maana inatakiwa tufanye mambo haya kwa pamoja kwa pande zote mbili"

Aidha, kuhusu kupimwa kwa Madereva wa Tanzania wanaotaka kuingia Kenya, amesema kidiplomasia ni kwamba nchi za jirani zina wasiwasi sana kwamba Tanzania inaweza kuwa inapeleka ugonjwa huu kwenye nchi fulani

Ameeleza "Wasiwasi huu unaweza kuwa unakuja baada ya kuona pengine hatufungamani ni vigezo vya WHO ambavyo vimewekwa na dunia nzima vinavifuata labda mpaka pale tutakapofungamana na vigezo vya WHO wanavyofuata wenzetu"

Ameongeza "Kwa na mna Tanzania inavyoshungulikia jnaga kama hili tutatengwa, majirani watatutenga na kutengwa ni kwa namna hii ya kufunga mipaka na kidiplomasia tunasema mtengano huu unatumiiza na kututesa zaidi sisi kuliko majirani"

Amemalizia kuwa ni kweli diplomasia imeshuka kwasababu awamu hii haijengi kwenda na dunia inaangalia zaidi matatizo ya ndani na ina athari zake hasa tukipata janga hili na ndio maana tunasema diplomasia imeshuka sana
 
Nimesikilza
Kwa makini mahojiano hayo,yalipangwa na DW na ni bias kabisa
Nasema hivyo kwa sababu eti ni Watanzania tu pekee ndio tutaathirika wakati hata Zambia wataathirika tena pakubwa kuliko sisi watanzania kwa sababu asilimia 70 %ya mizigo ya Zambia inatoka Tanzania
 
Nchi ya Viawanda inakosa hat akilo moja ya sukari hahahahaa tunadili na Wapinzani. Sasa tunatengwa na na majirani zetu. Hakuna mjadala serious kuhusu mambo yanayotokea nchini kila mtu anatetea uhai wake, njaa yake, familia yake.

Nani atasimama ahesabiwe kwa kalamu ya moto na damu tuikoe Tanzania? Karibuni kwa kejeli na matusi
 
Kichaa huyo kwani wakt wanagombea chakula na mzee wa monduli walitegemea nn badala kukaa chini km watu wazima waongee walileta ubinafsi walitegemea tutaumia sie wacha tusome number wote mwenzie mkwewe sijui mwaka wangapi huu yupo Segerea pamoja kurudi nyumbani jamaa bado amekaza...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akihojiwa na DW, waziri wa zamani wa mambo ya nje mheshimiwa Bernard Camilius Membe amesema katika awamu hii ya utawala wa Magufuli, diplomasia imeshuka mno.

Membe anaonya kwamba, tanzania awamu hii inajiendeshea mambo kivyakevyake nje ya utaratibu wa jumuia ya kimataifa.

Akoingelea suala la korona, Membe amedai kuwa Tanzania haiheshimu na imejitenga na miiko ya shirika la afya WHO.

Chanzo: DW
Vitu vingine vinatia hasira!! Miiko gani tumejitenga nayo? Kuna chuki Kali sana dhidi ya Tanzania isiyokuwa na sababu!! Kinachowakasirisha zaidi ni kutuona tunadunda na tunaendelea na shughuli zetu!! Walitazamia tufe kwa maelfu na haijawa hivyo!! Inawauma sana!!!

Rais wetu Dr Magufuli mamilioni ya watanzania tunakushukuru sana kwa uongozi wako katika kipindi hiki ambacho vinginevyo tungepita kwenye ugumu sana!! Tukikushukuru watanzania ikutoshe maana hao mabeberu na vibaraka wao hatutegemei kama wanaeeza kukiri uongozi wako imara japo nafsini mwa o wanajua hivyo! Mungu yuko upande wetu ndio maana matazamio yao hayajafanikiwa!!
 
Bila kupata taarifa unajuaje kama hatufi kwa maelfu?
 
Hivi kuna Mwafrika Anaweza kuishi bila beberu?

Huko Zimbabwe kwa sasa wanapambana kurudisha uchumba wao na Mabeberu

Hao mabeberu ndio wanakufanya uweze hata kuiona JF kwenye simu yako
Mtumwa wa fikra utamtambua tu!! Hata akiwa na uwezo namna gani bado hawezi kujiamini!! Tunaishi kwa kodi zetu pamoja na kwamba mabeberu wametupora sana!! Wanakasirika sana kuona ofisi namba moja haiingiliki!!
 
Nimesikilza
Kwa makini mahojiano hayo,yalipangwa na DW na ni bias kabisa
Nasema hivyo kwa sababu eti ni Watanzania tu pekee ndio tutaathirika wakati hata Zambia wataathirika tena pakubwa kuliko sisi watanzania kwa sababu asilimia 70 %ya mizigo ya Zambia inatoka Tanzania
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ndipo mnapojidanganya!
Hakuna Bandari zingine kwani Africa?
 
Nimesikilza
Kwa makini mahojiano hayo,yalipangwa na DW na ni bias kabisa
Nasema hivyo kwa sababu eti ni Watanzania tu pekee ndio tutaathirika wakati hata Zambia wataathirika tena pakubwa kuliko sisi watanzania kwa sababu asilimia 70 %ya mizigo ya Zambia inatoka Tanzania
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha upumbav.u wewe, asilimia 70 ya wapi? Umewahi kuyaona malori ya Zambia yanayotoka South Africa?..Hivi unajua Dar Lusaka ni mbali kuliko Lusaka Johburg kwa ubora wa barabara n.k? Uwe una-google mambo mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe atupumzishe tu aseme amemis safari za nje kwa kodi ya serkali

Hizo zingine ni kisingizio tu
 
Mtumwa wa fikra utamtambua tu!! Hata akiwa na uwezo namna gani bado hawezi kujiamini!! Tunaishi kwa kodi zetu pamoja na kwamba mabeberu wametupora sana!! Wanakasirika sana kuona ofisi namba moja haiingiliki!!

Lowasa alisema elimu elimu
 
Back
Top Bottom